Cabinet reshuffle: This is a disgustingly bad joke, Mr President

Cabinet reshuffle: This is a disgustingly bad joke, Mr President

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2007
Posts
1,116
Reaction score
4,773
575686_171810116354558_542460542_n.jpg

UCHAMBUZI WA HARAKA:

Yaelekea matatizo ya uchumi wetu si miongoni mwa mambo yanayomnyima usingizi Rais Jakaya Kikwete, ndio maana amefanya kituko cha mwaka kumteua Mwigulu Nchemba kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti. Ila mzaha huo ni wa kimkakati zaidi. CCM inahitaji fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2015. Hadi hapo si tatizo, lakini tatizo lipo kwenye kupata fedha hizo kwa njia halali. Ninatafsiri uteuzi wa Mwigulu kwenda Wizara ya fedha kuwa ni sehemu ya mkakati wa kuiwezesha CCM kupata fedha za uchaguzi mkuu ujao. Tutegemea EPA nyingine? Time will tell.

Adam Malima kupelekwa Wizara nyeti ya fedha si jambo la kushangaza, ikizingatiwa yyeye na JK wanatoka mkoa wa Pwani na ukaribu wao. Sijui nini kilichopeleka Juma Nkamia kupewa uwaziri wa Michezo, lakini majibu anayo JK mwenyewe.

BOTTOM LINE: Tatizo sio mawaziri bali Kikwete mwenyewe. Mbunge wa Ubungo aliwahi kuingia matatani alitamka bayana kuwa JK NI DHAIFU lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, na alichosema Mnyika ndo ukweli wenyewe. Mawaziri wanaweza kubadilishwa kila wiki, lakini as long as kiongozi wao ni dhaifu, basi tuendelee kutarajia yaleyale yanayopelekea kabineti kubadilishwa mfululizo kama safari za JK nje ya nchi.

Na kwa waliodhani Pinda angeng'oka walikuwa wanaota ndoto za mchana. Pinda ni nyenzo muhimu kwa JK, ni mtu anayebeba lawama za bosi wake. Madudu yakifanywa na JK,lawama zinaelekezwa kwa Pinda.

Tuombe Mungu 2015 ifike mapema, JK amalize majaribio yake ya urais, labda nchi yetu itapata mwelekeo mpya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kwa mawazo yangu uteuzi wa naibu waziri wa Fedha Nchemba hauna msingi. Kwa mawazo yangu sijawahi kusikia huyu waziri akiongea sera yeyote ya maana ya Fedha, wanasema mchumi lakini hajawahi kuongea strategy yeyote hapa ya maana, hajui vizuri uchumi wa dunia unavyoenda na ni mwanasiasa zaidi kuliko kiongozi na hata weza kufanya maamuzi bila kuangalia manufaa ya CCM pekee na jinsi ya kudidimiza wapinzani. Kiongozi ambaye anaweka upelelezi wa kutafuta mahawara wa viongozi wa upinzani si kiongozi wa kutegema kuleta maendeleo. Mimi ningeshauri kwenye sehemu za Fedha, Nishati na Madini tutafute wataalamu wenye uzoefu kwenye hizo sehemu na wamefanya kazi na kujua dunia inavyoenda. Vilevile kwa safu ninayoiona hapa ni bora tungetafuta diaspora mwenye uzoefu kwenye mambo ya fedha na amawahi kuwa kiongozi na kutuongoza.
 
Kaka acha tu,nna hasira kufanya uwaziri majaribio..Nkamia ataban magazeti mengi,Mwigulu umeshataja atakayofanya but uteuzi wake ni COMEDY tosha,Malima anapozwa ktk nafasi iliyomletea baba yake shida,Mbona mizigo imebaki? Lazaro Nyalandu yeye anakwenda kumalizia kuhujumu utalii..long live KAGASHEKI.
 
Kwa mawazo yangu uteuzi wa naibu waziri wa Fedha Nchemba hauna msingi. Kwa mawazo yangu sijawahi kusikia huyu waziri akiongea sera yeyote ya maana ya Fedha, wanasema mchumi lakini hajawahi kuongea strategy yeyote hapa ya maana, hajui vizuri uchumi wa dunia unavyoenda na ni mwanasiasa zaidi kuliko kiongozi na hata weza kufanya maamuzi bila kuangalia manufaa ya CCM pekee na jinsi ya kudidimiza wapinzani. Kiongozi ambaye anaweka upelelezi wa kutafuta mahawara wa viongozi wa upinzani si kiongozi wa kutegema kuleta maendeleo. Mimi ningeshauri kwenye sehemu za Fedha, Nishati na Madini tutafute wataalamu wenye uzoefu kwenye hizo sehemu na wamefanya kazi na kujua dunia inavyoenda. Vilevile kwa safu ninayoiona hapa ni bora tungetafuta diaspora mwenye uzoefu kwenye mambo ya fedha na amawahi kuwa kiongozi na kutuongoza.

8383251_orig.jpg
Busara imetumika hapa, ni sawa na ile maana ya promotion by demotion ndicho pengine kinachompata Mwigulu. Kuna wazuri ambao wangefaa nafasi hiyo, lakini Rais kaona amchomeke hapa awe busy na mambo ya serikali kuliko alivyobaki huru kufanya madudu anayojua mwenyewe na pengine kusababisha kuyumbisha amani ya nchi ambayo ni zao letu tangu tupate uhuru kusumbuliwa na mtu huyu.
 
Hivi kama kwenye ni mchumi na ana uzoefu Mwigulu ajibu swali hili.

1. Je ni kwanini mikopo ya bank za Tanzania ni 18%-30% wakati nchi nyingine mikopo ni 4%-10%
2. Tax za juu za magari bandarini zina faida au hasara kwa nchi? na kwanini nipe statistics
 
hivi ulitaka kusema nini hasa? hapa naona majungu tu na wivu. Nini hasa point yako ya kuleta uzi huu?
 
Wakuu,

Hivi hakuna marais WAKUKODISHA?pengine tunaweza tukamkodi OBAMA,au CLINTON wakatusogeza kimaendeleo,maana hawa wenzetu naona kama hawana VISION hivi!wanaongoza nchi kwa mazoea tu!

Naona kama wanajali maslahi Yao zaidi ya maslahi ya nchi!
 
Kwa mawazo yangu uteuzi wa naibu waziri wa Fedha Nchemba hauna msingi. Kwa mawazo yangu sijawahi kusikia huyu waziri akiongea sera yeyote ya maana ya Fedha, wanasema mchumi lakini hajawahi kuongea strategy yeyote hapa ya maana, hajui vizuri uchumi wa dunia unavyoenda na ni mwanasiasa zaidi kuliko kiongozi na hata weza kufanya maamuzi bila kuangalia manufaa ya CCM pekee na jinsi ya kudidimiza wapinzani. Kiongozi ambaye anaweka upelelezi wa kutafuta mahawara wa viongozi wa upinzani si kiongozi wa kutegema kuleta maendeleo. Mimi ningeshauri kwenye sehemu za Fedha, Nishati na Madini tutafute wataalamu wenye uzoefu kwenye hizo sehemu na wamefanya kazi na kujua dunia inavyoenda. Vilevile kwa safu ninayoiona hapa ni bora tungetafuta diaspora mwenye uzoefu kwenye mambo ya fedha na amawahi kuwa kiongozi na kutuongoza.

Ndugu yangu Kamundu, kwa yeyote aliye na macho ya uchunguzi kwa Baraza hili atagundua hila iliyojificha ndani yake; nayo ni kuwasogeza watu watakaofanikisha EPA nyingine mahsusi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.
Kwa kifupi Baraza hili limekaa kishkajishkaji zaidi kuliko kiutendaji. Yaelekea JK ameteua Baraza hili kwa ushauri na maslahi ya chama chake na si nchi.
Mimi sikuwa mmoja wa waliokuwa wakiamini JK ni dhaifu, lakini kwa Baraza hili sina la kusema, watanzania tuandike maumivu na tutarajie EPA nyingine, tena mbaya kuliko ya 2005.
 
Kwlei huu ni mzaha wa wazi..CCM wanamalizia maisha..na hivyo wanajitahidi kupeana nafasi ili angalua wengine wasife bila kuonja marupurupu ya kazi kubwa wlaiyoifanyia CCM mwishoni.
 
Kamundu,

..wako wa-Tz wengi tu ambao ni competent wangeweza kuteuliwa kutumikia wizara ya fedha.

..nadhani JK mwenyewe haamini kama wizara ya fedha ni muhimu kiasi hicho kulazimisha kuteua watu wenye solid track record kutumikia pale.

NB:

..halafu kitendo cha waandishi wa habari kucheka na kuguna kuhusu baadhi ya teuzi za Raisi, kinaleta taswira isiyo nzuri kwa mteuliwa, washauri wa Raisi, pamoja na Raisi mwenyewe.

cc Mchambuzi, Mdondoaji, NasDaz
 
Back
Top Bottom