Busara zenu wana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Busara zenu wana JF

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by STIDE, Jan 16, 2012.

 1. S

  STIDE JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kheri ya mwaka mpya wana Jf kila pande mlipo.
  Wandugu, mwishoni mwa mwaka jana nilijitambua kuwa sistahili kuendelea kuishi peke yangu ktk dunia hii, hivo niliamua kwenda home kutafta atakae nifaa. Namshukuru Mungu nilimpata.
  Ndugu zangu wana Jf, ktk mazungumzo yetu tulikubaliana kupima(tulifanya hivo) kabla ya jambo hili kulifikisha kwa wazazi.
  Tatizo ni kwamba wazazi(upande wa binti) wanatia uzibe kwamba tuko majirani sana pale kijijini na mimi ni Mkristo nae ni Muislam!! Mzazi mmoja (kiume) hana noma sana ila mwingine ni noma!
  Nimejaribu kutumia watu ili kushawishi juu ya jambo hili lakini wapi!!
  Binti mwenyewe anasema "japo ni busara kuwasikiliza wazazi wake maana ndo wamemfikisha hapa hadi namuona lakini kama wataendelea kutia ngumu BASI TUBEBANE TU!"
  Je wandugu nifanyeje maana natamani sana kufunga ndoa? Kubebana sitaki!! Wandugu mpaka sasa nimerudi kibaruani ugaibuni najiuliza la kufanya!!
  BUSARA ZENU JAMANI!!
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  sasa unataka umfurahishe nani? Unakumbuka maneno ya Steve Jacobs(RIP)?
   
 3. S

  STIDE JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nafsi yangu tu mkuu!!
   
 4. ram

  ram JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Bishanga Heri ya mwaka mpya! Siku nyingi sijakuona kwa jamvi.
  Mmependana wawili sasa huyo watatu anatoka wapi STIDE?

   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Rudi utafute mwingine wa dini yako...usitake bifu na wakwe zako,utakosa amani bure na yeye pia...sijaona umesema unampenda sana!

  Anyway, kila la kheri...kubebana is not a good option.
   
 6. S

  STIDE JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu Ram, kama nilivoeleza, kubebana sitaki, nahitaji kumaliza kila kitu ktk mpangilio sahihi lakini je bila huyu wa tatu kumuweka sawa nitafanikisha vp?
  Ni jinsi gani nitamuweka sawa? Ushauri kaka.
   
 7. S

  STIDE JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu sihitaji shari na mtu ndo maana nahitaji kuwaweka sawa.
  Kuhusu "kumpenda sana" nilisahau tu mkuu ila nampenda sana na ndo maana niko tiyari kutoa mahari!!
  Asante kwa ushauri wako kama vp ongezea kidogo!!
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Waombe wazazi wako au wazee wengine wenye kuheshimika uliowaacha huku Tanzania waende wakazungumze na hao wazazi, na binti nae azidi kuwashawishi mkuu,ni hayo tu nayoweza kuongeza.
   
 9. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama wao hawataki na mtoto wao abadili dini na wewe unampenda badili wewe dini uchukue mkeo,, la haiwezekani kubebana sio mtindo poa sababu ni muhimu sana kupata baraka za wazazi wa pande zote mbili,kama itashindikana itakua hukujaliwa kua na yeye.....
   
 10. ram

  ram JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Anaeleta shida hapo ni mama mkwe, baba mkwe hana noma, jaribu kumuomba babamkwe wako aongee na huyo mama kwa kina amuelezee faida ya binti yao kuolewa, kuolewa ni jambo la heri jamani, la yeye akishindwa basi ajaribu kufanya kikao na wazee wenye hekima wa familia zote mbili ili wajaribu kumshawishi huyo mama. Huyo mama nae kapitwa na wakati anataka akae na huyo binti hapo hadi lini, Akitia ngumu mwache, Mungu ni mwema atakuaptia mke mwema, hakuna kitu kibaya ndugu yangu kama mgogoro wa dini. Na ndo watashanga binti yao atakapowaletea mapacha wasio na baba hapo home

   
 11. S

  STIDE JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ubarikiwe sana mkuu!!
   
 12. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  yalaaaaaa yani wewe upo majuu alafu totoz yupo bongo!! hamna kitu hapoa wala usijisumbue wangu. potezea kabisaaaaaa
   
 13. salito

  salito JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Kwani wewe unataka kufunga ndoa ipi stide??ya kiislam,kanisan au bomani??
   
 14. S

  STIDE JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante sana Kaka
   
 15. S

  STIDE JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwanini Mkuu?
   
 16. S

  STIDE JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ya Kikristo mkuu! NI DHAMBI KWA MUNGU KWANI!!??
   
 17. ram

  ram JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  STIDE mimi ni dada, bt usijali, karibu, hapa huwa hapaharibiki jambo. All da best

   
 18. S

  STIDE JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  SAMAHANI na usijari ni vijimambo tu!
   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu ndie uliyekuwa unamuullizia hapa chini?????????


   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole bro,ila nakushauri tafuta namna ya kumshawishi huyo mzazi km unaingalia furaha ya badae pia,
  Japo sipo ndoan ila tunaona mifano mingi na matokeo ya watu kubebana kisa wanajiridhisha wenyewe kwa vile tu wamependana,
  Kumbuka yule ni mzazi wake hataweza kuwa na bifu naye siku zote za maisha yake,je ikitokea maishan humo akashawishiwa na wazazi na akaamua kenda kuwaomba radhi na kufuata matakwa ya mzazi wake ww utakuwa kwenye position gani?
  Amin kwa sasa ndio mmeanza mapna na huwa ni matamu sana mwazeza amua lolote bila kjali kesho nn cha weza tokea,
  Nakushauri km huyo mzazi atakomaa,mpen muda huku mkiendelea kumbembeleza,km atagoma basi amin huyo hakuwa wako mwombe mungu akupe wako wa dini yako.
   
Loading...