BVR ni Ufisadi mtupu - Dr Slaa

BVR ni Ufisadi mtupu - Dr Slaa

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi linaloendelea la uandikishaji wapiga kura kwa njia ya BVR.

Kiongozi huyo tishio kubwa kwa utawala wa CCM amesema alichojifunza akiwa nchini Marekani ni kwamba mbali ya Taifa hilo kuwa na teknolojia ya hali ya juu lakini hawatumii kitu kinachoitwa BVR

Dr Slaa amesema kuthibitisha ufisadi huo wa BVR hakuna uwazi uliofanyika kutoa tenda ya manunuzi ya vifaa hivyo.Ni wizi mtupu amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo aliyekuwa Marekani kwa ziara ya siku 10 ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari na wanachama walioenda kumlaki uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Wananchi kadhaa waliienda kumlaki walikuwa na mabango kadhaa hasa yale ya kumtambua kama Rais wa awamu ya Tano.

Source : ITV Habari
Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi la kujiandikisha,Mnyika amewahimiza wanachama wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na hata kwenye uzinduzi wa BVR mnyika alikuwepo na akapiga kambi wiki..naona Slaa anazeeka vibaya ukichanganya na vumbi la zito,,chadema kila mtu anaongea lake kama wanywa mataputapu
 
Kwa kifupi ni hivi; BVR= ESCROW...Na Watanzania watakuja shangaa siku watakayopewa 'bill' yao na hapo ndio ndio wastaajabu ni mafisadi gani wako nyuma ya hiyo bill mara baada ya uchaguzi...stay tuned!
 
Hivi Slaa ana hitaji nini? Anataka tutumie daftari la zamani?Mbona Mnyika na Mbowe wameu penda mfumo na kuhimiza wananchi kujitokeza?

Slaa tunaomba uoneshe huo ufisadi sio kuongea tuu!
 
Ajabu sana mpaka muda huu mapepo ya Lumumba hayajacharuka? Maana wakisikia jina la Dr Slaa mashetani ya kiccm na kikwao yanaanza kuchapana ngumi...!!!!!

Anyway hiyo ya Bvr Kiukweli ni maasi yajayo, kuna siri nzito iliyonyuma ya hiyo Makitu..!!

Kuna karenda iliyochapwa na Gazeti la Mwananchi ikionyesha Wakenya walitumia
13.000 kuandikisha wapiga kura 14.000.000ml kwa kipindi cha miaka mitatu...!! Wakati kule Nigeria walitumia Bvr 130.000 kuandikisha wapiga kura 40.000.000ml kama sijasahau kwa kipindi cha miaka minne...!!! Then sisi eti mpaka sasa tuna Bvr 250 plus 1.200 zinazokuja tukitaka kuandikisha wapiga kura 20.000.000 kwa kipindi cha Miezi minne..!!!!

Haya ni maajabu na kwakweli Mungu tu atusaidie Kwakweli Tanzania inakwenda kuandika historia ya machafuko makali kwa kuwahi kitokea kwasababu ya uroho wa madaraka wa watu wachache. Hili jambo linafanyika kana kwamba tulikuwa hatujui uchaguzi utafanyika lini, wakati jambo hili lipo kikatiba.

Ccm hii Ccm hiii....!!!!

BACK TANGANYIKA

Watasema watumie vitambulisho vya zamani kupigia kura.

Naona kuna mtu anataka kujiongezea muda wa kutawala.
 
Hivi Slaa ana hitaji nini? Anataka tutumie daftari la zamani?Mbona Mnyika na Mbowe wameu penda mfumo na kuhimiza wananchi kujitokeza?

Slaa tunaomba uoneshe huo ufisadi sio kuongea tuu!

Ukioneshwa utaishia kulalamika
 
Kwa kweli cyo siri nampenda nakumkubali kama Rais ajaye kwa kweli hakuna shaka Dr. Slaa pekee ndiye Rais wa mioyo ya watu ajaye naona Tanzania mpya nikimuangalia Dr. Slaa kama mkuu wa inchi
 
Naona kufisadi imekuwa ni agenda ya kawaida katika dili zote kubwa apa Tz.

EPA ESCRO BVR tutazoe tuu mpaka oct 2015 tutakapofanya maamuzi sahihi
 
Kwa kweli cyo siri nampenda nakumkubali kama Rais ajaye kwa kweli hakuna shaka Dr. Slaa pekee ndiye Rais wa mioyo ya watu ajaye naona Tanzania mpya nikimuangalia Dr. Slaa kama mkuu wa inchi

Watanzania wengi wamempachika jina la Nyerere wa Pili
 
Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi la kujiandikisha,Mnyika amewahimiza wanachama wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na hata kwenye uzinduzi wa BVR mnyika alikuwepo na akapiga kambi wiki..naona Slaa anazeeka vibaya ukichanganya na vumbi la zito,,chadema kila mtu anaongea lake kama wanywa mataputapu

Hujitambui wewe kichwani ni sawa na sifuri
 
Slaa amelaani na kupinga vikali zoezi la kujiandikisha,Mnyika amewahimiza wanachama wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na hata kwenye uzinduzi wa BVR mnyika alikuwepo na akapiga kambi wiki..naona Slaa anazeeka vibaya ukichanganya na vumbi la zito,,chadema kila mtu anaongea lake kama wanywa mataputapu

Slaa amezeeka vibaya, mchumba wake anampa stress
 
Hivi Slaa ana hitaji nini? Anataka tutumie daftari la zamani?Mbona Mnyika na Mbowe wameu penda mfumo na kuhimiza wananchi kujitokeza?

Slaa tunaomba uoneshe huo ufisadi sio kuongea tuu!

Hawa jamaa hawajielewi, they are confused, kila mmoja anazungumza yake!
 
Hata kiongozi wa mtaa anaongoza kuliko hiki chama, hivi inawezekana vipi mkoa mmoja ukaandikishwa zaidi ya miezi 2? nguvu zote ziko kwenye ku- deal na Gwajima. Shame ccm
 
Back
Top Bottom