Bwana harusi amuua baba yake kwa risasi

Bwana harusi amuua baba yake kwa risasi

Mtu mmoja wa miaka 47 aliyejulikana kwa jina la Shirima mkazi wa Kibaha, amemuua baba yake mzazi anayekadiriwa kuwa na miaka 70 kwa kumpigarisasi iliyotoka kwenye SMG yake.

Inasemekana baba huyo alikua amelala nyumbani kwa mwanae na alitokea Moshi kwa mualiko wa harusi ya bwana Shirima ambayo ilikwisha fanyikana hapo bwana Shirima na mkewe walikua honeymoon hapo nyumbani kwao.

usiku wa jana baba yake alipatwa na haja ndogo akaenda chooni wakati anarudi akakosea mlango wa chumba chake na kuingia chumbani kwa mwanae ndipo mke wa Shirima aliposikia mlango unafunguliwa na mtu yupo ndani - akapiga kelele za mwizi hapo ndo mumewe akachukua short gun yake na kumlenga babake na kumuua akidhani ni mwizi.

Inasemekana makazi ya bwana Shirima mtaani kwao nyumba zipo mbalimbali ndo mana akachukua uamuzi wa kumimina risasa bila kuuliza hata swali moja kwa mvamizi huyo wa chumbani kwake.

Imenisikitisha sana habari hii, yamkini tuwe waangalifu kabla ya kuchukua uamuziwowote.

SOURCE WAPO RADIO ASUBUHI HII

Hapo kwenye RED, hivi SMG na shortgun ni kitu kile kile? Kwa sheria za kumiliki silaha za Tanzania, zinaruhusu kweli mtu binafsi kumiliki SMG?

Naomba ufafanuzi hapa!!!!.

Tiba
 
Pombe si chai. Hakawii kuwa alilala nazo.
Salamu kwa wanaolewa hadi wanapotea milango lmao
 
Ila na bwana harusi nae analala na smg chini ya mto au? Manake kusikia kelele tu za mkewe akashoot? Ina maana na baba hakutoa sauti yoyote wakamtambua? Nna maswali milioni!
 
..Baada ya harusi msiba...furaha Vs huzuni...hakika wote tutaonja mauti katika hali tofauti tofauti (kwa ugonjwa, kwa panga, kwa ajali, kwa sumu, kwa......)

bwana ametoa bwana ametwaa

rip mpigwa risasi
 
mfanyabiashara maarufu mkazi wa mlandizi, mkoa wa pwani ndugu BON KAVISHE,amemuua babake mdogo kwa risasi majira ya saa 10 usiku nyumbani kwake mlandizi. tukio hilo limetokea siku ya jumamosi kuamkia jumapili ya tarehe 12.05.2013 baada ya kukamilika sherehe ya harusi ya mdogo wake.taarifa zinadai kuwa baada ya sherehe hiyo ndugu jamaa na marafik wakaenda kujipumzisha.ndipo ndugu KAVISHE ambaye ni mmiliki wa bar maarufu hapa mlandizi ya zimbabwe bar alipoenda kujipumzisha nyumbani yeye na babake mdogo, lakin wakati wa usiku babake mdogo akataka aende choon ndipo katka harakati akajikuta ameingia chumbani kwa mwanae na ndipo mke wa kavishe akapiga kelele akidhani ni mwizi na ndugu kavishe kumpiga risasi na kufariki papo hapo.mpaka sasa ndugu kavishe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.

Apokonywe hiyo silaha huyo punguwani...huwezi kukurupuka na kuanza kupiga risasi ovyo ovyo tu

Kuna haja ya Polisi wenyewe kuwapima akili hawa wamiliki wa silaha na sio kwenda kuleta cheti cha Daktari

Neno bahati mbaya kwenye matumizi ya silaha za moto ni UPUMBAVU
 
Hapo kwenye RED, hivi SMG na shortgun ni kitu kile kile? Kwa sheria za kumiliki silaha za Tanzania, zinaruhusu kweli mtu binafsi kumiliki SMG?

Naomba ufafanuzi hapa!!!!.

Tiba

Muite Dingswayo anajua vizuri. mi nadhani SMG stands for saab machine gun, bunduki inayoweza kutema mfululizo.
Ni kama corolla ni toyota lakini toyota sio lazima iwe corolla
 
Last edited by a moderator:
shirima na kavishe ni koo mbili tofauti wote wamefanya matukio tofauti au ni tukio hilo hilo kwani kuna threads 2 tofauti lakini maudhui ni haya haya.

wafiwa poleni sana.
 
Muite Dingswayo anajua vizuri. mi nadhani SMG stands for saab machine gun, bunduki inayoweza kutema mfululizo.
Ni kama corolla ni toyota lakini toyota sio lazima iwe corolla
Ni sawa kabisa. SMG ni submachine gun, na shotgun ni bunduki ambayo risasi ndani yake mna gololi.
 
Ina maana hao maharusi wapya hawakufunga mlango wa chumba chao?
 
gamebore_kent_cartridge.jpg
Hii ndiyo risasi ya shotgun ambayo ndani mwake kuna hizi shots nyingi ambazo baada ya kulipuka ndio zinazotoka kwenye mtutu.
 
hapana bwana wewe utamiminaje shaba ovyo bila kuangalia kitu unachokipiga au ndo usingizi

si unajua tena: my sweetie, my asali, my hanee zikizidi zinazidisha sukari mwilini mpaka unasahau kufunga mlango, hupunguza pia uwezo wa kuona kwa macho. si unaona hata mleta mada alianza na SMG akamalizia na shortgun, nahisi ilikuwa bastola.......
 
Back
Top Bottom