Bus la hood lashika moto mlima kitonga

Bus la hood lashika moto mlima kitonga

Xavier Africa

Senior Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
180
Reaction score
386
Habari wanajamvi nikiwa njiani kwenda tunduma usiku huu nimekuta bus la hood likishika moto na kuteketea lote maeneo ya mlima kitonga hakuna majeruhi wala hasara kwa abilia iliyotokea nimeshindwa kupiga picha
 
Mara nyingi mizigo ya abiria hasa MIZITO hufungiwa katika CHAMBERS za kuhifadhia mizigo PEMBEZONI MWA GARI kwa nje kulia na kushoto .... katika issue ya moto inakuaje rahisi kuokoa kila kitu na pasitokee madhara yoyote kwa mali za abiria?
 
Aysee yani limeungua lote na bado huoni kuwa hayo ni madhara tosha?? Au madhara ni kifo tu?? Mbona kusema limeungua lote hio ni hasara tosha?
Pia nawaza imekuwaje au abiria walishuka wote wakaenda nunua kiberiti wakakaa pembeni na kushusha mizigo yao then kuwasha moto na kucheki movie?

Rud ukapige picha au google ata ya uongo itumike kwa niaba basi.
 
Hivi hayo mabasi bado yapo!!!? I last saw them in 2010
 
Aysee yani limeungua lote na bado huoni kuwa hayo ni madhara tosha?? Au madhara ni kifo tu?? Mbona kusema limeungua lote hio ni hasara tosha?
Pia nawaza imekuwaje au abiria walishuka wote wakaenda nunua kiberiti wakakaa pembeni na kushusha mizigo yao then kuwasha moto na kucheki movie?

Rud ukapige picha au google ata ya uongo itumike kwa niaba basi.
Kwa taarifa ilivyo inaweza ikawa ni kweli ama kwa kuwa ni usiku labda kakurupuka kutoka usingizini na alikuwa yupo ndotoni.Samahani mkuu ni mawazo tu.
 
Mara nyingi mizigo ya abiria hasa MIZITO hufungiwa katika CHAMBERS za kuhifadhia mizigo PEMBEZONI MWA GARI kwa nje kulia na kushoto .... katika issue ya moto inakuaje rahisi kuokoa kila kitu na pasitokee madhara yoyote kwa mali za abiria?

Inawezekana dalili zamoto zilianza mbele mwa Bus wakati watu wote wameshuka na haukuenea haraka, kila kitu chawezekana ndugu, usiwe na wasiwasi!
 
Ujumbe huu umeandikwa dka 45 zilizoisha sasa hili basi limeungua sangapi huwa wanaruhusiwa kutoka mbeya saa 10 usiku au, mwingine hapo juu kasema eti alisikia lilikuwa likitokea arusha swali kwake lilifika muda gani mlima kitonga, tunaomba ufafanuzi tafadhali hamjaeleweka hapa.
 
Mara nyingi mizigo ya abiria hasa MIZITO hufungiwa katika CHAMBERS za kuhifadhia mizigo PEMBEZONI MWA GARI kwa nje kulia na kushoto .... katika issue ya moto inakuaje rahisi kuokoa kila kitu na pasitokee madhara yoyote kwa mali za abiria?
Moto ulianzia mbele taratibu wakafanikiwa kuokoa kutokana na maelezo ya nilio wauliza
 
Ujumbe huu umeandikwa dka 45 zilizoisha sasa hili basi limeungua sangapi huwa wanaruhusiwa kutoka mbeya saa 10 usiku au, mwingine hapo juu kasema eti alisikia lilikuwa likitokea arusha swali kwake lilifika muda gani mlima kitonga, tunaomba ufafanuzi tafadhali hamjaeleweka hapa.
Kwa taarifa ilivyo inaweza ikawa ni kweli ama kwa kuwa ni usiku labda kakurupuka kutoka usingizini na alikuwa yupo ndotoni.Samahani mkuu ni mawazo tu.
Sa hiv ni alfajiri sio usiku
Ajari imetokea usiku mimi nimepita saa kumi kasoro nikitokea dar
 
Ujumbe huu umeandikwa dka 45 zilizoisha sasa hili basi limeungua sangapi huwa wanaruhusiwa kutoka mbeya saa 10 usiku au, mwingine hapo juu kasema eti alisikia lilikuwa likitokea arusha swali kwake lilifika muda gani mlima kitonga, tunaomba ufafanuzi tafadhali hamjaeleweka hapa.
Yaan kwa hii mibasi ilivyo hovyo siku hizi yawezekana kabisa ilitokea arusha na usiku huu likawa kitonga...

Mwaka juzi nilitokea mbeya na Hood nikafika kesho yake asubuh mabasi mengine yanatoka stend na hatukulala njiani zaid ya ubovu wa gari....

Kutoka stend kuu kituo kinachofuata ni nanenane na hapo gari iliharibika tukasubiri hadi saa mbili gari nyingine ikaletwa.....

Kufika mafinga gari hoi tena matengenezo kama masaa mawili hivi....

Tukaenda hadi Morogoro ambapo tulifika saa mbili usiku ( kwa kipindi kile gari ya dodoma/arusha ilikuwa ilitakiwa kufika saa 8 na nusu mchana hadi saa 9 mchana). Morogoro tukakaa zaidi ya masaa mawili gari ikitengenezwa ko gereji yao....

Tukaanza safari tena tukiwa moshi kukaanza pambazuka na tukafika Arusha asubuhi...

Haya magari sio kabisa yamechoka mbaya sijui ilikuwaje wamiliki wameshindwa kuendesha kampuni na sasa inakufaa.....

Ilitakiwa awe na magari mapya kwa sasa sio yale ya zamani.
 
Mara nyingi mizigo ya abiria hasa MIZITO hufungiwa katika CHAMBERS za kuhifadhia mizigo PEMBEZONI MWA GARI kwa nje kulia na kushoto .... katika issue ya moto inakuaje rahisi kuokoa kila kitu na pasitokee madhara yoyote kwa mali za abiria?

Mleta mada anasema amepita akaona linashika moto, kuna maswali mengi ya kujibu kama unavyodokeza, kama ndiyo lilikuwa linashika moto na hakuna hasara, kama aliweza kujua hakuna hasara alishindwaje kuchukua picha ...a one second action anyway
 
Back
Top Bottom