SI KWELI Burkina Faso yalipa deni lote la taifa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Huku kwetu kila kukicha deni linazidi kupaa na maisha kuzidi kuwa magumu. Na hapo tunajinasibu kuwa na amani na utulivu.

Burkina Faso mbali ya kuwa katika machafuko kwa muda mrefu, kwa miaka 2 tu Traore kaweza kulipa deni la taifa la Dola Bil. 4.

Halafu Tanzania Wasira anajisifu kuwa deni ni la enzi na enzi huku Bi. Mkubwa akijisifia kupokea 'vijisenti' vya mkopo ambavyo hata la maana hatulioni zaidi ya anasa za Mama hiki na Mama kile.

Millard Ayo hawezi kuripoti habari kama hii. Media za bongo kazi ni kusifia upumbavu tu.

1743598653725.png
 
Tunachokijua
Burkina Faso ni nchi inayopatikana Magharibi mwa Afrika ikiwa imepakana na mataifa kama vile Mali na Niger. Nchi hiyo inaongozwa na kiongozi wa kijeshi Captain Ibrahim TRAORÉ aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa Marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Madai

Kumekuwepo na taarifa inayodai kuwa Rais wa Burkina Faso Ibrahim traore amelipa deni lote la serikali lilikodiriwa kuwa ni Dola bilioni 4. Tangu Ibrahim ashike madaraka katika Taifa hilo zimekuwepo taarifa nyingi ambazo si za kweli kumuhusu yeye na taifa lake huku miongoni mwa mzalishaji maudhui mkubwa anayefanya hivyo anajulikana kama African Hub katika mtandao wa X.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa hayana ukweli. Burkina Faso haijalipa madeni yake yote anayodaiwa na hakuna uthibitisho unaoleza kuwa Burkina Faso wamekamilisha deni wanalodaiwa.

Ufuatiliaji umebaini Burkina Faso ina mikopo kotoka maeneo mbalimbali ikiwemo kutoka shirika la fedha la kimataifa (IMF) Aidha taarifa za mwaka 2024 zinaonesha kuwa Burkina Faso ilipokea mkopo wa sawa na ziaid ya Bilioni 130 za kitanzania.

Ripoti ya shrika la kimataifa la fedha (IMF) ya madeni kati ya Machi 01, 2025 hadi April 01, 2025 inaonesha kuwa Burkina Faso inadaiwa zaidi ya Dola Milioni 324.
Huku kwetu kila kukicha deni linazidi kupaa na maisha kuzidi kuwa magumu. Na hapo tunajinasibu kuwa na amani na utulivu.

Burkina Faso mbali ya kuwa katika machafuko kwa muda mrefu, kwa miaka 2 tu Traore kaweza kulipa deni la taifa la Dola Bil. 4.

Halafu Tanzania Wasira anajisifu kuwa deni ni la enzi na enzi huku Bi. Mkubwa akijisifia kupokea 'vijisenti' vya mkopo ambavyo hata la maana hatulioni zaidi ya anasa za Mama hiki na Mama kile.

View: https://www.instagram.com/p/DHyRVijMniJ/?igsh=YXBldHJvdHZvZHc3

Unaweza weka transactions,credible sources,document,inayonesha hilo deni lilivyolipwa lote?
 
Hio ni fake news mkuu hakuna sehemu yoyote ile ukienda kwenye bank ya dunia na imf kufuatilia bado hutakuta kuwa burkinafo wanadaiwa sana
 
Mkuu jaribu kupitia hiyo ripoti alafu angalia baadhi ya mambo ndani ya nchi ya burkinafaso .....kuna vitu bado haviko sawa

Hio ni fake news mkuu hakuna sehemu yoyote ile ukienda kwenye bank ya dunia na imf kufuatilia bado hutakuta kuwa burkinafo wanadaiwa sana
Wamesema Deni la ndani .
Na hata la nje atalimaliza .
Utawala wa kijeshi ni utawala wa KiMungu maana ni Mungu wa majeshi. Miaka 2 amefanya mambo makubwa kuliko maraisi mafisadi wote Afrika .

Mbona hamtaki Waafrika wajiegemea wenyewe bila kunyonywa na kuuana .

Hivi Tanzania huoni kuwa ni aibu miaka 65 ya uhuru tuna pesa kama ambayo sio nembo ya Taifa bali dili la watu.

Pesa gani inayobadilishwa picha na mwonekano na saini yake kila baada ya miaka 5 .
Yaani baada ya miaka mitano pesa imeisha muda wake .

Nchi ya tatu duniani kwa kuwa na madini ya dhaha lakini haina hata akiba ya hata tan tano kumi za madini .
Gram moja ya dhahabu ni tshs 200K
Ukiwa na Tani Kumi ni sawa na Tsh tril.2 .

Hii nchi ningepewa kwanza kuna watu kama 2000 hivi ningewafyelelea mbali baada ya hapo miaka 10 ungekuwa kama Norway . Magereza yote tangefungwa kwasababu wafungwa wote wangekua wafanyakazi wanaolipwa migodini na mashambani .
Kila mtanzania baada ya hiyo miaka 10 angekua anawekewa pesa ya Kula kwa mwezi kwenya akaunti yake ya benki au Mpesa isiyopungua 500K.

Hapo ningekuwa nimewaangamiza wachache wasiozidi 2000 na kuwaokoa mamilioni ya Watangayika maskini na kuwa na Taifa lisilo na madeni wala ukosefu wa ajira wala uhalifu.
Ukiiba tu unakula chuma .
Hakuna kupoteza watu wema halafu unaacha mafisadi hiyo ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu .

Ukiwa na Tani 1000 tu za dhahabu basi ni tril.200 . Bajeti ya miaka mitano bila mikopo wala deni lolote .

Wazungu walikuja kwa teknolojia duni ya Miaka hiyo lakini walijenga Afrika na Ulaya kwa madini kidogo sana waliyochukua na kuacha akiba kubwa sana .

Mfano Tanzania wakoloni hawakuchukua dhahabu nyingi wakati wa ukoloni maana hapakuwa na migodi mikubwa ya dhahabu zaidi ya mgodi wa Almasi kule Mwadui .
Leo migodi iko mingi ya dhahabu lakini dhahabu inachorwa deni linaongezeka ,Watawala wanakua matrilionea na Mafisadi wakishirikiana na hao wawekezaji kuiibia nchi . Machawa wanashangilia . Ni Mungu wa majeshi tu aingilie Kati Ni reform No Election ifanikiwe .

Mama anaupiga mpunga mwingi.
Mia Tano tena 😂😂😂😂
 
Huku kwetu kila kukicha deni linazidi kupaa na maisha kuzidi kuwa magumu. Na hapo tunajinasibu kuwa na amani na utulivu.

Burkina Faso mbali ya kuwa katika machafuko kwa muda mrefu, kwa miaka 2 tu Traore kaweza kulipa deni la taifa la Dola Bil. 4.

Halafu Tanzania Wasira anajisifu kuwa deni ni la enzi na enzi huku Bi. Mkubwa akijisifia kupokea 'vijisenti' vya mkopo ambavyo hata la maana hatulioni zaidi ya anasa za Mama hiki na Mama kile.

Millard Ayo hawezi kuripoti habari kama hii. Media za bongo kazi ni kusifia upumbavu tu.

View: https://www.instagram.com/p/DHyRVijMniJ/?igsh=YXBldHJvdHZvZHc3

Unalinganisha mtu mwenye akili timamu na mataaaaahi!!
 
Wamesema Deni la ndani .
Na hata la nje atalimaliza .
Utawala wa kijeshi ni utawala wa KiMungu maana ni Mungu wa majeshi. Miaka 2 amefanya mambo makubwa kuliko maraisi mafisadi wote Afrika .

Mbona hamtaki Waafrika wajiegemea wenyewe bila kunyonywa na kuuana .

Hivi Tanzania huoni kuwa ni aibu miaka 65 ya uhuru tuna pesa kama ambayo sio nembo ya Taifa bali dili la watu.

Pesa gani inayobadilishwa picha na mwonekano na saini yake kila baada ya miaka 5 .
Yaani baada ya miaka mitano pesa imeisha muda wake .

Nchi ya tatu duniani kwa kuwa na madini ya dhaha lakini haina hata akiba ya hata tan tano kumi za madini .
Gram moja ya dhahabu ni tshs 200K
Ukiwa na Tani Kumi ni sawa na Tsh tril.2 .

Hii nchi ningepewa kwanza kuna watu kama 2000 hivi ningewafyelelea mbali baada ya hapo miaka 10 ungekuwa kama Norway . Magereza yote tangefungwa kwasababu wafungwa wote wangekua wafanyakazi wanaolipwa migodini na mashambani .
Kila mtanzania baada ya hiyo miaka 10 angekua anawekewa pesa ya Kula kwa mwezi kwenya akaunti yake ya benki au Mpesa isiyopungua 500K.

Hapo ningekuwa nimewaangamiza wachache wasiozidi 2000 na kuwaokoa mamilioni ya Watangayika maskini na kuwa na Taifa lisilo na madeni wala ukosefu wa ajira wala uhalifu.
Ukiiba tu unakula chuma .
Hakuna kupoteza watu wema halafu unaacha mafisadi hiyo ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu .

Ukiwa na Tani 1000 tu za dhahabu basi ni tril.200 . Bajeti ya miaka mitano bila mikopo wala deni lolote .

Wazungu walikuja kwa teknolojia duni ya Miaka hiyo lakini walijenga Afrika na Ulaya kwa madini kidogo sana waliyochukua na kuacha akiba kubwa sana .

Mfano Tanzania wakoloni hawakuchukua dhahabu nyingi wakati wa ukoloni maana hapakuwa na migodi mikubwa ya dhahabu zaidi ya mgodi wa Almasi kule Mwadui .
Leo migodi iko mingi ya dhahabu lakini dhahabu inachorwa deni linaongezeka ,Watawala wanakua matrilionea na Mafisadi wakishirikiana na hao wawekezaji kuiibia nchi . Machawa wanashangilia . Ni Mungu wa majeshi tu aingilie Kati Ni reform No Election ifanikiwe .

Mama anaupiga mpunga mwingi.
Mia Tano tena 😂😂😂😂
mkuu Nipe evidance kutoka Burkinafaso inayo someka kuwa kamaliza deni la ndani nami nisome ......Ndio shida yangu ....SIAMINI KWENYE MANENO BILA USHAHIDI
 
Vijana wengi hawapendi kusoma wala kufuatilia ndio maana unakuta hata Polisi na usalama wa taifa wanashiriki kuiba kura ili CCM ishinde bila kujua kua mtu anayeiba karatasi za kura kamwe haitaacha kuiba pesa.

Yaani Mkurugenzi anafanya njama ili kura ziibiwe halafu mkurugenzi huyo huyo anasimamia mabilioni ya pesa za Halmashauri . Mtu anatengeneza njama za kuiba kura halafu unamwamini asimamie pesa za Umma akishirikiana na Madiwani na Mbunge ni walioiba naye kura . Hawa ni Fisi waliopewa kazi ya kulinda Bucha .

Rais anashinda kwa wizi wa kura na Rushwa halafu anakwenda kumteua waziri wa fedha aliyeshinda kwa Rushwa na wizi wa kura .
Pesa zinazotengwa kila mwaka za kulipa madeni zinakwenda wapi .
Zinaishia mifukoni mwa watu wachache na Deni linakua badala ya deni kupungua.

Kwa nini uweke utaratibu wa kuwalipa watu pesa za Safari kama huna uwezo wa kuwalipa na kwa nini umpe mtu safari wakati unajua kuwa pesa za safari zinaliwa na wasioenda kwenye hiyo safari .
Wabunge walikua wanaandikiwa safari hata kama hawakwenda na wanalipwa lakini huko kwenye idara za umma wana madeni .
Deni litaishaje?

Jeshi ndio mpango mzima wa kuwaondoa vibaka kwenye nchi yoyote duniani .
 
Unaweza weka transactions,credible sources,document,inayonesha hilo deni lilivyolipwa lote?
Wewe unayo simu ya kupapasa unashindwaje kuipapasa na ukapata ukweli, mbona ya hovyo unaweza kuyapata unashindwaje hili!
 
HIZI NI BAADHI YA NEWS AGENCIES KUBWA HAPO BURKINA FASO NENDA KATAFUTE SEHEMU GANI WAMEWEKA CHAPISHO LA KUMLIZA DENI LA KIMTAIFA MKUU ALAFU UKIMALIZA NENDA KWENYE TOVUTI ZA SERIKALI KUTAFUTA ILO CHAPISHO ASANTE

Shirika la Habari la Burkina Faso (AIB) - Hili ni shirika linaloendeshwa na serikali ambalo hutoa habari juu ya maswala ya kitaifa na kimataifa yanayohusiana na Burkina Faso.

Radio Omega - Kituo maarufu cha redio kinachotangaza habari, vipindi vya mazungumzo

Le Faso Net - Tovuti ya habari ya mtandaoni ambayo inashughulikia mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na siasa, jamii, na utamaduni nchini Burkina Faso.

L'Observateur Paalga - Moja ya magazeti yanayoongoza nchini Burkina Faso ambayo hutoa habari na uchambuzi wa matukio ya sasa nchini.

B24 - Chombo cha habari cha dijiti ambacho hutoa habari juu ya Burkinabé na hafla za kimataifa, kwa kuzingatia yaliyomo kwenye video na kuripoti mkondoni.
 
Nani anaweza kuyafilisi mafisadi papa hiyo hela ikatumika kulipa deni?
 
Back
Top Bottom