Butiku apongeza serikali ya Rais Magufuli

Butiku apongeza serikali ya Rais Magufuli

nami naunga mkono ila ukaguzi uanzie juu mpaka chini.usibague maeneo tu.mfano wabunge, mawaziri na hata makatibu wakuu wapitiwe na zoezi hili....
Ninakubaliana na mtazamo wako.

Hili zoezi lisifanywe katika mtindo wa cherry picking.
 
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amepongeza ukaguzi wa vyeti pamoja na mfumo wa uchumi, unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.

Alisema kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha nidhamu na maendeleo ya nchi na kuwataka wananchi kumuunga mkono na sio kulalamika.

Butiku alisema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili, ambapo alisema kuwa kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa sheria na kanuni ambazo awali zilichezewa.

Alisema kushindwa kufuatwa kwa taratibu kulitengeneza mianya mbalimbali kwa wananchi kujiamulia mambo yao, huku wengine wakiichezea elimu ambayo ndio msingi wa taifa.

Butiku alionesha kukerwa zaidi na utitiri wa vyeti vya kufoji, uliokuwa umekithiri serikalini na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kukabiliana na hali hiyo sasa, kwa kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu walikuwa wamefikia hadi hatua ya kuwa na vyeti vya juu vya Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PHD), lakini vya kidato cha nne hawana.

“Kile kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa ahadi ya kurejesha mifumo ya nidhamu kwenye serikali, sasa kinachotakiwa ni kuunga mkono kwa kuhakikisha kuwa malengo ya Rais yanatimia kwa sasa,” alisema Butiku.

Alisema anashangazwa kwa uwepo wa wanafunzi hewa katika ngazi ya vyuo na hasa vyuo vikuu, kwa kusema kuwa hiyo ni ishara ya ukosefu wa umakini katika elimu.

“Mimi nikitoa mfano wa miaka yetu wakati tunasoma, ni matokeo yetu mazuri tu ndio yaliyokuwa yakitubeba na kuendelea zaidi ngazi za juu hadi mimi ninafikia kusoma Chuo Kikuu cha Makerere Uganda ni matokeo mazuri tu, lakini kuna muda hapa nchini ilikuwa fedha inaweza kukubeba,” alisema Butiku.

Butiku ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aligusia kuhusu mfumo wa sasa wa kiuchumi, ambapo alimpongeza Rais Magufuli kwa kurejesha fedha katika mfumo unaostahili.

Alisema kuwa ili uchumi uweze kusonga mbele ni dhahiri kuwa lazima fedha ziende kwa wazalishaji, akiwa na maana ya watu ambao wanazizungusha na kuendesha maendeleo.

Butiku alisema kuwa kwa sasa kinachofanyika ni fedha kurejea kwenye matumizi stahiki na yenye tija kwa nchi nzima, huku akiwalaumu wale wanaolalamika kuwa walikuwa wamezoea aina ya maisha ya matumizi na kwa sasa wanakabwa na upangwaji wa bajeti.

Alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni kuonesha umakini, hasa anapokabiliana na vitendo vya uovu hasa rushwa na ubadhirifu na kuwa hiyo inasaidia kurejesha heshima ya kimamlaka. Butiku alimtaka kutumia fedha zaidi katika kuimarisha mifumo ya elimu na hasa kuwasomesha vizuri vijana ili watumie elimu yao kwa tija ya taifa.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa ikishughulikia kwa kina suala la elimu kwa kuendesha misako ya kubaini watumishi hewa serikalini, pamoja na kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha, ambapo ni pamoja na kuzuia matumizi yasiyokuwa ya lazima hasa kwa watendaji wa serikali.
 
Zao lolote la Baba wa Taifa lazima limuunge mkono JPM! wanaolalamika acha walalamike
 
MsemajiUkweli

Tunaona jitihada zako za kusafisha au kule kwa malkia wanasema 'damage control'

Usiahau video ya Mzee Butiku aliyosema ' Sioni aibu kusema, chama CCM ndicho gwiji la Rushwa'

Hatujawahi kutawaliwa na chama kingine, pengine kukosekana kwa maadili ni zao la viongozi wanaopatikana kutoka chama alichosema Butiku ni gwiji la rushwa

Pili, Mzee Mwinyi yupo sahihi hakuna mwenye uhakika kama maadili ya Mwalimu bado yapo.

Inafika mahali kiongozi anaamuru watu wapigwe mitaani na Polisi yeye atajibu.

Halafu hachukuliwi hatua, bado tunatarajia maadili yatakuwepo!

Wenye dhama hawaoni ukosefu wa maadili, vipi tuwasote vidole vijana wadogo?
Nguruvi3
Kwanza ninakubaliana na wewe kwenye suala la rushwa. Ni kweli CCM ni gwiji la rushwa. Tuliona mpaka kwenye mchakato wa kupata mgombea Urais wa Tanzania.

Pili, ninakubaliana na wewe pia kwenye suala la maadili. Kumbuka chama ambacho ni gwiji la rushwa haliwezi kuwa na maadili. Maadili yameanza kumomonyoka siku ambayo taifa liliingia kwenye uchumi wa soko huria kupitia Maamuzi ya Zanzibar ya mwaka 1991 yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM.
 
Tatizo kubwa la vijana "mnaoshabikia" ufipa kwa sasa ni uelewa mdogo, japo najua kuna idadi si haba ya mnaolipwa kwa kuendesha kampeni chafu.
Waliyaongea Mwinyi, Butiku, na Warioba ni sahihi na kwa kiasi kikubwa hayapingani na utawala uliopo, ila mamluki wa ufipa wameamua kufanya "distorted enterpretation" na wanaendelea kuwa"bamba" mamluki wao.
Ukweli ni kwamba utawala uliopo unaungwa mkono kwa kiasi kikubwa sana na kundi kubwa la wasomi, wanasiasa, wanamageuzi, wanaharakati wa kweli, na wananchi wa kawaida.
Tuendelee kuvuta subira, wanafiki kwenye joho la "wanasiasa" wa upinzani waendelee kuumbuka.
 
Nguruvi3
Kwanza ninakubaliana na wewe kwenye suala la rushwa. Ni kweli CCM ni gwiji la rushwa. Tuliona mpaka kwenye mchakato wa kupata mgombea Urais wa Tanzania.
Lakini ukweli CCM walimtema Lowasa baada ya kunuka rushwa

Pili, ninakubaliana na wewe pia kwenye suala la maadili. Kumbuka chama ambacho ni gwiji la rushwa haliwezi kuwa na maadili. Maadili yameanza kumomonyoka siku ambayo taifa liliingia kwenye uchumi wa soko huria kupitia Maamuzi ya Zanzibar ya mwaka 1991 yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM.
Ongera kwa kuongea ukweli, mchakato wa uchaguzi aliyeongoza kwa kutoka rushwa ni Lowasa.
Na la pili umesema palipo na rushwa hamna maadili, kwa hiyo Lowasa na Kote alikokubaliwa hamna maadili
 
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amepongeza ukaguzi wa vyeti pamoja na mfumo wa uchumi, unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John
Magufuli.
Alisema kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha nidhamu na maendeleo ya nchi na kuwataka
wananchi kumuunga mkono
na sio kulalamika.

Butiku alisema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili,
ambapo alisema kuwa
kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa sheria na kanuni ambazo awali zilichezewa.

Alisema kushindwa
kufuatwa kwa taratibu kulitengeneza mianya mbalimbali kwa wananchi kujiamulia mambo yao, huku wengine wakiichezea elimu
ambayo ndio msingi wa taifa.

Butiku alionesha kukerwa zaidi na utitiri wa vyeti vya
kufoji, uliokuwa umekithiri serikalini na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kukabiliana na hali hiyo sasa, kwa kufanya
uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu walikuwa
wamefikia hadi hatua ya kuwa na vyeti vya juu vya Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PHD), lakini vya kidato cha nne hawana

“Kile kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa ahadi ya kurejesha mifumo ya nidhamu kwenye serikali, sasa
kinachotakiwa ni kuunga mkono kwa kuhakikisha kuwa malengo ya Rais yanatimia kwa sasa,” alisema Butiku.

Alisema anashangazwa kwa uwepo wa wanafunzi hewa katika ngazi ya vyuo na hasa vyuo vikuu, kwa kusema kuwa hiyo ni ishara ya
ukosefu wa umakini katika elimu.

“Mimi nikitoa mfano wa miaka yetu wakati tunasoma, ni matokeo
yetu mazuri tu ndio yaliyokuwa yakitubeba na kuendelea zaidi ngazi za juu hadi mimi ninafikia kusoma Chuo Kikuu cha Makerere
Uganda ni matokeo mazuri tu, lakini kuna muda hapa nchini ilikuwa fedha inaweza kukubeba,” alisema
Butiku.

Butiku ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aligusia kuhusu mfumo
wa sasa wa kiuchumi, ambapo alimpongeza Rais Magufuli kwa kurejesha fedha katika mfumo unaostahili.

Alisema kuwa ili uchumi uweze kusonga mbele ni dhahiri kuwa lazima fedha ziende kwa wazalishaji, akiwa na
maana ya watu ambao
wanazizungusha na kuendesha maendeleo.

Butiku alisema kuwa kwa sasa kinachofanyika ni fedha kurejea kwenye
matumizi stahiki na yenye tija kwa nchi nzima, huku akiwalaumu wale wanaolalamika kuwa walikuwa wamezoea aina ya maisha ya matumizi
na kwa sasa wanakabwa na upangwaji wa bajeti.

Alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni kuonesha
umakini, hasa anapokabiliana na vitendo vya uovu hasa rushwa na ubadhirifu na kuwa hiyo inasaidia kurejesha heshima ya
kimamlaka. Butiku alimtaka kutumia fedha zaidi katika kuimarisha mifumo ya elimu na hasa kuwasomesha vizuri vijana ili watumie
elimu yao kwa tija ya taifa.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa
ikishughulikia kwa kina suala la elimu kwa kuendesha misako ya kubaini watumishi hewa serikalini, pamoja na kukabiliana na matumizi
mabaya ya fedha, ambapo ni pamoja na kuzuia matumizi yasiyokuwa ya lazima hasa kwa watendaji wa serikali.

Chanzo: Habari Leo

Huyu mzee si ndio yule aliesema hawataki Rais tembo? Sijui nn maana ya usemi ule
 
Huyo ni muongo..! Juzi tu hapa kasema Rais tembo!!! Leo anasifia nini? Huo ni unaaa tena uliopitiliza
Mkuu;
Huwezi kuelewa mantiki ya Rais Tembo kama umesoma vichwa vya habari kwenye magazeti na kutoa hitimisho.

Jaribu kusoma habari yote au angalia video kuhusiana na dhana ya Rais Tembo.
 
Huyu mzee anabiashara gani? Au nayeye anasheli ya mafuta?
 
Butiku anapalilia asiporwe kigoda chake mfuko wa Nyerere. Kulitumikia sharti ni uwe mnafiki.
Wala msihangaike na post hii mtapoteza muda wenu tu, chanzo chenyewe gazeti la Habari Leo, tena ni mahojiano na mwandishi! Wala msimfikirie vibaya mzee Butiku, labda waweke video ya mahojiano hayo kama wanayo!
 
Back
Top Bottom