Bw. Mohammed Said yuko wapi?

Kuna watu wajinga kama Mohamed Said, hawajui misingi iliyojengwa hadi Tanzania ikaitwa kisiwa cha amani...wanadhani amani hiyo ilishushwa tu kama manna kutoka mbinguni. Sasa wasubiri kuvuna walichokuwa wakikitafuta...kuna "red line" haikutakiwa kuvukwa! Wafuasi wake vipofu kama zomba, Ritz na wengineo kama kweli maji mmeyavulia nguo, sasa mkae tayari kuyaoga. Nina hakika wako Waislaam wengi tu wanaungana na wazalendo wa kweli wa taifa hili wasiokubaliana na haya matendo yenu ya kihuni kwa kutumia kivuli cha dini...enough is enough!

Unaweza kutueleza maana ya Dar Es Salaam?

Ukiijuwa hiyo, utajuwa kuwa Tanzania hii, ambayo ilikuwa ikiitwa Tanganyika, haijawahi kutokuwa na amani toka mwaka 1918 wakati Waislaam walipopigana Jihad vita vya Majimaji kupinga ujio wa Wajerumani. Jee, unayapinga hayo?
 
Historia ni kitu kimoja na uchochezi kwa kutumia historia ni jambo jingine.

Tunamwalika Mohamed Said ili aje atufafanulie yale waliyoongea na profesa kuwa '' Tanzania is another Rwanda in the making'' je ndio wakati wake umefika?

Tunamsihi aje hapa afafanue kuhusu uchochezi wa kidini ambao tulimuuliza hakuweza kujibu. Je, haya ndiyo aliyokuwa anataraji au alimaanisha kitu kingine?

Kwa vyovyote iwavyo Mohamed Said ni kiungo muhimu sana katika vurugu zinazoendelea au zitakazotokea.
Ima ajitokeze kutufahamisha tusipomwelewa au ajifiche.
Kitu cha muhimu ni kuwa tunakumbu kumbu zake na tunazidurusu.

Mohamed Said uko wapi?

Naona yale maneno ya Barubaru yanaanza kuoneka kivitendo... Kuna hatari nchi hii ikagawika kama ilivyokua India na Pakistani. Zama za kuwaburuza waislamu zimekwisha.
 
quote_icon.png
By mwakaboko

katika zaidi ya post mbili hapa JF, nilimwambia wewe ni tatizo, akanitusi. Kwa fujo zinazoendelea sasahivi Mohamed Said in my view hatoki salama huyu ni muhimu serikali imfuatilie kujua his ABCs zinazohusiana na fujo hizi, yeye ameshiriki vipi. Hata kama hahusiki serikali ni muhimu ikijiridhisha.

Ni nani anamfadhili Ponda? ajulikane, Je, Mohamed Said ndiye mfadhili? serikali ijiridhishe

Tuwekee post aliyo kutusi Mohamed Said, kama hujaiweka, tunaomba ban kwako kwa kusema uongo.
 
analalamika kuwa kila akiandika makala zake JF zinafutwa au zinahamishwa toka kwenye siasa

nimemwambia aanzishe website yake kama wenzie akina ULIMWENGU
 
MM Brilliant!
Mohamed Said tafadhali sana karibu tujadiliane.
Hapa namnukuu 'Tutafika mahali pa kuita EU na AU watusuluhishe'

Sioni kwanini serikali imkamate Sheikh Ponda. Nasema hivi kwasababu haya tunayo yaona tumeyasema sana hasa katika thread za Mohamed Said. Tumetahadharisha sana kuwa tatizo si jamii, tatizo ni kundi la wasomi wachache wanaowatumia watu wenye ushaiwishi katika jamii zao kueneza chuki.

Sheikh Ponda ni kipaza sauti tu, chuki hizi nadiriki kuzisema wazi kuwa zimejengwa kwa usimamizi wa Mohamed Said.
Namkaribisha Mohamed Said hapa! tuendelee pale tulipoishia na hapa tulipo leo.

Mzee Said, all these upheaval and unrest have significant link with you.
Mohamed you have the onus to come out and tell fellow Tanzanian what's going on!

Nguruvi ina maana Mohamed Said akiondolewa (kifo - siombi hilo japo wote tutakufa, kufichwa, kufungwa nk), haya yote yanayotokea hapa TZ hayatatokea?
 
Kwa kweli ningependa sana kusikia msimamo wa mwanaharakati Mzee Mohammed Said hasa kufuatia haya yanayoendelea leo hii nchini na hasa kitendo cha serikali kumkamata Shehe Ponda Issa Ponda na kundi la vijana wa Kiislamu? Je inamkumbusha ile kamatakamata ya miaka ya sitini ambapo baadhi ya mashehe na wanasiasa wengine walikamatwa na aliyekuwa Shehe Mkuu kurudishwa Zanzibar?

Baadhi yetu tunatarajia kumsoma tena kwa makini akitupatia busara zake katika mlolongo wa matukio haya ambayo yanaonekana kuzidi kutugawa.

Mnajua ndugu zangu mnaoandika kama ulivyoandika na wengine wenye mtazamo wako, huwa nawashangaa sana. Tatizo sio Shehe Ponda na vijana hao wakiislam waliokamatwa, tatizo ni waislam kutoridhika na utaratibu uliopo ndani ya nchi yetu katika sekta mbali mbali ikiwa pamoja na elimu, ajira, utawala na kadhalika.

Ndugu zangu wakristo kweli miminawashangaa sana kwa tabia ya kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu sana. Kwa mfano, wewe unazungumzia kushikwa kwa Sheh Ponda, lakini hata siku moja hujajadili Barua ya Ponda aliyomuandikia Mh Benjamini Mkapa akiwa madarakani, ihusuyo uwiano usiolingana kati ya waislam na wakristo katika ajira za serikali. Mkapa alikubali kuwepo kwa tatizo hilo, kwahilo nilimsifu sana kwa vile hiyo ni hatua moja muhimu sana kama Rais wa nchi.

Baada ya hapo hakuna kilichofanyika. Lakini kibaya zaidi hoja zilizokuwa na ambazo zinaendelea kutolewa ni kuwa nyie waislam mlikimbia shule za Mission kwa kuogopa kulishwa Nguruwe. Ndio, hata mimi nisingeenda kusoma shule ambayo inabidi niiuze imani yangu kwa mbadala wa kitu fulani. Hii ni sawa na miaka ya hivi karibuni, kwa wahisani vijijini kutumia chakula kama njia ya kuwabadilisha watu dini. Kwa vile una njaa nitakupa mahindi lakini kwanza kuwa mkristo. Lazima wote tukubali kuwa haya yalikuwa makosa na kuwasifu wale waliokataa kwenda shule kwa ajili ya kulinda imani zao.

Ninachofahamu mimi Serikali yeyote makini huwekeza zaidi pale penye maendeleo hafifu ili napo pafikie level ya sehemu nyingine. Hata kwa sasa hivi Serikali huwekeza sana vijijini kwa vile huko maendeleo ni duni, kwa mfano miundo mbinu n.k Kwa hiyo huwa nawashangaa wote wasemao eti kwa vile mlichelewa basi iwe hivyo Tanzania yetu mpaka milele. Ukweli ni kwamba wote wenye mawazo hayo bado hawajafahamu kwanini au ni nini chanzo cha mauaji ya Halaiki kule Rwanda. Tatizo lile kwa wengi wanaliona kama Tatizo la kikabila, kumbe hali halisi ni Tatizo la kundi moja (watusi) kuwa juu sana kielimu, ajira na hivyo kuwa na awezo wa kumiliki rasilimali nyingi nchini humo.

Waisla hawadai matatizo hayo yatatuliwe leo au kesho, tunachotaka ni kuwepo utaratibu na mpango makini endelevu utaohakikisha kuwa hata kama kuna ajira chache tugawane sawa kwa kila makundi. Na mpango huu uanzie katika elimu na kuendelea. Mfumo huu wa elimu hatukuwa nao, ulipofika wote tumehamasishwa mpaka tukauelewa na wengine wakatangulia kuupenda kabla ya wengine. Sasa hatuwezi tukasema eti mmasai hauelewi huu utaratibu basi serikali imtose na waendelee na mchaga aliyeielewa shule mapema. Kweli hii si kazi ya serikali, serikali makini itawekeza zaidi kwa wamasai ili nao waonekane ofisini.

Leo hii mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari 252, ni mkoa unaoongoza Tanzania nzima, ndio ni vizuri lakini changamoto kubwa kwa serikali ni kujiuliza wafanye nini ili na Mtwara, Lindi, Pwani n.k nao wapate shule 252? Hii ndio changamoto kubwa na ningependa kuwaona wenzetu wakristo wanatoa ufumbuzi wa maswali haya magumu, kuliko kutoa hoja kuwa sisi tumeshaelimika ndio basi. Nyie wengine hamtatupata maana mliogopa nguruwe na hoja nyingine nyepesi.

Ndugu zangu wakristo tatizo si Ponda au Sheikh Farid bali ni vijana wote wa kiislam waliochoshwa na utaratibu uliopo. Panueni wigo wa kufikiri, ili tuwe pamoja katika kutatua matatizo haya.
 
analalamika kuwa kila akiandika makala zake JF zinafutwa au zinahamishwa toka kwenye siasa

nimemwambia aanzishe website yake kama wenzie akina ULIMWENGU

Huu ni ukweli, futa futa sasa hivi imetawala hapa JF. Ni hoja zenye muelekeo wa KI-JF, ndio zenye uhakika wa kubaki nyingine na bahati kubaki. Unajua mwezi huu tu wamefungiwa watu wangapi. Andika kuwa Waislam ni wadini hiyo itabaki, lakini ukibadili tu pale penye waislam ukaweka wakristo, thread itakaa dakika mbili tu na kutolewa. Sioni cha ajabu kwa vile hii ndio katiba ya JF.
 
Huu ni ukweli, futa futa sasa hivi imetawala hapa JF. Ni hoja zenye muelekeo wa KI-JF, ndio zenye uhakika wa kubaki nyingine na bahati kubaki. Unajua mwezi huu tu wamefungiwa watu wangapi. Andika kuwa Waislam ni wadini hiyo itabaki, lakini ukibadili tu pale penye waislam ukaweka wakristo, thread itakaa dakika mbili tu na kutolewa. Sioni cha ajabu kwa vile hii ndio katiba ya JF.

kuna ka ukweli hapa
 
Wanajamvi,
Hoja kubwa ni kumwalika Mohamed Said ili aje tujadiliane kuhusu mustakabali wa nchi. Kumwalika kunatokana na kauli na maandiko yake mengi ambayo ameyatumia katika kupandikiza chuki. Chuki ambayo ukimuuliza mwenye hiyo chuki hawezi kukuambi inatokana na nini zaidi ya kusikia au kusoma maandiko ya Mohamed.

Kuna mada zake nyingi zimekaa hapa jamvini kwa takribani miezi 4 au mitano zikijadiliwa kila siku.
Ukizitazama mada hizo hakuna anayekataa historia ya kile kinachoonekana au kuelezeka kama ni ukweli.
Kawawa alikuwepo huo ni ukweli, Mzee Kyaruzi alikuwepo huo ni ukweli. Kulikuwa na mikakati ya kupigania uhuru huo ni ukweli n.k.

Kilichogomba katika nyuzi zake ni pale alipojitahidi kuingiza udini na hata kutuhumu pasipo na ushahidi wa maandishi au mantiki zaidi ya hadithi za kutunga. Hapo ndipo alipokutana na maswali na kila mara akiulizwa swali linaloonekana kukinzana na dhana ya chuki au kushinda hoja ya dhana ya chuki, Mzee Said amekuwa mwepesi sana kusema anatoa mihadhara na kutembelea Ulaya. Siku zote hiyo ndiyo njia pekee ya kujibu maswali mazito.

Zawadi Ngoda, hoja zako ulizojadili nazo zilijadiliwa kwa kina. Kwa bahati mbaya Mohamed alipoulizwa anatoa suluhu gani hakuweza kuja na suluhu hata moja. Jibu kubwa alililosema serikali ikae waongee. Endapo hili ni tatizo la kitaifa kwanini asiweke hadharani kama anavyoweka mada zake? Kwanini atake kufanya yeye ndiye waislam wa Tanzania.

Katika hoja zako kama Mohamed, umeelezea vema kuhusu maeneo yaliyo hafifu kupewa kipaumbele.
Nakubaliana nawe kuwa hiyo ni kitu wanaita Positive Affirmative action.
Umetaja mikoa kama Mtwara na Lindi kwa uchache tu.
Ninachoshangaa ni kuwa mikoa hiyo ina watu wasio na dini, wasio amini, wakristo na Waislam. Kwanini basi wote wasiungane kama Watanzania waibane serikali Dodoma na hata ikiwezekana waonyeshe hasira zao mjengoni?

Kwa vile mgawanyo wa madaraka nao pia una matatizo, kwanini watu hao wasiungane na wabunge wao kwa pamoja bila itikadi zao ili waweze kukidhi haja ya kushinikiza serikali?

Kwanini tatizo la Lindi lihusishe kanisa la mbagala au kijichi. Je, kuchoma makanisa moto kutatoa jibu la tatizo au ni kulifanya tatizo liwe kubwa zaidi? Kama hilo linaweza kutoa jibu wapi ambapo limeweza kufanikiwa? Nigeria au nchi gani nyingine?

Tatizo hili halitaishia katika mgawanyo wa madaraka na elimu, ipo siku tutasikia kuwa waasia kwanini wanamiliki biashara kuliko watu fulani.

Na muhimu zaidi ni kuwa tatizo lilikuwa kunajisi Korani lililofanywa na mtoto wa miaka 12 au kulikuwa na matatizo mengine yaliyokuwa yanatafutiwa sababu?
Na kama yapo matatizo mengine je njia hiyo ni ya busara na hekima kwa jamii inayojitambua na kujiheshimu?

Umetoa mfano wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa na shule 252. Je, umeangalia kisayansi kwanini kuna shule nyingi huko?
Nani anamiliki na jamii inaitiikia vipi uwepo wa shule hizo?

Kibohehe seondari inamilikiwa na Waislam na ni shule iliyokuwa maarufu sana. Imetoa watu katika kada zote za kitaifa.
Je, kosa la Kibohehe kuwa Kilimanjaro ni lipi?

Lakini pia uangalie mabali zaidi ya hapo. Ni wapi duniani positive affirmative action imewahi kufanikiwa?
Je, upendeleo huo utasaidiaje Kilwa ambapo tayari kuna shule na wanafunzi wanakimbia bila wazazi, kamati za shule, wabunge, wananchi, mkuu wa Wilaya au Mkoa kufanya jambo?

Kwanini shikizo lizianzie kwa mkuu wa mkoa wa Lindi kwanza, kinyume chake lihalalishwe kwa kuchoma nyumba za ibada za watu wengine? Kama tatizo ni nyumba za ibada kwanini yasichomwe mahekalu ya wahindi waliofanikiwa kibiashara na kihali za maisha kuliko wengine?

Kikubwa zaidi, nafasi za ajira kama Engineering, Uhasibu, Udaktari na Ualimu unazaweje kuzigawa ili kuleta uwiano ulio sawa? Na mwisho kama tutatoa nafasi za upendeleo kwa Wakristo au Waislam, katiba ya nchi inawatetea vipi wasio na dini au wasioamini? Je, hawa hawana haki ya kupewa fungu katika mgao huo?

Nguruvi3
 
Napenda kukumbuka nukuu hii ya maalim Mohammed Said.

Hivi sasa kuna vitabu viwili vilivyoandikwa na Wakristo wenyewe vinavyothibitisha kuwa Wakristo wametumia nyadhifa zao katika serikali kuuhujumu Uislam na Waislam. Jan P van Bergen katika kitabu chake, Development and Religion in Tanzania,(1981) [1] ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa nao Rais Mstaafu, Nyerere dhidi ya Uislam na Waislam.

Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsi Nyerere wakati alipokuwa madarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Kanisa kuweka mikakati ya kuupa nguvu Ukristo.

Katika mikutano hiyo Nyerere aliwahakikishia viongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo. Kitabu hicho kinaeleza jinsi Nyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwa kuhakikisha kuwa anawapa Wakristo nafasi za juu katika serikali na chama. Kitabu hiki kilikuwa kinauzwa Catholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakini ilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwa kitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti na siri za Kanisa kuhusu njama dhidi ya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa. [1] Hadi hivi sasa kitabu hicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.

Kitabu cha pili ni cha Dr John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 (1992). [1] Kitabu hiki kinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalon anafichua kuwa kuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisa lilikuwa na hofu mbili.

Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislam kati ya Sunni, Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwa kwa makao makuu ya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwa linahofu kuwa mali walizokuwanazo Waasia Waislam zikitiwa katika harakati za Waislam ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukristo katika Afrika ya Mashariki. Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislam ni adui wake na ikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislam ili kuudhoofisha."

Ndugu yangu ikiwa unaishi kwenye nyumba ya nyasi usipendepende kucheza na kibiriti.
 
Mnajua ndugu zangu mnaoandika kama ulivyoandika na wengine wenye mtazamo wako, huwa nawashangaa sana. Tatizo sio Shehe Ponda na vijana hao wakiislam waliokamatwa, tatizo ni waislam kutoridhika na utaratibu uliopo ndani ya nchi yetu katika sekta mbali mbali ikiwa pamoja na elimu, ajira, utawala na kadhalika.


Ndugu zangu wakristo tatizo si Ponda au Sheikh Farid bali ni vijana wote wa kiislam waliochoshwa na utaratibu uliopo. Panueni wigo wa kufikiri, ili tuwe pamoja katika kutatua matatizo haya.

Tatizo la ndugu zenu ni kukimbilia KUTIBU badala ya kutafuta CHANZO.

Hawajui kuwa sasa mambo basiiiii, Liwalo na liwe.

Je HAutashangaa mtu mzima na akili zake'' AKITEMA ASALI NA KUTAMANI PILIPILI''?
 
Umenena kaka, nadhani pana watu wanatumwa kutuchanganya tusifikirie mambo ya msingi kuhusu maisha yetu na kutufanya tufikirie UPUUZI wao tu!
Mimi naona hii 'movie ya Sheikh Ponda' mnaichukulia very serious...
after one week tutakuwa tumeshasahau...
:embarrassed:
Leo hakuna anaezungmzia' movie ya Ulimboka' tena..


ndo Tanzania yetu hiii...

kila wiki ni new movie...
 
Nadhani watu wengi hatujamuelewa Mwanakijiji, yeye anataka Mohammed Said aje aseme kama kamata kamata ya viongozi wa kiislamu sasa hivi inalingana na ile ya miaka ya sitini. Wakati ule Rais alikuwa Nyerere ambaye Mohammed Said huwa anamlaumu kwa kuonea waislamu. Sasa hivi Rais ni muislamu na bado kuna kamata kamata ya viongozi wa kiislamu, yapi maoni ya Mohammed Said? Au mheshimiwa Rais hausiki?
 
Sasa naona shaka ya baadhi ya memba wa JF juu ya MMM inaweza kuwa kweli kuwa ni mtu hatari kwa ustawi wa Tanzania.Anamtakia nini mwandishi mchochezi ambaye fahamu zake ni chongo?
Huyu Mohamed Said ni kama Seidina Omari ambaye aliamuru matoleo mengine ya kuran yachomwe moto kwavile yako tofauti na ile aliyoandika yeye wakati usahihi wa nakala yake ulikuwa ni mashaka hata kwa maswahiba wengine wa karibu zaidi na mtume Muhamad.Mwandishi anayeangalia upande mmoja tu na kuacha sehemu nyingine ya ukweli hafai kwa jamii huru kwani uhuru unatokana na unalinda ukweli.

Sitaki na sitakuwa tayari kumwona mwandishi huyo mwenye fikra hasi juu ya nafsi yake na anayekwepa kujifunza kwa kuwasingizia wengine kuwa ni chanzoo cha uduni wake.Wote wenye mtazamo namna hiyo ni watumwa na watabakia katika utumwa wa fikra zao mbovu hadi pale watakabaini chanzo cha mtume Muhamad kuwaagiza wafuasi wake waifuate ilimu, hata kama inapatikana uchina.
 
Mimi naona hii 'movie ya Sheikh Ponda' mnaichukulia very serious...
after one week tutakuwa tumeshasahau...

Leo hakuna anaezungmzia' movie ya Ulimboka' tena..


ndo Tanzania yetu hiii...

kila wiki ni new movie...

Boss ya Ulimboka mbona mbali watu tumeshasahau hii ya juzi iringa..

attachment.php

Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.


attachment.php

Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.

attachment.php

Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
 
Back
Top Bottom