Mara nyingi sana moto wa kwenye bus huanzia kwenye fuse box(siyo Mara zote). Ukiangalia mazingira ya hilo bus in wazi tu mfumo wa umeme haukua sawa, hivyo huenda wakati dereva amewasha taa.. Ile full,..dim... Full... Dim fuse ikapiga short na kuanza kuungua mdogo mdogo. Mara nyingi sana ukifungua fuse box ya magari makubwa unakuta kuna fuse kadhaa zinadalili ya kuungua.
Kuhusu kuwa kitonga usiku ule ni sawa! Safari ya kutoka Arusha mpaka kitonga kwa Bus zima so chini ya masaa 10 kwa wastani wa 80kph maana Arusha- Kitonga kuna kama 800km+ kidogo... Kwahiyo ukiweka sehemu za kutembea 50kph, ukiweka ratiba ya sumatra, ukiweka vituo kadhaa vya hapa na pale kutia ndani kituo chao kikubwa cha Morogoro bus likiwahi sana basi kitonga litapandisha SAA 4 usiku hivi ukichangia na ubovu wa hayo magari ndiyo kabisaa.
Ila kuna jambo moja naliona kwa hood.. Nahisi mzee anatakiwa abadilishe management.. Marco polo Andare ni body ngumu na nzuri sana, ikitunzwa vizuri inaweza kwenda miaka na miaka! Ukiangalia kampuni zingine Abood na Kilimanjaro Exp wote hawa bado wanazo body za Marco polo Andare G5 na G6.. Tena zina gari zao zina usajili wa namba A kama tu hizi za Hood.. Ila za hood zimechoka sana.. Hazina matunzo, mzee Hood ni lazima abadilike, wenzie wa na Andare za namba DG.. Pia wana michina ya kutosha, halafu wanapitia njia ya Babati-Dom- Iringa .. Na yeye aongeze Bus lingine lipite njia hiyo.