white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,880
ila hili zoezi linahitaji moyo!! kwani kujiandikisha tu utadhani unaomba uraia wa USA!!Leo njoo unapewa namba, then kesho ndio uje kupigwa picha, na unakutana na wengine waliopewa namba juzi hawajaisha unaambiwa tena rudi kesho, yaani ni full shida kama huna nia ya dhati kuwa liwe jua iwe mvua lazima nipate kisu cha kumchinjia mkoloni mweusi, mbona unashindwa tu. Mimi nilikaa na namba mkononi siku 3!!ndio nakuja iona hiyo mashine live!! naanza tu kuigusa mala ohho imegoma njoo kesho!! nikawa mpole kesho yake ndio napata kadi, ni shida mno, tena kama dsm sijui kwani kila siku ni mishemishe umwambie mtu leo tunatoa kadi tu urudi kesho, yaani siku 2,mtu lazima upoteze kwa ajili ya bvr!! kama ni mkakati wao wa kuacha watu wengi wasijiandikishe wamefanikiwa, Eti unamsikia kiongozi wa Tume ya uchaguzi kuwa wamevuka malengo!!? kivipi sasa, kwani unakuta kijiji kina wakazi 5000,wamepewa mashine 4,kila mashine kwa sasa hata watu 100,kwa siku haziandikishi, na ni siku 7 tu!! sasa hayo malengo wanayoyavuka ni yapi jamani??!