CAG Atilia Shaka Malipo ya Sh Mil 830.7 Clouds & TBC

interlacs

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
213
193
Ripoti ya CAG imeonesha kuwa Clouds FM na TBC walilipwa shillingi za Kitanzania zaidi ya Milioni 800 kwa ajili ya kutangaza tamasha la Urithi, lakini malipo hayo hayana ushahidi wowote as hawakuonesha risiti ya kielektroniki (source: CAG report, 08 Apr 2021).

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa kituo cha televisheni cha Clouds kililipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kiasi cha Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha la urithi lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo hayo.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

“Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani

-------
Kwa kuwa vyombo hivi vimekuwa mstari wa mbele kutetea wa nyonge na kuonyesha kuwa ni wazalendo, naomba wana JF wote tuwaombe warudishe fedha za wanyonge ili mama aendeleze kazi ya ujenzi wa nchi yetu. walijifanya wapo karibu na serekali ya awamu ya 5 kumbe ni mchwa.

Haiwezekani ku tweets tu ndo igharimu milion 600 zote hizo.

Rudisheni fedha zetu Clouds FM na TBC tafadhali
 
Maneno ya CAG 📚📚📚📚
Ingekua ni final exams Sasa wananchi tungekua tunasubiri hati safi na chafu tujue kina nani wame-Pass na kina nani wame-Disco

IMG-20210408-WA0016.jpg
IMG-20210408-WA0015.jpg
IMG-20210408-WA0014.jpg
IMG-20210408-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom