CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

Ilikua inakaguliwa ila ripoti wanaficha
Nadhani ilikuwa inakaguliwa kama sehemu ya utafiti ili kujiridhisha kama kuna faida au hasara.
Ola kilichofanyika Leo ni kuweka uwazi kwa wachangiaji wa ununuzi wake yaani walipa Kodi.
 
Kuna uzushi mkubwa uliletwa na Zitto kuwa kasma ya Atcl imehamishiwa ikulu ili watu waibe pesa sababu pesa za ikulu hazikaguliwi. Jambo ambalo lilikuwa sio kweli na wafuasi wa Chadema walikomaa sana juu ya ishu. Leo wameumbuka.
View attachment 1736519
Hata hivyo,hoja ya hasara iko palapale. Mbona huko nyuma hatukuambiwa ukweli huu kwamba shirika letu linapata hasara tu?

Mama hataki wapambe waganga njaa. Kamuagiza CAG afunguke zaidi. Aache kupakapaka rangi. Kama ni nyeusi....aseme nyeusi. Period.

Nimependa bure Madam President. Ameanza vizuri mno!
 
Acha kupotosha hapa.
Zito alisema Kasma ya ununuzi wa ndege za ATCL ilihamishiwa ikulu ili mchakato wa manunuzi yake usikaguliwe.

Sio kuwa shirika la ATCL lilihamishiwa kwenye Kasma ya Ikulu.
Mmeanza kubadili maneno?
 
Kuna uzushi mkubwa uliletwa na Zitto kuwa kasma ya Atcl imehamishiwa ikulu ili watu waibe pesa sababu pesa za ikulu hazikaguliwi. Jambo ambalo lilikuwa sio kweli na wafuasi wa Chadema walikomaa sana juu ya ishu. Leo wameumbuka.
View attachment 1736519
AIseee...
Yaani wewe umefurahi kuwa wamepata jibu KULIKO HUKO KUPATA HASARA...
Kuwa wamejibiwa hakuharibu huduma za kijamii, lakini kuwa inaendeshwa kwa hasara, maana yake kuna hela ingepataikana ya kuendeleza huduma za kijamaa lakini imepotelea hapo...
 
Kuna uzushi mkubwa uliletwa na Zitto kuwa kasma ya Atcl imehamishiwa ikulu ili watu waibe pesa sababu pesa za ikulu hazikaguliwi. Jambo ambalo lilikuwa sio kweli na wafuasi wa Chadema walikomaa sana juu ya ishu. Leo wameumbuka.
View attachment 1736519
Kamwe usingeusikia huo uchunguzi kurasa ingechomolewa hyo
Umesahau yaliyomkuta Assad
 
Kwani mashirika kama, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Malaysia na wao wanaendesha Kwa hasara??
Kama yanaingiza faida basi tatizo letu sio ndege....hayati alikua na malengo mazuri kufufua hilo shirika tujifunze Kwa hayo mashirika mengine wanapataje faida na sisi wapi tunakosea hadi tunakula hasara lakini sio kuacha kabisa hiyo biashara.
 
Sekta ya usafiri wa ndege imeathirika sio tu Tanzania ulimwenguni mwote
Haya mushaanza kuja na njia za kutetea kisichoweza kutetewa. Sekta ya usafiri duniani imeanza kuathirika miaka miwili iliyopita tu, jee sasa kwa miaka mitatu kabla ya hapo una sababu gani ya kutudanganya hapo?
 
Kuna uzushi mkubwa uliletwa na Zitto kuwa kasma ya Atcl imehamishiwa ikulu ili watu waibe pesa sababu pesa za ikulu hazikaguliwi. Jambo ambalo lilikuwa sio kweli na wafuasi wa Chadema walikomaa sana juu ya ishu. Leo wameumbuka.
View attachment 1736519
Sio Chadema walioumbuka, nazani umejisahaurisha!! lini ulisikia hesabu za shirika la ndege zikiwekwa wazi!!

Inawezekana shirika lilikuwa linakaguliwa, lakini baba suzan hakutaka hesabu ziwekwe wazi!! na alikuwa anafanya hivyo ili, kulinda uamuzi wa kununua ndege bila kufata taratibu.
Chadema hawajaumbuka, Ila ukweli tumeujua kuwa, shirika linajiendesha kwa hasara miaka mitano.
 
Back
Top Bottom