CAG aonya ukubwa wa deni la Taifa kwa GDP tushafika 73% ikifika 76% itakuwa shida, Magufuli asema wataendelea kukopa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
mkopo+pic.jpg

Kwa ufupi
Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16)

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtoa wasiwasi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu Deni la Taifa, akisema nchi inakopa fedha na kuzitumia kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya ukaguzi ya CAG mwaka 2016/17, Rais Magufuli alisema uwekezaji katika miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa umeme wa Stieglers Gorge, utasaidia kukuza uwezo wa Serikali kulipa deni hilo.

Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16) sawa na ongezeko la asilimia 12, kinatia wasiwasi na kwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka, tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) si mbaya lakini ikifika asilimia 76 ya nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control (kudhibiti) ukuaji wa deni hilo,” alisema Profesa Assad.

Katika ufafanuzi wake Rais Magufuli alisema miradi hiyo mikubwa imechagiza baadhi ya wahisani kujenga matumaini ya kuendelea kutoa ushirikiano na wameanza kurejea baada ya kuona Serikali ikiitekeleza kwa kutumia fedha za ndani.

Alisema Serikali inazo fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa na umeme.

Akitoa maoni yake kuhusu deni hilo, Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema wasiwasi wa deni hilo unaweza kuchagizwa na aina ya mkopo, akisema ipo ya riba nafuu ya marejesho ya muda mrefu.

“Tunaita non- concessional, lakini kuna mikopo ya riba kubwa,” alisema.

Alitaja mambo matatu ya kuzingatia katika kudhibiti ukuaji huo wa deni kuwa ni pamoja na kuangalia upya mikataba ya misamaha ya kodi kwa kampuni za kigeni nchini.

Alisema tafiti kadhaa zinaonyesha misamaha hiyo inatengeneza mazingira ya Taifa kuibiwa kodi.

“Pili, Serikali inatakiwa kuongeza kasi ya udhibiti ukwepaji kodi na kasi ya ukusanyaji kodi, lakini (tatu) Serikali inatakiwa kutekeleza miradi haraka inayotokana na mikopo ili kuepuka mazingira ya ufisadi.”

Chanzo: Mwananchi
 
Kwenye ukubwa wa deni la taifa ulipofika kunahitajika mjadala wa kitaifa, maana huyu rais aliyepo hana uelewa wowote kuhusu masuala ya uchumi na ukizingatia kuwa yeye ndiye mshauri mkuu wa wachumi kuhusu mambo ya uchumi

Hili suala la vigogo watano wa Chadema kulala lupango huenda ni ajenda ya kuhamisha mjadala wa report ya CAG kwenda kwenye suala la kunyimwa dhamana viongozi wa Chadema

Taifa hili linaenda kimatukio tukio tu, mambo ya msingi na afya kwa taifa yanafukiwa fukiwa kijinga kijinga tu ili tujadili umafia wa serikali
 
mkopo+pic.jpg

Kwa ufupi
Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16)

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtoa wasiwasi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu Deni la Taifa, akisema nchi inakopa fedha na kuzitumia kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya ukaguzi ya CAG mwaka 2016/17, Rais Magufuli alisema uwekezaji katika miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa umeme wa Stieglers Gorge, utasaidia kukuza uwezo wa Serikali kulipa deni hilo.

Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16) sawa na ongezeko la asilimia 12, kinatia wasiwasi na kwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka, tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) si mbaya lakini ikifika asilimia 76 ya nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control (kudhibiti) ukuaji wa deni hilo,” alisema Profesa Assad.

Katika ufafanuzi wake Rais Magufuli alisema miradi hiyo mikubwa imechagiza baadhi ya wahisani kujenga matumaini ya kuendelea kutoa ushirikiano na wameanza kurejea baada ya kuona Serikali ikiitekeleza kwa kutumia fedha za ndani.

Alisema Serikali inazo fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa na umeme.

Akitoa maoni yake kuhusu deni hilo, Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema wasiwasi wa deni hilo unaweza kuchagizwa na aina ya mkopo, akisema ipo ya riba nafuu ya marejesho ya muda mrefu.

“Tunaita non- concessional, lakini kuna mikopo ya riba kubwa,” alisema.

Alitaja mambo matatu ya kuzingatia katika kudhibiti ukuaji huo wa deni kuwa ni pamoja na kuangalia upya mikataba ya misamaha ya kodi kwa kampuni za kigeni nchini.

Alisema tafiti kadhaa zinaonyesha misamaha hiyo inatengeneza mazingira ya Taifa kuibiwa kodi.

“Pili, Serikali inatakiwa kuongeza kasi ya udhibiti ukwepaji kodi na kasi ya ukusanyaji kodi, lakini (tatu) Serikali inatakiwa kutekeleza miradi haraka inayotokana na mikopo ili kuepuka mazingira ya ufisadi.”
Kuna nchi wana 278% na bado wanakopeshwa kinachoangaliwa ni uimara wa uchumi na rasilimali zilizopo!
 
GDP YETU KWA SASA NI 52BN USD AU TR 117 TSH KAMA DENI NI 41TN NI SAWA NA ASILIMIA 35 TU KWA HILO KAMA UKOMO NI 72% TUNAWEZA KUKOPA BASO 37% YA GDP NA KWA KUWA UCHUMI UNAKUA HII RATIO ITAZIDIKUPUNGUA, RAIS ANA POINT MAANA HELA TUNAYOKUPA INACHOCHOA ZAIDI UKUWAJI WA UCHUMI KWA VILI INAELEKEZWA KWENYE UBOROSHAJI WA MIUNDOMBINU
 
Hahaha...hadi raha,Kuna mtu anachishwa kazi siku si nyingi za Usoni.CAG ametoa wapi ripoti kama hiyo?Haoni Viwanda?Haoni SGR na soon tunaanza kuitumia.Haoni kuwa Tunatumia Hela yetu na hatukopi popote.Miradi yote Mikubwa ni Pesa Zetu na si za msaada.Sasa Deni limekuaje?CAG ajiangalie na Ripoti zake,hatuazimi cha mtu sisi.Wasiturudishe Nyuma Bwana Idadi ya Viwanda inaongezeka.Na Uchumi unakuaa kwa kasi kwa sasa.Samahani kama nimeandika vibaya
 
Wala hamna cha kustaajabisha hapo. Kama anaweza kujilinganisha na malaika sembuse CAG ambaye ni binadamu tu!!! Teh teh teh!!!
 
Hilo ni gazeti gani? Upuuzi na upotoshaji, deni la taifa kwa sasa ni chini ya 35% ya GDP. Ni mawili, either tuna waandishi vilaza au gazeti ni ka sehemu ka kupeperusha kiwanda cha uongo.
 
Mbona sielewi elewi!! Watuambie vizuri upandaji wa hili deni!

SI walishatuambia miradi mikubwa nchini kama vile ujenzi wa reli; tunatumia mapato yetu wenyewe?!
 
GDP YETU KWA SASA NI 52BN USD AU TR 117 TSH KAMA DENI NI 41TN NI SAWA NA ASILIMIA 35 TU KWA HILO KAMA UKOMO NI 72% TUNAWEZA KUKOPA BASO 37% YA GDP NA KWA KUWA UCHUMI UNAKUA HII RATIO ITAZIDIKUPUNGUA, RAIS ANA POINT MAANA HELA TUNAYOKUPA INACHOCHOA ZAIDI UKUWAJI WA UCHUMI KWA VILI INAELEKEZWA KWENYE UBOROSHAJI WA MIUNDOMBINU

na wewe unamaini hizo figa?
na huko kukua wewe unakuona?
 
Mbona sielewi elewi!! Watuambie vizuri upandaji wa hili deni!

SI walishatuambia miradi mikubwa nchini kama vile ujenzi wa reli; tunatumia mapato yetu wenyewe?!

sasa hapo huelewi kitu gani?? kutumia pesa zetu za ndani ndo hivo.. unakopa alaf unalipa mwenyewe kwa fedha za ndani.

kwani wewe ukikopa bank ukafanya mradi wako baadae ukarejesha kwa mshahara wako, utasema mradi umejenga kwa fedha zako au za bank???
 
Iko siku mtakuja kutuelewa nyie lumumba.....time will tell

Ova
 
GDP YETU KWA SASA NI 52BN USD AU TR 117 TSH KAMA DENI NI 41TN NI SAWA NA ASILIMIA 35 TU KWA HILO KAMA UKOMO NI 72% TUNAWEZA KUKOPA BASO 37% YA GDP NA KWA KUWA UCHUMI UNAKUA HII RATIO ITAZIDIKUPUNGUA, RAIS ANA POINT MAANA HELA TUNAYOKUPA INACHOCHOA ZAIDI UKUWAJI WA UCHUMI KWA VILI INAELEKEZWA KWENYE UBOROSHAJI WA MIUNDOMBINU
Duuh kweli watu tunatofautiana, yaani ndugu pamoja na maelezo ya CAG bado unapotosha umma mchana kweupe!
Amesema deni la taifa limefikia 46 trilioni, sawa na 72%, na tukifikia 76% ni hatua ya hatari, hayo unajifanya huyaoni kbisa, unazungumza habari ya Trilioni 41!!
Hiyo ni zaidi ya mahaba mzee
 
Back
Top Bottom