BVR ni Ufisadi mtupu - Dr Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi linaloendelea la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR.

Kiongozi huyo tishio kubwa kwa utawala wa CCM amesema alichojifunza akiwa nchini Marekani ni kwamba mbali ya Taifa hilo kuwa na teknolojia ya hali ya juu lakini hawatumii kitu kinachoitwa BVR

Dr Slaa amesema kuthibitisha ufisadi huo wa BVR hakuna uwazi uliofanyika kutoa tenda ya manunuzi ya vifaa hivyo.Ni wizi mtupu amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo aliyekuwa Marekani kwa ziara ya siku 10 ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari na wanachama walioenda kumlaki uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Wananchi kadhaa waliienda kumlaki walikuwa na mabango kadhaa hasa yale ya kumtambua kama Rais wa awamu ya Tano.

===================
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amerejea kutoka Marekani huku akieleza kuwa utoaji wa zabuni ya kuingiza nchini vifaa vya uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapigakura (BVR kits), ulikubikwa na ufisadi na usanii katika utoaji wa zabuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Njerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, baada ya kuwasili, alisema Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ilikataa zabuni ya kwanza ya uletaji wa vifaa hivyo nchini, lakini serikali ikachomeka suala hilo bila kutangaza zabuni kama taratibu na sheria zinavyoelekeza.

"BVR ni ufisadi na usanii na ndiyo maana hakuna anayejua na hawataki kutoka hadharani kueleza mzabuni alipatikanaje, PPRA walipokataa zabuni ya kwanza serikali ikaenda kuchomeka bila kutangaza zabuni," alisema.

Dk. Slaa alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imekuwa ikilalamikiwa kuhusiana na kuchelewa kuletwa kwa BVR, lakini dosari ya msingi katika suala la BVR ni serikali kushindwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivy0.

Alisema Agosti 30 na Septemba 8, mwaka jana, viongozi wa vyama vya siasa nchini walikutana na Rais Jakaya Kikwete

kujadiliana masuala kadhaa likiwamo la uandikishaji wa daftari la wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR na kukubaliana kuwa mambo ambayo siyo ya kikatiba na yasiyo ya lazima yasifanyike kwanza katika kipindi hiki ili kupunguza gharama.

Alisema miongoni mwa mambo waliyoyaomba yasifanyike kwanza ni kura maoni kwa ajili ya Katiba inayopendekezwa kwa kuwa siyo jambo la kikatiba, lakini katika hali ya kushangaza serikali ikatangaza tarehe ya kufanyika kura ya maoni licha ya kuwapo makubaliano hayo.

"Rais Kikwete alikubali na kupendekeza kuahirishwa kura ya maoni hadi baada ya uchaguzi mkuu ili kuokoa fedha ili zitumike kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, lakini hilo halikuzingatiwa," alisema.

Aliongeza kuwa hadi sasa serikali imetumia fedha nyingi sana kufanya kampeni kwa ajili ya kura ya maoni na cha kushangaza ni kuwa serikali ndiyo inayofanya kampeni badala ya wananchi.

Dk. Slaa alisema wamebaini kuwa kuandikisha wapiga kura kwa kutumia BVR ni mbinu inayofanywa na serikali kwa sababu kuna maeneo ambayo wananchi hawataandikishwa na ndiyo maana wameanza maeneo ambayo ni ngome za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Tunataka kuwaambia kuwa tumeshtukia na tunatoa rai kwa Rais Kikwete nchi hii ni muhimu kuliko yeye, nchi ni muhimu kuliko CCM na kuliko Chadema, hata siku moja upinzani hauwezi kuleta vurugu utaletwa na serikali yenyewe inayotaka kulazimisha mambo yake," alisema.

Hata hivyo, alisema kukwama kuandikisha wananchi katika daftari kwa kutumia BVR Chadema haiwezi kukimbilia mahakamani kwa sababu zipo kesi nyingi za Chadema ambazo hazijaanza kusikilizwa.

MAJIBU YA TUME
Alipoulizwa kuhusiana na madai hayo, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alisema mchakato wa kumpata mzabuni ulifuata taratibu zote za kisheria na kama kuna ambaye hakuridhika, alipaswa kukata rufaa kwa mujibu wa sheria.

Alipoulizwa kuhusu kampuni zilizoomba zabuni ya kuleta BVR, alisema aulizwe Mkurugenzi wa Nec, Julius Malaba.Hata hivyo, Malaba, alipoulizwa, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu.

Kuhusu madai kuwa uandikishaji unapendelea CCM, Jaji Lubuva alisema uandaaji wa ratiba hauangalii vyama bali waliangalia mikoa jirani na Mkoa wa Njombe ambao ulikuwa wa kwanza kuandikisha wapigakura.

AONYA UCHAGUZI MKUU
Dk. Slaa akizungumzia suala la uchaguzi mkuu unaoatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, alisema serikali isithubutu kuuahirisha kwa kuwa upo kwa mujibu wa katiba na kama inataka kufanya hivyo ijifunze katika nchi nyingine ambazo zimekumbwa na machafuko kwa sababu watawala wake wamekuwa ving'ang'anizi wa madaraka.

"Tunataka kumwambia Kikwete muda wake unaisha Oktoba 28, mwaka huu mpaka pale atakapoapishwa rais mpya," alisema.

Alimtaka Rais Kikwete apunguze ziara za nchi na badala yake atumie fedha kwenye daftari la kudumu la wapigakura ili wananchi wengi wapate fursa ya kupigakura.

ACT HAWANA UBAVU KWA CHADEMA
Akizungumzia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT) Wazalendo , alisema hakiwezi kuitisha Chadema hata kidogo.

"Chadema tumeijenga kuanzia ngazi za chini kwa miaka mingi, hatumuogopi yeyote. Dk. Slaa, Mbowe na timu nzima tumezunguka Tanzania nzima kijiji kwa kijiji, hivyo hakuna mtu yeyote atakayekuwa tishio kwetu," alisema.

AUPINGA MUSWADA WA MAKOSA YA MTANDAO
Kuhusu Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, alisema sheria hiyo haifai na kwamba atakuwa tayari kuwa mtu wa kwanza kufungwa kwa sababu haiwezekani mtu atumiwe ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake halafu anakamatwa na kushitakiwa.

"Hatuogopi kufungwa, mimi nitakuwa wa kwanza kwenda kupelekwa gerezani kwa sababu ninaamini kama nitaletewa meseji au jambo lolote litakalohusiana na hiyo sheria na nikapelekwa mahakamani ndiyo utakuwa ukombozi wa Taifa hili utaanzia hapo hapo," alisema.

Alisema ni kitu ambacho hakiwezekani kwenda kumshtaki mtu kwa kuandika mawazo yake, fikra zake kwenye mtandao bila kueleza ni fikra hizo zinakiuka vipi fikra za mwingine kwani kosa ni kukiuka haki ya mtu mwingine, lakini siyo kuandika fikra kwenye mtandao.

VURUGU AFRIKA KUSINI
Alisema vurugu nchini Afrika Kusini wanazofanyiwa raia wa kigeni zimetokana na serikali ya chama cha ANC kushindwa kuwahudumia vijana wake na kwamba hilo bomu linaweza kutokea hata Tanzania.

"Kuna vijana wengi hawana ajira, na ndiyo maana yanazaliwa makundi kama Panya road, Mbwa mwitu chanzo ni kukosa ajira," alisema.

Dk. Slaa alisema: "Ifike mahali Waafrika wawe watu wa demokrasia, mwenzao akikosea akavuruga demokrasia, unamwambia kwamba amekosea bila kuoneana aibu."

Alisema msingi wa ziara yake ni kwenda kujenga mahusiano Marekani na kwamba amejifunza mambo mengi.

ZIARA YAKE MAREKANI
Dk. Slaa alifanya ziara hiyo kufuatia mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana, Mike Pence, pamoja na taasisi mbalimbali za Marekani vikiwamo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wake na chama chake kisiasa na kijamii katika maendeleo ya Bara la Afrika.

Akiwa nchini humo alishiriki mijadala mbalimbali inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo lake kuu ni kuitangaza Tanzania na mihadhara kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indiana na Marion.

CHANZO: NIPASHE
 
Raisi wa awamu ya tano ameliona hili na ni kweli kabisa maana kinachofanyika kwa sasa na tume ni usanii tupu,mashine chache ili uchaguzi uahilishwe kwa manufaa ya ccm.
 
Rais wangu wa Nov 1 .......... 2015 , karibu nyumbani.... huku kuna wasaliti wako mbio kweli.....Wanadhani kujenga chama kunachukuwa miezi 6 tu....naomba uwape somo
 
Hapo mwanzo watawala walisema vitambulisho vya Uraia vitatumika kupiga kura..hii njiii ni ngumu
 
Rais wa moyoni kasema kweli kwani tangi waanze kuandikisha ni matatizo kibao na hakuna hata moja lililo patiwa ufumbuzi ni usanii mtupu
 
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi linaloendelea la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR.

Kiongozi huyo tishio kubwa kwa utawala wa CCM amesema alichojifunza akiwa nchini Marekani ni kwamba mbali ya Taifa hilo kuwa na teknolojia ya hali ya juu lakini hawatumii kitu kinachoitwa BVR

Dr Slaa amesema kuthibitisha ufisadi huo wa BVR hakuna uwazi uliofanyika kutoa tenda ya manunuzi ya vifaa hivyo.Ni wizi mtupu amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo aliyekuwa Marekani kwa ziara ya siku 10 ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari na wanachama walioenda kumlaki uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Wananchi kadhaa waliienda kumlaki walikuwa na mabango kadhaa hasa yale ya kumtambua kama Rais wa awamu ya Tano.

Source : ITV Habari

Kumcounter Dr. Slaa ujipange kweli kweli hili la BVR na Zimetoka China ni fukuto lingine ngoja tuone
 
Ajabu sana mpaka muda huu mapepo ya Lumumba hayajacharuka? Maana wakisikia jina la Dr Slaa mashetani ya kiccm na kikwao yanaanza kuchapana ngumi...!!!!!

Anyway hiyo ya Bvr Kiukweli ni maasi yajayo, kuna siri nzito iliyonyuma ya hiyo Makitu..!!

Kuna karenda iliyochapwa na Gazeti la Mwananchi ikionyesha Wakenya walitumia
13.000 kuandikisha wapiga kura 14.000.000ml kwa kipindi cha miaka mitatu...!! Wakati kule Nigeria walitumia Bvr 130.000 kuandikisha wapiga kura 40.000.000ml kama sijasahau kwa kipindi cha miaka minne...!!! Then sisi eti mpaka sasa tuna Bvr 250 plus 1.200 zinazokuja tukitaka kuandikisha wapiga kura 20.000.000 kwa kipindi cha Miezi minne..!!!!

Haya ni maajabu na kwakweli Mungu tu atusaidie Kwakweli Tanzania inakwenda kuandika historia ya machafuko makali kwa kuwahi kitokea kwasababu ya uroho wa madaraka wa watu wachache. Hili jambo linafanyika kana kwamba tulikuwa hatujui uchaguzi utafanyika lini, wakati jambo hili lipo kikatiba.

Ccm hii Ccm hiii....!!!!

BACK TANGANYIKA
 
10537268_304205009752932_1108764607_n.jpg

Mambo ya mzee Ole bwana!? YAANI KUTUA TU TAYARI, WATU WAANZE MCHAKAMCHAKA!
 
Ajabu sana mpaka muda huu mapepo ya Lumumba hayajacharuka? Maana wakisikia jina la Dr Slaa mashetani ya kiccm na kikwao yanaanza kuchapana ngumi...!!!!!

Anyway hiyo ya Bvr Kiukweli ni maasi yajayo, kuna siri nzito iliyonyuma ya hiyo Makitu..!!

Kuna karenda iliyochapwa na Gazeti la Mwananchi ikionyesha Wakenya walitumia
13.000 kuandikisha wapiga kura 14.000.000ml kwa kipindi cha miaka mitatu...!! Wakati kule Nigeria walitumia Bvr 130.000 kuandikisha wapiga kura 40.000.000ml kama sijasahau kwa kipindi cha miaka minne...!!! Then sisi eti mpaka sasa tuna Bvr 250 plus 1.200 zinazokuja tukitaka kuandikisha wapiga kura 20.000.000 kwa kipindi cha Miezi minne..!!!!

Haya ni maajabu na kwakweli Mungu tu atusaidie Kwakweli Tanzania inakwenda kuandika historia ya machafuko makali kwa kuwahi kitokea kwasababu ya uroho wa madaraka wa watu wachache. Hili jambo linafanyika kana kwamba tulikuwa hatujui uchaguzi utafanyika lini, wakati jambo hili lipo kikatiba.

Ccm hii Ccm hiii....!!!!

BACK TANGANYIKA

Dr Slaa katufumbua macho leo.
 
mpaka aende marekani kwanza na kisha kuja na hayo majibu si angesema wakati zikinunuliwa hii nakumbuka kuwa siasa za slaa ni kupinga kila jambo kama ilivyokuwa kipindi cha marekani na uchina.
 
Ndiyo maana unasikia zitaletwa kwa mafungu na eti ndege ya kukodi.This is ridiculous,ullishawahi hata sikia serikali imekodi ndege kuleta dawa nchini kwa kuwa pametokea uhaba na watu wanakufa?Then why this rubish BVR?I too smell something fishy at NEC
 
Back
Top Bottom