Busara Itangulie kwa wana JF

Busara Itangulie kwa wana JF

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,500
Reaction score
7,431
Palikuwepo mke & mume ambao walipendana sana, ila hawakuwa na mtoto hatimae wakaamua kumfuga paka kama mwanao. Baadae mke alishika mimba wakapata mtoto, walifurahi na kumlea kwa upendo wote. Siku moja wakiwa wanapunga hewa bustanin mtoto walimuacha ndan kalala, ghafla walimwona paka wao akija amelowa damu akiwa na kipande cha nyama mdomon. Bila kuchelewa mke alishika gongo na kumpiga yule paka kichwan hatimae paka alipoteza maisha papo hapo. Walipoingia ndan walimkuta mtoto akiwa amelala kama walivyomwacha, na pemben mwa kitanda palikuwepo JOKA kubwa alieuawa na yule paka... Ebu nipe jb umejifunza nini?
 
Fikiri kabla ya kutenda

hasira hasara
 
Moral of the story:umdhaniae ndiye siye,usituhumu bila uchunguzi wa kina.

Bora angemtuhumu alafu akafanya uchunguzi mwisho akatoa HUKUMU!siunajua Tuhuma sio Kosa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom