CAG apigwa kufuli

CAG apigwa kufuli

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
SERIKALI imewasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008, huku ikiongeza vifungu ambavyo vinapunguza nguvu ya Bunge katika kushughulikia taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Marekebisho hayo yamo kwenye Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria, namba 3 ya mwaka 2012 (The Written Laws - Miscellaneous Amendments Bill) uliowasilishwa bungeni jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CAG anawajibika kuwasilisha taarifa yake kwa Rais ambaye baada ya kuipokea atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha Bunge kilicho karibu.

Taarifa hiyo inabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.

Sheria ilivyo sasa inaelekeza kuwa baada ya ripoti hiyo kuwa silishwa bungeni itajadiliwa katika kamati tatu zinazosimamia Hesabu za Serikali kwa ajili ya kuifanyia uchambuzi, kisha kuwasilisha taarifa zake bungeni katika muda zitakazopangiwa.

Kamati hizo za Bunge ni zile za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Serikali Kuu (PAC) ambazo hufanya uchambuzi kisha kusoma taarifa zake ndani ya Bunge kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, marekebisho yaliyowasilishwa Bungeni jana na Jaji Werema yanapendekeza kubadili utaratibu mzima wa kushughulikia taarifa hiyo, kwani yanaongeza vipengele, "vinavyoliwajibisha Bunge kwa Serikali" badala ya kinyume chake.

Serikali imeongeza vipengele vya ziada ambavyo vinazitaka kamati za Bunge zinapofanya uchambuzi wa ripoti ya CAG, kupeleka maazimio yake kwa Serikali ili "yatafutiwe majawabu" badala ya utaratibu wa sasa wa kupeleka hesabu zake bungeni.

Kimsingi Kamati za Bunge hufanya kazi kwa niaba ya Bunge, hivyo taarifa zake husomwa Bungeni na siyo kwingineko kama ambavyo marekebisho ya sheria yanataka kuelekeza.
Jaji Werema alisema: "Marekebisho haya yamefanywa ili kumwezesha Waziri wa Fedha kuwasilisha taarifa ya majibu ya Serikali ya hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali".

Ikiwa Bunge litapitisha marekebisho hayo ni dhahiri kwamba Bunge halitakuwa tena na uwezo wa kuwawajibisha watendaji wa Serikali ambao watabainika kuhusika na upotevu wa fedha au kufuja fedha za umma, hivyo kupunguza uzito wa mjadala na uwezo wa wabunge kuhoji.

Kadhalika taarifa za LAAC, POAC na PAC kuhusu taarifa ya CAG na mapendekezo ya kamati hizo, yatajadiliwa sambamba na majibu ya Serikali. Hivyo hakutakuwa na nafasi ya Bunge kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Serikali kama inavyoainishwa katika Katiba.

Hatua hiyo ni sawa na kulifunga Bunge mikono kutokutekeleza wajibu wake kuhusu ripoti ya CAG, kwani kwa mujibu wa sheria halitaweza kujadili chochote hadi Serikali kupitia kwa Mlipaji Mkuu (Paymaster General) atakapokuwa ametoa majibu ya utetezi kuhusu kasoro katika ripoti hiyo


source: mwananchi gazeti.08/02/2013
 
... Serikali dhaifu inatafuta kila aina ya njia ili kuweza kujilinda na udhaifu wake.
Hii inaonyesha jinsi gani viongozi wa serikali wa wanavyotafuta mbinu chafu za kila aina ili kujinufaisha wao, ndugu na jamaa zao ili wanaendelea kuitafuna nchi yetu mpaka tone la mwisho.
Na wale wanaMagamba walioko mjengoni wataipitisha bila wasiwasi kwa sababu ya wingi wao.
Na kama kawaida utasikia Bi mkubwa akisema "sasa nina wahoji"
"Anayehafiki aseme ndiyo" hata kama hakuna aliyehafiki' na wengine wote wakasema "HAPANA" lazima bibi ataipisha.

Hili ni janga kubwa la kitaifa. Ccm wameona kuwa vitumbua vyao vinamwagiwa mchanga kila wakati.
Tunahitaji "PP" wakati huu na ujao, iwe na nguvu zaidi.
 
Hivi Tanzania tuna watu wanafikiria kwa kutumia nini? serikali inachosema hapo ni kwamba audit queries za CAG zisomwe pamoja na majibu ya serikali. tumeshuhudia bunge linapewa audit queries za mwaka uliopita ambazo by the time zinasomwa bungeni na kusikilizwa na wananchi unakuta marekebisho yalishafanyika au kama ni masurufu yanakuwa yamerudishwa... so whats wrong eith that. kinachopendekezwa hapa ni bunge na wananchi kupewa taarifa sahihi wakati CAG report ikisomwa bungeni na kwa wananchi.
 
nimeshasahau rekodi za bunge kuwawajibisha wafanyakaz wa serikali. kama majibu na ripoti vitawakilishwa haraka hamna tatizo. ila kwa ufisad ulivyo mwingi sidhani. wakikosa majibu ndo itakuwa vipi. wataipotezea?
 
mpaka 2015 tutaona mengi

mi naona tutakuwa tumeibiwa mpaka dudu zetu. Na hii inatokana na bunge kufanya kazi isiyokuwa yake ya kuitetea serikali. Huu ni upuuzi wa wezi wa mali za umma wanaotaka kuficha madudu yao yasifahamike. Ndo hapo ambapo jk huwa anafanya kinyume na yale anayoongea kwani alisema amemuwezesha cag kufanya kazi zake kwa uhuru kumbe ameagiza sheria ibadirishwe.
 
Hizi ni tik tak tu, wataondoka na sheria zitabadilishwa upya, waacheni wachezee hizi sheria kwa kuwa wana uwezo huo kwa sasa!
 
utaona mabunge ya maccm yanaunga mkono huo mswada tena mia kwa mia

Hi Great Thinkers,

Kwa watu makini tunajua kabisa ni nini kinakuja au kuandaliwa. Uchaguzi wa 2015 unakuja muda si mrefu(just a year ahead). Serikali ya CCM tayari wameshaanza MBINU ZA KUPATA FEDHA at any cost!!!

Lengo na mabadiliko ya Sheria hii ni kulinda WIZI ambao utaiwezesha CCM kupata mabilioni ya KAMPENI ZA UCHAGUZI 2015. Tunajua CCM lazima wawe na pesa ya kuwahonga wapiga kura kwanza na wawe na pesa ya kuwahonga UWT- mashushu ili waweze kuchakachua matokeo!!!
 
Aibu kwa serikali dhaifu namna hii.

Mjumbe naomba nitofautiane na wewe for the first time, na hii ni kwa sababu Mwananchi limepotosha ukweli. Mabadiliko haya yana tija sana kwa usimamizi wa serikali

Report zitatakiwa zipatiwe majawabu kwanza ndipo zipelekwa Bungeni ili bunge lichukue fursa ya kuwajibisha tu. tofauti na sasa ambapo bunge na kamati zake bado zinapoteza mda mwingi kuomba majibu na malimbikizo ya majibu ya miaka hata 5 ya nyuma. Inamaanishwa kuwa hakutakuwa tena na mambo ya ''rudini mkalete jibu hili, sijui karekebishe hiki''. No, badala yake ni kwamba kitakachopelekwa bungeni ni baada ya serikali kujibu ipasavyo na bunge litapitia hoja pamoja na majibu ya serikali na kuwajibisha kwenye mapungufu
 
Mjumbe naomba nitofautiane na wewe for the first time, na hii ni kwa sababu Mwananchi limepotosha ukweli. Mabadiliko haya yana tija sana kwa usimamizi wa serikali

Report zitatakiwa zipatiwe majawabu kwanza ndipo zipelekwa Bungeni ili bunge lichukue fursa ya kuwajibisha tu. tofauti na sasa ambapo bunge na kamati zake bado zinapoteza mda mwingi kuomba majibu na malimbikizo ya majibu ya miaka hata 5 ya nyuma. Inamaanishwa kuwa hakutakuwa tena na mambo ya ''rudini mkalete jibu hili, sijui karekebishe hiki''. No, badala yake ni kwamba kitakachopelekwa bungeni ni baada ya serikali kujibu ipasavyo na bunge litapitia hoja pamoja na majibu ya serikali na kuwajibisha kwenye mapungufu

Kwa hiyo unasema serikali inataka kufanya haya mabadiliko in good faith?

Kwamba kinachookolewa hapo ni muda? Really?
 
Hizi ni tik tak tu, wataondoka na sheria zitabadilishwa upya, waacheni wachezee hizi sheria kwa kuwa wana uwezo huo kwa sasa!

Tik tak kama hiyo avator yako...... this is Bongo land....
 
Kufuatana na mjadala unaoendelea sasa hivi Bungeni naona wabunge wa ccm wanatumia wingi wao kupitisha vifungu bila kusikiliza wapinzani mi naomba wakimaliza kikao cha Bunge watembee nchi nzima kuwaeleza wananchi upuuzi huo wa wabunge wa ccm na serkali yake.
 
Ngoja wataporudi majimboni ndio watajua nn kinaendelea kwe vichwa vya wananchi kwasasa. Wananchi wamewazidi wabunge wengi wa CCM kasi katika uraia.
M4C si mchezo ati.
 
Wanaaga kwa staili yao,wanajua hawarudi tena 2015
 
Hi Great Thinkers,

Kwa watu makini tunajua kabisa ni nini kinakuja au kuandaliwa. Uchaguzi wa 2015 unakuja muda si mrefu(just a year ahead). Serikali ya CCM tayari wameshaanza MBINU ZA KUPATA FEDHA at any cost!!!

Lengo na mabadiliko ya Sheria hii ni kulinda WIZI ambao utaiwezesha CCM kupata mabilioni ya KAMPENI ZA UCHAGUZI 2015. Tunajua CCM lazima wawe na pesa ya kuwahonga wapiga kura kwanza na wawe na pesa ya kuwahonga UWT- mashushu ili waweze kuchakachua matokeo!!!

Lazima kizazi hiki kibadilike hizi sio zama za nidhamu ya woga na kinafiki. Let us call spade as spade not big spoon. Mabadiliko lazima yatokee utake usitake upo katika mabadiliko hayo ya sayansi na teknolojia kwa kila kitu. Kama hutaki acha kutumia internet, acha kutumia simu za kiganjani, acha kutumia computer n.k
 
Ripoti ya CAG huwa inaanzia kwanza Ikulu kwa rais ndipo inatinga bungeni!. Hata tume zote za rais ripoti zake huishia kwa rais!.

Watu wanapozungumzia rais kupunguziwa madaraka ndiko huku. Japo sijazisikia hoja zenyewe halisi, ninaamini wabunge makini wangependa ripoti ya CAG itinge bungeni moja kwa moja bila kupitia kwa rais.
P.
 
Watu mnasema rais apunguziwe madaraka ndiyo kwanza mnamrundikia!,kumpelekea rais report ni njia mojawapo ya kuficha makosa,si rahisi report kama ikiwa mbovu itawekwa hadharani,watuambie ni mapungufu gani yaliyojitokeza kwa utaratibu uliopita,hiki ni kitanzi kingine kwa ccm,
 
Back
Top Bottom