Usafiri mzuri wa kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam mida ya jioni

Paa

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
1,449
2,924
Ni heri?

Watu wazuri wa Mungu, wenyeji wa mkoa wa Arusha na waliowahi kusafiri kutoka Arusha kwenda Dar, huwa mnatumia usafiri gani mida jioni kuanzia saa kumi?

Kwa muda huo wa jioni ninaweza kupata basi?

Na kama nisipopata basi, nikaamua kusafiri asubuhi, naomba mapendekezo ya basi zuri luxury ambalo haliwekwi muziki kwa sauti ya juu ambayo inakua kero, lenye siti nzuri na safi, lisilokuwa na harufu zisizoeleweka.

Pia pendekezo la sehemu nzuri ya kupumzika(lodge/inn/hotel) ambayo haiko mbali sana na stendi ya basi

Mbarikiwe.
 
Back
Top Bottom