Mambo mengine mnajisemea tu! Hivi Taifa kama Ufaransa likihamua kufanya kweli Rwanda ina uwezo gani wa kushindana nalo?
Wafaransa wakisema enough is enough PK na wapambe wake si watashikwa kama kuku wa kienyeji tu, yakawatokea kama ya Gabgo na mkewe - maoni yako nafikiri yako yako geared for home consumption only - nchi zote ulizo zitaja zilihamua kuwa ignore sio kwamba hawana uwezo wa ku-deal nanyi mkashindwa pa kutokea.
adhabu pekee waliyoifanya Rwanda dhidi ya ufaransa ni kuamua kubadili lugha ya kifaransa na kujiunga na kiingereza na kujiunga na commonwealth...ujue Rwanda limekuwa koloni la ufaransa miaka mingi sana na hadi sasa ufaransa ilitaka waendelee kuwa chini yao, sasa ufaransa ilipoona wanawakimbia ikabidi wajibembeleze ili wasikimbie. lakini hata hivyo ufaransa wangetaka, wangeweza tu kuwapa silaha waasi wa FDLR ambao walikuwa wakiwasapoti tangu kabla kagame hajatwaa kigali, silaha nzuri za kumpindua kagame na kuweka utawala wao, Kabila wasingeweza kumtumia kwasababu yeye ni Mnyarwanda sio mcongo. vilevile, wangeweza kutumia hata tz kutoa silaha na kupitishia waasi wapitie hapa kwetu kumpindua, na ujue mkwere alienda ufaransa kipindi kile na kagame aliogopa sana akijua mwisho wake umefika, ndo maana alifyata mkia.
unachotakiwa kujua ni kwamba, Kagame kwa sasa hana uwezo hata wa kupigana na Burundi, hawezi kukubali icho kitu kitokee,....amekajenga kale kanchi kwa garama kubwa sana, amesacrifice vitu vingi kuijenga kigali, na anapenda rwanda iendelee kuwa na mazingira mazuri kuvutia wawekezaji, na vimajengo alivyojenga hataki vibomolewe kwasababu ni hivyo tu anavyo nchi nzima, hakuna sehemu kama kigali. kuruhusu tz kuingia kupigana, kungevuruga uchumi wote ambao aliujenga, kungevuruga wawekezaji, na anajua uchungu wa vita ulivyo, hakuna vita ambayo haina hasara. vyote alivyovijenga kwa miaka mingi vitadondoshwa ataanza upya, sasa hakuna mtu mweney akili anayeweza kukubali icho kitu na kuingia vitani wakati ana foresee hali kama hiyo itatokea. the same would apply to Burundi, haina kitu cha kupoteza, na kuingia vitani, wawekezaji watajua kuwa rwanda kuna vita na Burundi na hawatakuja na uchumi utayumba. na ujue Rwanda ni nchi ndogo sana, kama mkoa mmoja tu wa tz, hivyo vita ikianza upande mmoja unaathiri nchi nzima. Burundi pia wanayo advantage kwasababu FDLR wako committed kwenye vita kuliko waasi wa kiburundi, hivyo akiingia vitani, Nkrunzinza anaweza tu akawa anapigana na wakati huohuo anawasapoti FDLR kijeshi na kuwapa njia ya kupitia kuingia Rwanda....na ujue hakuna kitu kagame anakiogopa kama FDLR kwasababu anawajua walivyo imara na wanavyomchukia na anajua wakipata nafasi tu hawawezi kupoteza lazima wamrudishe msituni,,,,na kagame hataki kuacha ikulu uzee wote ule arudi kupigana msituni......
kwa sababu hizo, Rwanda wanaiogopa Burundi kuliko chochote na wanaogopa vita kwasababu atakayekula hasara zaidi ni Rwanda na sio Burundi. ujue Burundi wamewa accuse sana Rwanda kusapoti waasi , jambo ambalo kagame anajua kama wakiingia vitani, burundi pia itasapoti fdlr ambao kagame anawaogopa halali usingizi. na nkurunzinza anaweza kufanya hivyo kulipiza kisasi akawapatia njia au eneo la kutulia pale burundi na huku akisubiria kagame aingie nchini mwake atangaze kwamba amemvamia, then yeye anajibu na hapohapo anapata support ya FDLR. who will lose then?
hapo Kagame ataomba Mungu Tanzania tuwe upande wake, kwasababu kama sio hivyo, tungepitisha silaha kwenda burundi na ujue vita ni silaha wala sio maneno ya mdomoni.