Bwana Sesere

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Naona kuna mwana Sesere yule ambae watoto huwa wanapewa kucheza nae na kumfanya kila ,kama watamnyofoa miguu ,watamvika nguo nzuri ,watamuimbia nyimbo alimradi wanacheza nae na mwana Sesere hata hajui wala hashughuliki mradi yupo tu.
Na raisi wetu Mh.Jakaya Kikwete naona kwa vile ni jitu zima baba la miraba minne lakini watu wamemgeuza na kumfanya Bwana Sesere , wanaomwibia , wanaomdanganya na wanomfanyia kila vituko na visa yeye hata hana habari wala hashughuliki yupo tu na miunzi yake na mkono mmoja mfukoni.
Yaani kama anaandaa mikakati basi naona ataifanya utakapokaribia uchaguzi ili kuongeza upendo kwa wale wanaomuibia na kumfanyia matendo ya kumdanganya.
Bwana Sesere atavuka 2010 na Chama chake na kuendelea na miunzi na mkono mmoja mfukoni sijui anakamata hirizi .Maana mafisadi na wale wanaomdanganya watafanya kila hila ili ashinde tena kwani kuwepo kwa Bwana Sesere ni faraja kwao kufanya watakalo.
 
Nimekuelewa mkuu, yaani ni kweli JK amekuwa kama mdoli/mwanasesere kwa kuwa sasa kila afanyiwalo anatulia utadhani huwa anatumia betri na zimeisha.

Kuna walioanza kumkumbuka Mkapa na kusema ingawa alifanya mengi underground lakini alikuwa akisimama anakoroma na vijibwa vidogo vidogo vinatulia, sasa huyu jamaa yaani nakwambia kaifanya hii nchi kama mpira. Kila mtu anapiga kwenda anakotaka na kiasi anachotaka yeye. Tena akiona watu wengine asiowataka wanataka kupiga mpira basi yeye anauchukua anashika kwa mikono. Sasa hata kama ni mechi ndio style gani hiyo?
 
Huyu alisema serikali yake haina ubia ,hivi alikusudia kitu gani jamani ,huyu alisema maisha bora kwa kila Mtanzania , huyu alisema mafisadi wajitayarishe ,alikuwa na maana gani ,naona bado anao wakati wa kijurekebisha ,la si hivyo wenziwe watampiga kikumbo ,sasa akishapigwa kikumbo naona atapata tabu kuliko wengine ,huwezi kujua maraisi wa siku hizi waote wamejanjaruka unaweza ukamuona jamaa katulia tuli kumbe tayari ameshakuwa na vitega uchumi kibao ,naona safari haziishi hata amekuwa na sahau kuwa wapiga debe wake tunahitaji hotuba ya kila mwezi ameanza kutusahau hata utamu wa pili hatujampigia debe.
Hawa mafisadi nadhani ameshawapa green light wasiwe na wasiwasi kila mmoja aendelee kuchukua chake mapema.Ila wapiga debe tunajipanga kumpatia awamu yake ya mwisho.
 
Naaam naam naaaam
ikawa ahsubuhi ikawa jioni siku ya kwanza..... nasubiri siku ya kura nishuhudie tena unafiki wa watanzania wanaolalamika ubovu na ufisadi wa serikali ya ccm huku wakiiunga mkono asilimia 10000
 
Na raisi wetu Mh.Jakaya Kikwete naona kwa vile ni jitu zima baba la miraba minne lakini watu wamemgeuza na kumfanya Bwana Sesere , wanaomwibia , wanaomdanganya na wanomfanyia kila vituko na visa yeye hata hana habari wala hashughuliki yupo tu na miunzi yake na mkono mmoja mfukoni.
JK Ni bwana sesere siku nyingi kajifanya hivyo mwenyewe kawakumbatia mafisadi wenzake.....awaongoze hao hao wanasesere wenzake simtambui kama raisi bora.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom