CAG aonya ukubwa wa deni la Taifa kwa GDP tushafika 73% ikifika 76% itakuwa shida, Magufuli asema wataendelea kukopa

mkopo+pic.jpg



Kwa ufupi
Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16)


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtoa wasiwasi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu Deni la Taifa, akisema nchi inakopa fedha na kuzitumia kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya ukaguzi ya CAG mwaka 2016/17, Rais Magufuli alisema uwekezaji katika miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa umeme wa Stieglers Gorge, utasaidia kukuza uwezo wa Serikali kulipa deni hilo.

Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16) sawa na ongezeko la asilimia 12, kinatia wasiwasi na kwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka, tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) si mbaya lakini ikifika asilimia 76 ya nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control (kudhibiti) ukuaji wa deni hilo,” alisema Profesa Assad.

Katika ufafanuzi wake Rais Magufuli alisema miradi hiyo mikubwa imechagiza baadhi ya wahisani kujenga matumaini ya kuendelea kutoa ushirikiano na wameanza kurejea baada ya kuona Serikali ikiitekeleza kwa kutumia fedha za ndani.

Alisema Serikali inazo fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa na umeme.

Akitoa maoni yake kuhusu deni hilo, Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema wasiwasi wa deni hilo unaweza kuchagizwa na aina ya mkopo, akisema ipo ya riba nafuu ya marejesho ya muda mrefu.

“Tunaita non- concessional, lakini kuna mikopo ya riba kubwa,” alisema.

Alitaja mambo matatu ya kuzingatia katika kudhibiti ukuaji huo wa deni kuwa ni pamoja na kuangalia upya mikataba ya misamaha ya kodi kwa kampuni za kigeni nchini.

Alisema tafiti kadhaa zinaonyesha misamaha hiyo inatengeneza mazingira ya Taifa kuibiwa kodi.

“Pili, Serikali inatakiwa kuongeza kasi ya udhibiti ukwepaji kodi na kasi ya ukusanyaji kodi, lakini (tatu) Serikali inatakiwa kutekeleza miradi haraka inayotokana na mikopo ili kuepuka mazingira ya ufisadi.”


Chanzo: Mwananchi
CAG.....76% is not just a reason....the reason here is China, hii ndiyo nchi hatari sana duniani kwasababu ya njia ya Urubuni wao juu ya uchumi wa nchi maskini na zenye tawala mbaya barani Africa. Hawa wana-override sheria na taratibu zozote ili mradi waweze kuingia kwenye rasilimali yoyote ilie iwayo hata chumba kimoja anachoweza kuishi Mchina mmoja.
 
Ni vyema tukasikiliza na kufuata ushauri wataalamu wetu uchumi na sector nyingine.Tuna wataalam wenye upeo kwa uchache, mkuu TIC,Katibu mkuu viwanda; CAG na wengine.Mkuu awape nafasi kushauri na kusimamia.
 
CAG nimemuelewa, kwasababu by defacto ni "mchumi". JPM pia nimemuelewa, kwasababu si "mchumi" kama mwenyewe anavyosema. Ila huyu profesa wa UD ndio sijamuelewa kabisa. Sidhani kama kwa sasa nchi hii tuna tatizo la kukwepa kodi. Nadhani kwa sasa tuna tatizo la kutotengeneza vyanzo vingi vya kutoza kodi.

Kimsingi kodi haipaswi kutozwa katika any economic activity bali kodi yapaswa kutozwa kwenye "profitable" economic activities. Profesa anaposema miradi itekelezwe haraka kuepuka ufisadi sijui anamasnisha nini hapa. Jambo la msingi katika mikopo ni "sensible" predictable returns kule hizo pesa zinakoelekezwa. Reli, Stiglers Gorge ni miradi mizuri lakini lazima tukubali yote ni derived demand nature. Return kutoka katika miradi hiyo inategemea na other government policies, siyo yenyewe kama ilivyo.

Fine, tunataka tuwe na umeme mwingi ili utumike kwenye viwanda vyetu. Tunataka SG ili tusafirishe bidhaa zetu za kilimo na viwanda. Lakini cause-impact siyo "having enough electricity implies many industries". Kuna factor nyingine nyingi zinazotakiwa kuchochea uanzishwaji wa viwanda.

Government should avoid single direction policy! Inclusive government policy is needed ili kufikia kile tunachokipata. Inclusive government policy lazima ijumuishe hard policy and soft policy.
Thank you. This is a wonderful piece of observation and advice. Kitu cha kujiuliza je hizo pesa tunazokopa zinaenda kwenye miradi ipi? Serikali inatuchanganya maana kila siku miradi ya SGR na Stieglers Gorge tunaambiwa inajengwa kwa fedha zetu za ndani; wakati huo huo utetezi wa kukopa ni kutekeleza miradi hii hii mikubwa. Na deni linaendelea kupanda! Je tunakopa kwa ajili ya miradi ipi?

Kama ulivyosema kutekeleza miradi hii kikamilifu siyo 'automatically' inatupa uwezo wa kulipa deni husika. Tulijenga reli ya TAZARA; sina hakika kama wachina wangetukopesha tungeweza kulilipa deni hilo. SGR isitufanye tukafikiria itatuwezesha mara moja ikiisha tu kuanza kutupa uwezo wa kulipa. Tunaweza tukashindwa hata kuiendesha. Stieglers Gorge halikadhalika. Tunatakiwa tuwe waangalifu katika kukopa...'tusije lazimishwa kulipa kwa kipande cha mnofu wetu'.
 
Huyu dereva wetu haambiliki kabisaa, hajui kama hapa pana kona, hajui kama hapa mlima, hajui hapa kama pana tuta yy ni speed tu, hata haoni kama hapa ni mteremko akanyage breki nadhani mwisho wa safari yetu wengi tutafika tukiwa vilema
Nchi yetu tajiri bwana kwani nini
 
Hiyo Mikopo inaenda wapi na kodi zetu zinafanya kazi gani mbona hakuna miradi mipya.
 
Ripoti ya CAG Mkuu kama haizungumzii ubadhirifu mkubwa wa kuchota trillions hazina bila idhini ya Bunge unaofanywa na huyu DU kupitia mtoto wa dada yake Dotto James basi hiyo ni ripoti UCHWARA.

Bunge liliidhinisha 2 billions kwa Chato Airport zilizochotwa hadi sasa ni 350 billion. Ununuzi wa ndege zimechotwa $485 millions na uchotwaji mwingine mbali mbali ikiwemo rushwa kwa Wabunge wa MACCM na ununuzi wa wachumia tumbo Wabunge na Madiwani.

Jana nilienda kwenye tovuti ya CAG ili niisome ripoti hiyo kwa mshangao wangu ilikuwa haijawekwa. Nitaitafuta tena baadaye leo.

Ina maana CAG hajaona viwanda kila mahali,hajaona watu walivyouawa Kibiti.

Haaaa haaaa nawaza kama Pascal Mayalla

c.c BAK
 
Mbona sielewi elewi!! Watuambie vizuri upandaji wa hili deni!

SI walishatuambia miradi mikubwa nchini kama vile ujenzi wa reli; tunatumia mapato yetu wenyewe?!
Rais Magufuli kapewa adhabu ya kuwa na ndimi mbili.
Tuendelee kumlilia Mungu ampe mapigo zaidi
 
Rais Magufuli kapewa adhabu ya kuwa na ndimi mbili.
Tuendelee kumlilia Mungu ampe mapigo zaidi
Kwa muda mrefu niliamini Mzee wa Msoga ni bonge la msanii lakini mbele ya Jecha Palamagamba Muhongo; Mzee wa Msoga tupa kule!

Jecha Palamagamba Muhongo sio tu msanii bali ni Muhongo mwenye PhD ya taaluma husika!
 
Hati zilizosemwa kama ni chafu ni saba, tatu zikiwa za Halmashauri ambako baba akachukua maamuzi vipi kuhusu hao wengine wenyewe sio wakuchukuliwa hatua nchi hii
 
Back
Top Bottom