CAG: Bwawa la Nyerere liliharakiswa

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,292
2,000
Ripoti ya CAG inatanabaisha sintofahamu kuhusu UTARATIBU wa ujenzi wa Bwawa la umeme la Nyerere mto Rufiji.. mfano,

1. Ujenzi wa bwawa ULISIMAMA KWA MIEZI MI(5) Baada ya kuta za bwawa kugharikishwa na maji. Sababu iliyobainishwa na CAG ni kuwa plan ya ujenzi ya 2017 ilitaka mikondo miwili ya kuchepushia maji(lita elfu7/sekunde) lakini ukajengwa mkondo mmoja kuchepusha lita elfu6 hali iliyopelekea ukuta kuzidiwa na kubomoka na kazi kusimama miezi mi5!

Walipoulizwa kwanini hawakufuata plan ya awali,2017 wahandisi walidai WANATAKA KUHARAKISHA MRADI!

2. Tanesco kama mmiliki wa Mradi ndio haohao wametoa mhandisi mshauri!

3. Inaonekana utaratibu wa ujenzi haufuati plan ya awali bali ni kuplan section flan na kujenga hapo hapo!(design and construct)!

4. Upembuzi yakinifu unaotumika ni uliofanyika miaka ya 1970, bila kuhuishwa kujua hali ya sasa kama athali za kimazingira za sasa!

Hayo ni baadhi tu ya mengi kuhusu Ujenzi wa Bwawa. Mwendo ukiwa huu wa kuplan ujenzi unavyoendelea basi kuna shaka juu ya usalama wa mradi na wa wananchi maeneo hayo na shaka juu ya tija ya mradi wenyewe!

Screenshot_20210411-172727.jpg
Screenshot_20210411-172631.jpg
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,305
2,000
Hapo anayebeba hilo zigo ni mhandisi mshauri. Alibadilishaje design bila kuwa na facts?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,204
2,000
Hapo anayebeba hilo zigo ni mhandisi mshauri. Alibadilishaje design bila kuwa na facts?

..wanasema walitaka kazi iende haraka.

..Magufuli, bila kuzingatia maoni ya wataalamu,alikuwa na tabia ya kulazimisha miradi imalizwe haraka-haraka kwa madai kuwa fedha zipo.

..bila shaka Tanesco walitaka kumfurahisha bwana mkubwa matokeo yake tumeingia HASARA.
 

Right3

Member
Aug 16, 2015
82
125
Naomba nisahihishe kidogo. Consultant wa mradi huu ni TANROADS hivyo alipaswa kuona hili chini ya usimamizi wa mwajiri ambaye ni TANESCO.

Ni kweli yalitokea haya lakini wakati tunaargue tufanye hivyo kwa utaalam kidogo kwani mkandarasi alitakiwa kuleta mitigating plan ya kufanya recovery ya muda uliopotea na alipeleka na naamini wanafanya kazi hiyo kwa mujibu plan ndio maana tukaambiwa muda wa kuisha mradi ni ule ule.

Wakati tunaona makosa amvayo tunafikiri yatamfanya mkandarasi aombe extension basi tujiulize ni jitihada gani zinafanyika kuzuia delay na je hiyo haijawahi kutokea katika mradi wowote iwe wakati wa Nyerere,Mwinyi,Mkapa au Kikwete.

Na hili lilikua kosa la mkandarasi pamoja na wasimamizi ambao ni TECU na TANESCO.

Haya mambo kwenye ujenzi yapo isipokua kwa mradi STRATEGIC km huu why TECU hawakuona hili.

Kwa kua Resident Engineer wa muda huo amefariki basi tumsamehe.

Kwa vile mitigation plan ilipelekwa basi wafanye kazi kwa bidii kuendana na plan. Kama watacope tutafurahi kwa kua tunauhitaji huo umeme wa bei nafuu.

Kuna miluzi mingi sana hichi kipindi kwa kua Magu is no more basi tumchallenge kwa facts na vile ambavyo kahusika moja kwa moja.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
9,731
2,000
Huo mradi usipoangaliwa kwa makini utakuja kusababisha maafa makubwa sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom