Butiku apongeza serikali ya Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amepongeza ukaguzi wa vyeti pamoja na mfumo wa uchumi, unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.

Alisema kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha nidhamu na maendeleo ya nchi na kuwataka wananchi kumuunga mkono na sio kulalamika.

Butiku alisema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili, ambapo alisema kuwa kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa sheria na kanuni ambazo awali zilichezewa.

Alisema kushindwa kufuatwa kwa taratibu kulitengeneza mianya mbalimbali kwa wananchi kujiamulia mambo yao, huku wengine wakiichezea elimu ambayo ndio msingi wa taifa.

Butiku alionesha kukerwa zaidi na utitiri wa vyeti vya kufoji, uliokuwa umekithiri serikalini na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kukabiliana na hali hiyo sasa, kwa kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu walikuwa wamefikia hadi hatua ya kuwa na vyeti vya juu vya Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PHD), lakini vya kidato cha nne hawana.

“Kile kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa ahadi ya kurejesha mifumo ya nidhamu kwenye serikali, sasa kinachotakiwa ni kuunga mkono kwa kuhakikisha kuwa malengo ya Rais yanatimia kwa sasa,” alisema Butiku.

Alisema anashangazwa kwa uwepo wa wanafunzi hewa katika ngazi ya vyuo na hasa vyuo vikuu, kwa kusema kuwa hiyo ni ishara ya ukosefu wa umakini katika elimu.

“Mimi nikitoa mfano wa miaka yetu wakati tunasoma, ni matokeo yetu mazuri tu ndio yaliyokuwa yakitubeba na kuendelea zaidi ngazi za juu hadi mimi ninafikia kusoma Chuo Kikuu cha Makerere Uganda ni matokeo mazuri tu, lakini kuna muda hapa nchini ilikuwa fedha inaweza kukubeba,” alisema Butiku.

Butiku ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aligusia kuhusu mfumo wa sasa wa kiuchumi, ambapo alimpongeza Rais Magufuli kwa kurejesha fedha katika mfumo unaostahili.

Alisema kuwa ili uchumi uweze kusonga mbele ni dhahiri kuwa lazima fedha ziende kwa wazalishaji, akiwa na maana ya watu ambao wanazizungusha na kuendesha maendeleo.

Butiku alisema kuwa kwa sasa kinachofanyika ni fedha kurejea kwenye matumizi stahiki na yenye tija kwa nchi nzima, huku akiwalaumu wale wanaolalamika kuwa walikuwa wamezoea aina ya maisha ya matumizi na kwa sasa wanakabwa na upangwaji wa bajeti.

Alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni kuonesha umakini, hasa anapokabiliana na vitendo vya uovu hasa rushwa na ubadhirifu na kuwa hiyo inasaidia kurejesha heshima ya kimamlaka. Butiku alimtaka kutumia fedha zaidi katika kuimarisha mifumo ya elimu na hasa kuwasomesha vizuri vijana ili watumie elimu yao kwa tija ya taifa.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa ikishughulikia kwa kina suala la elimu kwa kuendesha misako ya kubaini watumishi hewa serikalini, pamoja na kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha, ambapo ni pamoja na kuzuia matumizi yasiyokuwa ya lazima hasa kwa watendaji wa serikali.

Chanzo: Habari Leo

Akizungumza katika ufunguzi wa Mhadhara wa tatu ulioandaliwa na Kavazi la Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi, Jaji Warioba alisema kuwa viongozi wa kisiasa siku hizi hawaendi kwa wananchi kuzungumzia sera na namna ya kutatua matatizo ya wananchi badala yake huenda kwa lengo la kushtakiana na kulalamika kwa wananchi kuhusu matatizo yao binafsi.

“Nilishasema wakati mmoja, huko nyuma viongozi wetu hawa…. akina Kahama (George Kahama, Waziri Serikali ya Awamu ya Kwanza) kazi yao ilikuwa ni kuhangaika na matatizo ya Taifa na matatizo ya wananchi. Siku hizi viongozi wanachukua matatizo yao wanataka wananchi ndio wayashughulikie,” alisema Jaji Warioba. “Yaani wananchi ndio sasa washughulikie matatizo ya viongozi,” aliongeza.

Kwa maelezo zaidi soma hapa;
Jaji Warioba akosoa hali ya kisiasa nchini, ‘inaongozwa bila sera’ - Dar24
 
WAKATI Tanzania ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema ana wasiwasi na Taifa la sasa kwani halina uadilifu, aliotujengea Mwalimu Nyerere.

“Kazi za kawaida kweli zinafanywa na zinaendelea, lakini sina uhakika hata kidogo kama uadilifu aliotuachia Mwalimu bado tunao, sijui nani wa kulaumiwa,” alisema Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa. Alisema kwa namna ambavyo mambo yanakwenda, ni kiashiria tosha kuwa nchi haina uadilifu tena.

“Mambo yanavyokwenda kama gari lililovunjika usukani,” alieleza Mwinyi na kuongeza kuwa kuna kila sababu ya kutafakari hali ilivyo sasa ikilinganishwa na ile ambayo iliachwa na Baba wa Taifa miaka hiyo 17 toka kufa kwake.

Alisema nafasi hiyo ya mazungumzo katika mdahalo, inawapasa kukaa kutafakari namna ya kurudisha nchi kwenye reli ambayo iliachwa na Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa taifa hili katika misingi ya uongozi.

Kwa maelezo zaidi soma hapa;
Mwinyi: Nchi haina uadilifu alioacha Mwalimu Nyerere
 
Nadhani siku hizi amekuwa mzee wa kung&[HASHTAG]#039[/HASHTAG];ata na kupuliza
AUGUSTINO MREMA ALIOMBA KAZI KIUTANITANI JUKWAANI AKAPEWA UENYEKITI WA PAROLE SASA HUYU BUTIKU USISHANGAE UKASIKIA INAANZISHWA BODI YA KIMBINYIKO NA BUTIKU AKAPEWA UWENYEKITI WA KUBINYA ANAVYOAMINI MAJUKWAANI
 
Nadhani siku hizi amekuwa mzee wa kung&[HASHTAG]#039[/HASHTAG];ata na kupuliza
POLE ZAKE SISI HUKU KWENYE VIJIWE VYA POMBE KUNA WENZETU TUNAOKUNYWA NAO HUWA TUNAWAFUKUZA KIJIWENI TUKIKUGUNDUA UNALEWA POMBE KILA UKIKUTANA NA WALEVI KABLA HUJANYWA POMBE KIJIWENI SASA HUYU NA MASTERS YAKE YA MAKERERE UNIVERSITY ANAJIONA MWANASIASA AU KASUKU
 
MsemajiUkweli

Tunaona jitihada zako za kusafisha au kule kwa malkia wanasema 'damage control'

Usiahau video ya Mzee Butiku aliyosema ' Sioni aibu kusema, chama CCM ndicho gwiji la Rushwa'

Hatujawahi kutawaliwa na chama kingine, pengine kukosekana kwa maadili ni zao la viongozi wanaopatikana kutoka chama alichosema Butiku ni gwiji la rushwa

Pili, Mzee Mwinyi yupo sahihi hakuna mwenye uhakika kama maadili ya Mwalimu bado yapo.

Inafika mahali kiongozi anaamuru watu wapigwe mitaani na Polisi yeye atajibu.

Halafu hachukuliwi hatua, bado tunatarajia maadili yatakuwepo!

Wenye dhama hawaoni ukosefu wa maadili, vipi tuwasote vidole vijana wadogo?
 
Huyo ni muongo..! Juzi tu hapa kasema Rais tembo!!! Leo anasifia nini? Huo ni unaaa tena uliopitiliza
 
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amepongeza ukaguzi wa vyeti pamoja na mfumo wa uchumi, unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.

Alisema kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha nidhamu na maendeleo ya nchi na kuwataka wananchi kumuunga mkono na sio kulalamika.

Butiku alisema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili, ambapo alisema kuwa kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa sheria na kanuni ambazo awali zilichezewa.

Alisema kushindwa kufuatwa kwa taratibu kulitengeneza mianya mbalimbali kwa wananchi kujiamulia mambo yao, huku wengine wakiichezea elimu ambayo ndio msingi wa taifa.

Butiku alionesha kukerwa zaidi na utitiri wa vyeti vya kufoji, uliokuwa umekithiri serikalini na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kukabiliana na hali hiyo sasa, kwa kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu walikuwa wamefikia hadi hatua ya kuwa na vyeti vya juu vya Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PHD), lakini vya kidato cha nne hawana.

“Kile kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa ahadi ya kurejesha mifumo ya nidhamu kwenye serikali, sasa kinachotakiwa ni kuunga mkono kwa kuhakikisha kuwa malengo ya Rais yanatimia kwa sasa,” alisema Butiku.

Alisema anashangazwa kwa uwepo wa wanafunzi hewa katika ngazi ya vyuo na hasa vyuo vikuu, kwa kusema kuwa hiyo ni ishara ya ukosefu wa umakini katika elimu.

“Mimi nikitoa mfano wa miaka yetu wakati tunasoma, ni matokeo yetu mazuri tu ndio yaliyokuwa yakitubeba na kuendelea zaidi ngazi za juu hadi mimi ninafikia kusoma Chuo Kikuu cha Makerere Uganda ni matokeo mazuri tu, lakini kuna muda hapa nchini ilikuwa fedha inaweza kukubeba,” alisema Butiku.

Butiku ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aligusia kuhusu mfumo wa sasa wa kiuchumi, ambapo alimpongeza Rais Magufuli kwa kurejesha fedha katika mfumo unaostahili.

Alisema kuwa ili uchumi uweze kusonga mbele ni dhahiri kuwa lazima fedha ziende kwa wazalishaji, akiwa na maana ya watu ambao wanazizungusha na kuendesha maendeleo.

Butiku alisema kuwa kwa sasa kinachofanyika ni fedha kurejea kwenye matumizi stahiki na yenye tija kwa nchi nzima, huku akiwalaumu wale wanaolalamika kuwa walikuwa wamezoea aina ya maisha ya matumizi na kwa sasa wanakabwa na upangwaji wa bajeti.

Alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni kuonesha umakini, hasa anapokabiliana na vitendo vya uovu hasa rushwa na ubadhirifu na kuwa hiyo inasaidia kurejesha heshima ya kimamlaka. Butiku alimtaka kutumia fedha zaidi katika kuimarisha mifumo ya elimu na hasa kuwasomesha vizuri vijana ili watumie elimu yao kwa tija ya taifa.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa ikishughulikia kwa kina suala la elimu kwa kuendesha misako ya kubaini watumishi hewa serikalini, pamoja na kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha, ambapo ni pamoja na kuzuia matumizi yasiyokuwa ya lazima hasa kwa watendaji wa serikali.
Chanzo: Habarileo.
Butiku anapalilia asiporwe kigoda chake mfuko wa Nyerere. Kulitumikia sharti ni uwe mnafiki.
 
Akizungumza katika ufunguzi wa Mhadhara wa tatu ulioandaliwa na Kavazi la Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi, Jaji Warioba alisema kuwa viongozi wa kisiasa siku hizi hawaendi kwa wananchi kuzungumzia sera na namna ya kutatua matatizo ya wananchi badala yake huenda kwa lengo la kushtakiana na kulalamika kwa wananchi kuhusu matatizo yao binafsi.

“Nilishasema wakati mmoja, huko nyuma viongozi wetu hawa…. akina Kahama (George Kahama, Waziri Serikali ya Awamu ya Kwanza) kazi yao ilikuwa ni kuhangaika na matatizo ya Taifa na matatizo ya wananchi. Siku hizi viongozi wanachukua matatizo yao wanataka wananchi ndio wayashughulikie,” alisema Jaji Warioba. “Yaani wananchi ndio sasa washughulikie matatizo ya viongozi,” aliongeza.

Kwa maelezo zaidi soma hapa;
Jaji Warioba akosoa hali ya kisiasa nchini, ‘inaongozwa bila sera’ - Dar24
Halahala Kipi kutumbuliwa.
 
MsemajiUkweli

Tunaona jitihada zako za kusafisha au kule kwa malkia wanasema 'damage control'

Usiahau video ya Mzee Butiku aliyosema ' Sioni aibu kusema, chama CCM ndicho gwiji la Rushwa'

Hatujawahi kutawaliwa na chama kingine, pengine kukosekana kwa maadili ni zao la viongozi wanaopatikana kutoka chama alichosema Butiku ni gwiji la rushwa

Pili, Mzee Mwinyi yupo sahihi hakuna mwenye uhakika kama maadili ya Mwalimu bado yapo.

Inafika mahali kiongozi anaamuru watu wapigwe mitaani na Polisi yeye atajibu.

Halafu hachukuliwi hatua, bado tunatarajia maadili yatakuwepo!

Wenye dhama hawaoni ukosefu wa maadili, vipi tuwasote vidole vijana wadogo?
Pamoja na nayo aliyosema Butiku bado hayafuti yale maneno yake kuwa " Hatutaki Rais Tembo' au "chama changu Ccm ndio kinara wa rushwa".
Mleta mada kasahau kuwa ni jambo la msingi kujadili challange hizo za Butiku kuliko sifa zake maana yeye bado ni mwanachama wa ccm.
Ni sawa na kujadili mtu anaye msifia mkewe kuwa ni mrembo, badala ya kujikita kuuliza kuna nini pale atakapo sema mke wangu anatabia mbaya!
 
Kwa pongezi lazima uonekane haraka sana mtoa mada, lakini pa kukosoa unaweza ukamchoma mtu na jambia.
 
nami naunga mkono ila ukaguzi uanzie juu mpaka chini.usibague maeneo tu.mfano wabunge, mawaziri na hata makatibu wakuu wapitiwe na zoezi hili....

Hii mizee na ife ipishe dunia, maana hakuna busara wanayoiacha kwa watoto. Uzee ni busara, hilo tunalikosa
 
hapa kuna kaharufu kwa UNAFIKI....,Mara hatutaki rais tembo.
Na mimi nasema sitaki rais swala,sungura,topi wala twiga maana wataleta ufisadi kwa kuwaogopa nyangumi,papa nyati,pofu na simba.NI BORA TEMBO maana kila mnyama ataogopa
MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO
 
Back
Top Bottom