Naona unatuwekea ka-skeleton tu, ongezea basi na ka-beef japo kidogo ili angalau tupate picha japo kwa mbali.
Mkuu nilizozipata, ni kwamba sasa hivi kuna mchuano mzito kati ya Membe, na Lowassa, wajumbe wengi wa cc, na wabunge, wanaridhika na kazi ya Membe, kama waziri wanasema he is doing a fine job, lakini kwenye kushika kaya hawawataki wote wawili, kwa hoja kwamba waliyoyaona na Mtandao, tayari yanatosha,
kwa hiyo waliamua kwa kauli moja na kumshinikiza Mwandosya, kugombea NEC, ili waanze kumtayarisha, nasikia huko Mbeya, kijana Tom alikuwa akishindana na almost 75%, ya cc na wabunge wa ccm, ndio maana hakuweza kuona ndani na alibidi akubali baada ya uchaguzi kuisha maana aligundua mwishoni mwiba uliomchoma,
Nasikia wenye uchungu na nchi sasa ni kumfagilia tu Mwandosya, mipango imeshaanza siku nyingi!
Kingunge alipojaribu kuleta kidomo domo, alinyamazishwa na hoja iliyotolewa na makamu na kuungwa mkono na Mama Zakhia, na mjumbe mmoja kutoka Zanzibar, na wajumbe wote baadaye, Hoja ni kwamba wabunge ni wamasai, wakati Lowassa, sio Mmasai, nasikia aliambiwa hii live huko ndani, akaambiwa kuwa wa-Mmasai huipigia kura ccm kwa asilimia 99.9%, hawajawahi kuwapigia upinzani, akambiwa kuwafukuza wabunge hao ni kuwapa Chadema majimbo ya bure maana watajiunga na Chadema na kugombea na watashinda, Muungwana akaulizwa kama anafahamu ni wa-Massai wangapi wanaoenda mahakamani kila hiyo kesi inaposomwa, akapewa namba rasmi, Muungwana, akaamuliza Kingunge, kama ameshawahi kwenda kwenye jimbo wakati wa uchaguzi mdogo wowote ule? Jawabu hakuna, akaambiwa yeye na ndugu yake wanyamaze, na hafukuzwi mtu!
Ahsante Mkuu!