Bwana mdogo ashinda kesi mahakamani!!

Upanga

Senior Member
Jun 18, 2007
145
50
Bwana Mdogo ameshinda kesi Mahakamani ya kutaka kukaa na mtoto wake wa miaka tisa baada ya mzozo na mama mtoto wa karibu miaka kadhaa!!
Bwana Mdogo alipeleka malalamiko yake serikali za mitaa kudai kukaa na mtoto baada ya kuona mama mtoto hamjali wala hampi matunzo mazuri mtoto,lakini huyu dada alikataa katakata kukubaliana na Serikali ya mtaa na hivyo baba mtoto kuruhiswa kwenda ustawi ili wakawekewe mambo sawa!
Hata hivyo kule ustawi mama mtoto akashindwa tena lakini akagoma kumruhusu mtoto aende kwa baba.Ustawi wakampa ruhusa baba aende mahakami.
Jana kesi imeisha baada ya kusikilizwa almost miezi minne,na mahakama imeamuru baba apewe mtoto,lakini mama amekataa kutoa mtoto kwa kigezo cha kusema anakataa rufaaa!
Je rufaa ambayo mtu anafikiria kukata inaweza zuia adhabu isitekelezwe?
Tunaomba michango yenu kwa hili.
 
Lazima aombe court injunction - hukumu isitekelezwe. hawezi kukataa kutekeleza hukumu eti anatazamia kuomba rufani. Utaratibu uko hivyo>
 
nashukuru kwa maelezo mazuri!kwahiyo asipofanya hivyo hana haki ya kukatalia hukumu kwa utemi tuuu wa mtaani!
Thanks
 
Chukua mtoto wenu hakuna mtu anayeweza kugoma kutekeleza hukumu ya mahakama, labda kama ameweka court injunction kwa kutumia mahakama iliyo juu ya hiyo iliyotoa adhabu.
 
nashukuru kwa maelezo mazuri!kwahiyo asipofanya hivyo hana haki ya kukatalia hukumu kwa utemi tuuu wa mtaani!
Thanks

Kama hajaomba court injunction nenda ukaze hukumu. Usimchukue mtoto kwa kutumia nguvu/mabavu , that will turn against you then. Unakaza hukumu!!! Ukiomba mahakama hukumu itekelezwe
 
Back
Top Bottom