real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Burundi imepiga marufuku umiliki wa laini mbili za simu kutoka kwa kampuni moja inayotoa huduma za mwasiliano ya simu.
Idhaa moja ya redio ya Bonesha FM imeripoti kuwa imepata taarifa hiyo kutoka kwa wizara ya fedha.
Kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano ya simu zimepewa kipindi cha miezi miwili kutekeleza sheria hiyo mpya.
Kampuni hizo zitalazimika kusajili wamiliki wote wa laini za simu la sivyo wataadhibiwa na faini ya takriban dola $3,000 kwa kila laini ambayo itatumiwa pasi na kusajiliwa.
Sheria hii mpya imewekwa baada kutokea machafuko ya kisasa kwa takriban mwaka mooja sasa. Machafuko nchini humo yalianza mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu.
Wapinzani wake wanasema kuwa hatua hiyo ya Nkurunziza inakiuka katiba ya taifa inayomzuia rais kuongoza kwa zaidi ya miaka 10 ama mihula miwili.
Nigeria iliiadhibu kampuni ya mawasiliano ya MTN faini ya dola bilioni 5.2 kwa kuendelea kuruhusu utumizi wa simu ambazo hazijasajiliwa.
Rais Muhammadu Buhari aliilaumu MTN kwa kuruhusu wapiganaji wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi nchini humo kwa kuruhusu laini za simu ambazo hazijasajiliwa kuendelea kutumika hata baada ya ilani ya kutofanya hivyo.
Chanzo: BBC