Buriani Saidi Alli Masimango, tunakukumbuka Daima

Buriani Saidi Alli Masimango, tunakukumbuka Daima

Mkuu umenisikitisha sana japokua mimi ni mkristo safi siungi mkono huu ujinga wako wakristo hawako hv....pole sana nasriya pole barubaru....poleni wafiwa wote Mungu ampumzishe kwa Amani

Shukran sana mkuu.

Nadhani wewe ni miongoni mwa wema kabisa.

Na tuseme ukweli tu kuwa hizi jamii mbili za wakristo na waislam hapo awali ndani ya taifa hili zimekuwa zinaishi kwa upendo na aman kabisa na mshikamano wa kindugu wa utaifa.

Pamoja na tofauti zetu za dini na iman haikutokea watu kusemeana maneno ya chuki kias hiko.

Lakini kuibuka kwa baadhi ya viongoz na watu wasio na heri kwenye kizazi hiki kilichopandikizwa na kilichopita ndicho kimesababisha taharuki na uwepo wa watu kama hao.

Wengine km sisi tunareact haraka sana.
 
sasa wewe ndio bure kupita maelezo..HUNA BUSARA WALA STAHIMILI.. watu wa aina ya jamaa huyo wapo na wataendelea kuwepo... unachotakiwa kuwapuuza maana wamepanga kukera watu kwa makusudi..SASA WEWE UMEUINGIA MTEGO WAKE..KAMA UMEFUNGA LEO HEBU FANYA KUTIA CHAI BAAI huku ukisubiri BAN

Sasa wewe ukitaka amjibu vipi??
 
RIP mzee,

Nilikuwa sijui, nilimfahamu wakati nafanya Field NSSF miaka ya nyuma kwenye kitengo cha ICT pale makao makuu, alikuwa amezama kweli kweli kwenye computing.
 
Mkuu umenisikitisha sana japokua mimi ni mkristo safi siungi mkono huu ujinga wako wakristo hawako hv....pole sana nasriya pole barubaru....poleni wafiwa wote Mungu ampumzishe kwa Amani

jina lake ni mbwa wa manzese naomba muachane nae
 
Sasa wewe ukitaka amjibu vipi??

Sa na wewe unaunga mkono?
Kusema kweli ahmed didat nae ana majibu ya ovyo. Wakianza hao wenzetu kutukana na yeye huja na mitusi yake. Kwani sisi tunaopuuza tu wajinga?
 
Last edited by a moderator:
Sa na wewe unaunga mkono?
Kusema kweli ahmed didat nae ana majibu ya ovyo. Wakianza hao wenzetu kutukana na yeye huja na mitusi yake. Kwani sisi tunaopuuza tu wajinga?

Uko sahihi nakubali.

Tunatakiwa kupuuza.

Lakin sometimes anaekutukana kilabuni ili hali wewe ni mpita njia tu huna unalolijua na wewe mtukane kilabuni hapo hapo.

Baadae hawakawii hawa...utaskia oooh samahani nilikua nimelewaa.

Sasa ujinga huo nani anataka.

Wanatukana kila siku wanadhani sisi hatujui hayo matusi??

Ajabu ukiripot kwa mods hawafanywi chochote.

Thats why sometimes watu huona potelea mbali.

Enough is enough na liwalo na liwe.

Sasa wewe hayo matusi ya huyo mbwa jike wa manzese yanavumilika yale??

Umeona mods wakimpa adhabu yule?

Potelea mbali.
 
Lkn ukumbuke tumeusiwa kuh kuutumia ulimi ipaswavyo. Tuongee maneno ya kheri na mazuri. Na sio matusi. Dhambi nyingi zinatokana na ulimi. Basi tunoweza kujiepusha tuepukane nalo. Hasa kwa mwezi huu wa Ramadhan na hasa kwa kumi hili la mwisho.
 
Uko sahihi nakubali.

Tunatakiwa kupuuza.

Lakin sometimes anaekutukana kilabuni ili hali wewe ni mpita njia tu huna unalolijua na wewe mtukane kilabuni hapo hapo.

Baadae hawakawii hawa...utaskia oooh samahani nilikua nimelewaa.

Sasa ujinga huo nani anataka.

Wanatukana kila siku wanadhani sisi hatujui hayo matusi??

Ajabu ukiripot kwa mods hawafanywi chochote.

Thats why sometimes watu huona potelea mbali.

Enough is enough na liwalo na liwe.

Sasa wewe hayo matusi ya huyo mbwa jike wa manzese yanavumilika yale??

Umeona mods wakimpa adhabu yule?

Potelea mbali.

Ahali yangu,
Kinachotakiwa ni KUHISHIMIANA NA SIO KUVUMILIANA. Kwani siku zote mkihishimiana hakutakuwa na dharau wala mas'khara katika matendo yenu ya kila siku.

Naunga mkono hoja.
 
Ahali yangu,
Kinachotakiwa ni KUHISHIMIANA NA SIO KUVUMILIANA. Kwani siku zote mkihishimiana hakutakuwa na dharau wala mas'khara katika matendo yenu ya kila siku.

Naunga mkono hoja.

Shukran sana Alhabiby Baru Baru.

Nikutakie Ramadhan Kareem.
 
Uko sahihi nakubali.

Tunatakiwa kupuuza.

Lakin sometimes anaekutukana kilabuni ili hali wewe ni mpita njia tu huna unalolijua na wewe mtukane kilabuni hapo hapo.

Baadae hawakawii hawa...utaskia oooh samahani nilikua nimelewaa.

Sasa ujinga huo nani anataka.

Wanatukana kila siku wanadhani sisi hatujui hayo matusi??

Ajabu ukiripot kwa mods hawafanywi chochote.

Thats why sometimes watu huona potelea mbali.

Enough is enough na liwalo na liwe.

Sasa wewe hayo matusi ya huyo mbwa jike wa manzese yanavumilika yale??

Umeona mods wakimpa adhabu yule?

Potelea mbali.

Jamiiforums wakristo wana haki zaidi sisi tuvumilie tu.ila kikweli jamiiforums inabidi iitwe christian thinkers.maana mwanzo walikuwa peke yao wakawa wanatukana tu liwali na liwe jamiiforums ni christian thinkers
 
kumbe vijana wa zamani wa kariakoo walikuwa wanasoma hivyo! Da siku hizi sijui nini kimeingia kama si kuimba taarabu na bongo fleva basi ni kuwa punda, utandawazi huu,tumejifunza ujinga. R.I.P brother kwa historia yako iliyo tukuka. Mungu awape faraja wafiwa.
 
Mbona Kariakoo ndio chimbuko la kila kitu hata Uhuru wa Tanganyika vuguvugu lake lilianzia hapo. We soma kitabu cha Mohamed Said kinachoitwa HISTORIA YA TANGANYIKA ILIYOSAHAULIKA. Hapo alidadavua wazee hao walivyokuwa makini katika kutafuta ilmu na uhuru wa nchi yenu.

Ahsantum nakutakaia Eid Mubarak!

Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.

Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.

Buriani Saidi Alli Masimango.
Ilikuwa taarih 23 July 2013 saa kumi na nusu alfajr saa za Oman, nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu Zulekha Haji Sheikh wa Mbezi beach ,Dar es salaam akinifahamisha msiba wa ndugu yetu, rafiki yetu na mwanafunzi mwenzetu Saidi Ali Masimango. Msiba huu ulitokea nyambani kwake huko Dar es salaam kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua sana ugonjwa wa kisukari.. Na kuzikwa siku ya taarih 24 July 2013 baada swala ya adhuhur katika makaburi ya kisutu , Dar es salaam.

Kwa leo ningepende kumzungumzia nilivyomfahamu marhum Said Alli Masimango tokea tukiwa pamoja shule ya msingi Gerezani darasa la nne mwaka 1977. Nakumbuka wakti huo Said Masimango alikuwa akiishi mtaa wa Kariakoo na sisi tulikuwa tukikaa mtaa wa Agrey hapo hapo kariakoo.

Hakika Said alikuwa mtu wa watu sana na mcheshi sana, mkarimu sana na alipenda sana kusaidia wenzake pindi wanapopata taabu katika masomo lakin kubwa alikuwa mchezaji wetu mzuri sana wa shule katika timu ya football ya Gerezani primary.

Mimi nitamkumbuka sana marhum Said Ali Masimango kama mwalimu wangu darasani wa hisabu, kwani mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa hawapendi kabisa somo la hisabu lakin nilikuwa mzuri sana katika masomo mengine yote. Marhum Masimango pamoja na kuwa mimi ndie niliekuwa mshindani wake pekee darasani ,ambaye tulikuwa tunanyang’anyana namba moja ,lakin mara zote alikuwa akinipita somo la hisabu pekee. Na wanafunzi wa Gerezani tulizowea kumwita Computer kwa umahiri wake katika somo la hisabu.

Kwa waliosoma gerezani Primary tutazidi kumkumbuka kama mchezaji wetu mahiri wa soka wa timu ya shule lakin kubwa kama kiranja mwaminifu na mtiifu na kiongozi shupavu sana .Na tulibahatika sote kufaulu darasa la saba mwaka 1980 na mimi kwenda jangwani Secondary kwa mama Tegisa (Head mistress wakti huo)na Masimango alichaguliwa kujiunga na Sekondari ya Forodhani iliyokuwa ikiongozwa na mama Kamsini (Head mistress wakti huo) iliyopo Posta karibu na bandarini pale Dar e s salaam.

Pamoja na kusoma Forodhani na mimi jangwani lakin Marhum Masimango tulikuwa tukishirikiana sana katika masomo . Na nafikiri hata wale waliosomea Forodhani mwaka 1981 mpaka 1984 watamkumbuka sana Masimango kama mchezaji na alikuwa captain wa shule hiyo wa timu ya football lakin pia alikuwa yupo vizuri sana kichwani mpaka kufikia kufanya vizuri sana form four na kuchaguliwa kujiunga na masoma ya high school huko Tanga school.

Mimi nitamkumbuka zaidi pale tulipomaliza form Four nilipoamua kuolewa . Yeye ndie miongoni mwa watu wachache walionishauri niachane na kuolewa bali niendelee na masomo ya high school kwani nilipata daraja la kwanza katika mtihani wangu wa form four na kuchaguliwa kujiunga KLF Zanaki Secondary. Pamoja na ushauri wake huo mimi niliamua kuolewa ili ujiepusha na vishawishi vya Dunia ambapo kwa wakti ule vilianza kuninyemelea lakin mume wangu Dr Hamza wakti huo alikuwa UDSM mwaka wa mwisho aliniruhusu niendelee na masomo yangu ya high school Zanaki.

Ninachomkumbuka zaidi ni kuwa ni yeye pekee nje ya familia yangu aliweza kuhudhuria katika harusi yangu kwani tulifanya harusi ya ndani. Na aliweza kunifichia siri yangu hiyo kwa kipindi chote mpaka tulipoweka hadharani wenyewe kwa kufanya harusi kubwa nilipomaliza form six.

Nakumbuka tulipomaliza form six yeye alikwenda JKT na mimi nilibaki kwa mume wangu na hatimaye kufanikiwa kupata mtoto wangu wa kwanza wakti wao wanamaliza JKT. Nakumbuka alinibembeleza zaidi na zaidi niendelee na masomo ya Chuo kikuu name na mume wangu tuliupokea ushauri wake name nikajiunga na Chuo kikuu cha makerere kitivo cha Sheria wakti yeye akiwa amekwenda Uturuki kusomea Shahada yake ya Uhandisi.

Nitakumbuka sana kuwa kule Uturuki alipata matatizo na kuamua kurudi Tanzania na kufundisha kidogo shule ya Sekondari Al haramain na kisha kwenda India (Hydrabad ) kusomea shahada yake ya BSC Computer na baadae kwenda Burawayo kusomea shahada Msc Computer na kurudi Dar na kujiunga na Swiss Port kama Manager Computer.

Tumekuwa karibu sana na familia yangu kwa kipindi chote cha maisha yake hata watoto wangu walimpenda sana walipokuwa wakija Tanzania, kwani muda wote alizungumzia maendeleo tu na mikakati mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi lakin pia alisisitiza sana vijana wasome.

Kama familia yangu watamkumbuka sana mara alipomshauri mtoto wangu Haitham ajiunge na Shahada ya Computer na kumtaka a specialize katika GIS ambayo alifanya hivyo na sasa ni Mtaalamu wa GIS na anasomesha Ontario University iliyopo Canada.
Mpaka kumkuta umauti wake Masimango alikuwa Mkurugenzi wa TEHAMA katika shirika la NSSF Tanzania.

Ninakumbuka siku nne kabla kifo chake tuliongea nae katika simu kwa kipindi kirefu sana lakin kubwa tulilojadili ni kumtaka yeye na familia yake waje watutembelee hapa Mascat ili tufanye nao Ziara kwenye mji wa Mecca na Madina.

Kwa kweli ulikuwa msiba mkubwa sana kwangu na familia yangu kijumla usioweza kuzungumzika wa classmate wangu, ndugu yetu,mwenzetu na kubwa zaidi ni mshauri wetu Said Ali Masimango.

Kuna mengi sana ya kumwelezea lakin kwa leo nimeamua kukomea hapo. Tunaamini kuwa kila kilichozaliwa basi lazima kionje mauti. Nasi hatuna la ziada zaidi ya kumuombea Mola amlaze pahala pema peponi na kuzidi kumlipa kwa amali zake alizotenda hapa Duniani wakti wa uhai wake ikiwemo zile swadakat Jaaliya.

Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.

Nasriayah Saleh Al Nahdi
Muscat Oman
Rip masimango, naomba kuuliza hisabu=hesabu?
 
Mbona Kariakoo ndio chimbuko la kila kitu hata Uhuru wa Tanganyika vuguvugu lake lilianzia hapo. We soma kitabu cha Mohamed Said kinachoitwa HISTORIA YA TANGANYIKA ILIYOSAHAULIKA. Hapo alidadavua wazee hao walivyokuwa makini katika kutafuta ilmu na uhuru wa nchi yenu.

Ahsantum nakutakaia Eid Mubarak!

Asante sana kwa taarifa mkuu, wala sikuwa natambua haya yote, ubarikiwe sana uwe na afya njema, tuendelee kujuzana historia ya nchi yetu. Asante
 
kuna vingi umeongea lkn kuitwa computer miaka ya sabini sijui themanini naona kama hii ni chumvi,sababu hazikuwepo hata zilizokuwepo ni kwenye taasisi labda ni calcurator ntakuelewa.

ila niliwahi pita NSSF alikuwa anaonyesha namna ya kuprint document kwa kutumia simu ya mkononi bila kwenda kwenye computer.na kuhusu wema ni kweli hakupenda aone unakuwa mnyonge sababu ya matatizo na wengi walitumia weakness hii kumuomba pesa bila kumlipa/na zengine alikuwa anatoa tu kwa mapenzi yake mwenyewe.
 
Barubaru nyie ni vijana wa miaka ya sabini hadi themanini walioshi na kukaa katikati ya dar es salaam miaka hiyo najua kuna matukio mengi sana yalitokea miaka hiyo na mengi ni ya kutuelimisha naomba kwa mtirirko huu wewe au mkeo mtuletee mambo haya ambayo wengi wetu hatuyafahamu

Jamaa huyu alioa mtoto wa shule na kumuweka ndani; alivunja sheria na angeweza kwenda Lupango!! R.I.P masimango ulimtunzia siri Barubaru!!!
 
Back
Top Bottom