Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,609
- 1,739
Naona kuna mwana Sesere yule ambae watoto huwa wanapewa kucheza nae na kumfanya kila ,kama watamnyofoa miguu ,watamvika nguo nzuri ,watamuimbia nyimbo alimradi wanacheza nae na mwana Sesere hata hajui wala hashughuliki mradi yupo tu.
Na raisi wetu Mh.Jakaya Kikwete naona kwa vile ni jitu zima baba la miraba minne lakini watu wamemgeuza na kumfanya Bwana Sesere , wanaomwibia , wanaomdanganya na wanomfanyia kila vituko na visa yeye hata hana habari wala hashughuliki yupo tu na miunzi yake na mkono mmoja mfukoni.
Yaani kama anaandaa mikakati basi naona ataifanya utakapokaribia uchaguzi ili kuongeza upendo kwa wale wanaomuibia na kumfanyia matendo ya kumdanganya.
Bwana Sesere atavuka 2010 na Chama chake na kuendelea na miunzi na mkono mmoja mfukoni sijui anakamata hirizi .Maana mafisadi na wale wanaomdanganya watafanya kila hila ili ashinde tena kwani kuwepo kwa Bwana Sesere ni faraja kwao kufanya watakalo.