Kupitishwa kwa sheria inayotaka taarifa ya CAG zijadiliwe kwanza na kamatiza fedha, baadhi ya wabunge walipinga kwa kusema kufanya hivyo, ni kutungasheria ya kulinyima Bunge madaraka.
Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) alisema haiwezekani Bungelijifunge mdomo wakati upo ubadhirifu unaolalamikiwa na wananchi.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) alisema Bunge linatunga sheria yakujibana. Kwa upande wake Mnyika alitaka mabadiliko hayo yaondolewe, alisemauamuzi wa kuamua kuzipa kamati kujadili taarifa hiyo badala ya wabunge wote, niwa kuzuia CAG asiianike Serikali. Mnyika alipinga kwa kusema kanuni zinaelekezakwamba waraka wowote unaowasilishwa mezani, unakuwa wazi kwa umma.
Alisisitiza kwamba pia taarifa ya CAG inapowekwa mezani iko wazi kujadiliwana si kusubiri kamati. Hata hivyo, Naibu Waziri Mawasiliano, Sayansi naTeknolojia, Januari Makamba alieleza kushangazwa na wabunge kuona Kamati zaBunge kama si sehemu ya mhimili huo.
Makamba alisema sheria imewapa wenyeviti wa kamati hizo za fedha ambazo zoteziko chini ya vyama vya upinzani, kuhakikisha wanajadili yaliyomo katikataarifa hizo za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. Alisema kitendo cha kuzipa kamati husika, kunasaidia kupata taarifa zauhakika kutoka upande mwingine unaopaswa kujadiliwa.
Kulingana na maelezo hayo ya Makamba, mfumo wa awali wa kujadili moja kwamoja, ulikuwa ukisababisha wanaotajwa kufanya ubadhirifu kutokuwa na mwanya wakujieleza ama kutoa ufafanuzi badala yake, walijadiliwa moja kwa moja bungeni.
Mbunge anadiriki kusema Kamati ya Bunge si Bunge. Anaona tabu kutoa heshimakwa Kamati ya Bunge kwa kuwa haiko kwenye televisheni, alisema Makamba