CAG Mstaafu amsifu Mkulima aliyewaburuza kortini wabadhirifu waliotajwa na CAG

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesifu uamuzi aliouchukua mkulima Thomas Nkola, kuamua kufungua kesi mahakamani kushinikiza waliotajwa kuhusika na ubadhirifu wa mabilioni katika ripoti ya mwaka 2021/22 ya CAG kuchukuliwa hatua.

Nkola, mkulima na mkazi wa Mtaa wa Majengo wilayani Maswa mkoani Simiyu, ameamua kufungua kesi hiyo kwa kuzingatia Ibara ya 27(I) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Ibara ya 27(1) inatamka: "Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine."

Ibara ya 27(2) inatamka: "Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao."

cHANZO: Nipashe

Pia soma > Ripoti ya CAG: Mkulima kuwafungulia kesi vigogo Mwigulu, January, Kabudi na Mbarawa
 
Nchi ngumu sana hii utashaa wavaa suti nyeusi wanakwenda kumshika mkulima kwa kuwazalilisha wateule wa Honorable causa
 
Nashauri JF tupendekeze aina ya Tuzo ya kumpa mkulima huyu kwa ushujaa huu alioonyesha.
Au tutoe tamko rasmi la kumpongeza. Najua wapo wale wahafidhina watapinga hili
 
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesifu uamuzi aliouchukua mkulima Thomas Nkola, kuamua kufungua kesi mahakamani kushinikiza waliotajwa kuhusika na ubadhirifu wa mabilioni katika ripoti ya mwaka 2021/22 ya CAG kuchukuliwa hatua...
Ludovick anajikosha tu maana hapa juzi ametoa maneno ya kusifia hao wabadhirifu.
 
Back
Top Bottom