TANZIA Buriani Roziana, MOI itakukumbuka daima

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
114
Reaction score
200
Watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameungana na familia, ndugu na jamaa katika kumuaga aliyekuwa mtumishi wa taasisi hiyo, Bi. Roziana Philipo Mnzava, aliyefariki usiku wa Septemba 06, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

IMG-20260908-WA0042.jpg
Akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga marehemu leo Septemba 08, 2026 katika jengo la kusubiria huduma MOI, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, ameiomba familia ya marehemu kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hicho kigumu, akisema watumishi wa MOI nao wamepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwenzao.

IMG-20260908-WA0041.jpg
“Tunawaomba familia muwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia... Sisi kama MOI tumepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mtumishi mwenzetu. Pengo la Bi. Roziana litakuwa ni gumu sana kuliziba, lakini tutaendelea kumuombea na kumuenzi kwa mema aliyotuachia,” amesema Dkt. Mpoki.

Dkt. Mpoki ameongeza kuwa kuondoka kwa Bi. Roziana kunapaswa kuwa fundisho kwa watumishi waliobaki kuendelea kufuata nyayo zake kwa kufanya mema, kushirikiana na kutambua mchango wa wenzao wakiwa hai, ikiwemo kupongezana na kuthaminiana.

“Watumishi tuliobaki tunapaswa kufuata nyayo zake kwa kuchagiza na na kuyaishi yaliyo mema. Pia tujifunze kupeana pongezi na kuthaminiana tukiwa hai, kwa sababu hatujui nani atatangulia. Pengo lake litakuwa ni gumu sana kuliziba, lakini MOI itaendelea kumuombea na kumuenzi,” ameongeza.

IMG-20260908-WA0040.jpg
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mifupa MOI, Dkt. Anthony Assey, amemtaja marehemu Roziana Philipo Mnzava kuwa alikuwa mtumishi mwenye bidii na kujituma katika kutekeleza majukumu yake, akisema hata afya yake ilipoanza kuzorota aliendelea kufanya kazi kwa kujituma.

“Roziana alikuwa mtumishi mwenye bidii sana na aliyekuwa akijituma katika kazi zake. Hata afya yake ilipoanza kuzorota, aliendelea kufanya kazi kwa moyo na kujituma. Huo ni mfano mzuri wa kujitolea na upendo kwa kazi ambao tutaendelea kuukumbuka,” amesema Dkt. Anthony

Marehemu Roziana Philipo Mnzava anakumbukwa na watumishi wenzake kwa mchango wake katika taasisi hiyo, huku MOI ikiahidi kuendelea kuhifadhi kumbukumbu ya maisha yake, kazi na mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

IMG-20260908-WA0037.jpg
IMG-20260908-WA0039.jpg
IMG-20260908-WA0043.jpg
IMG-20260908-WA0038.jpg
 
Poleni sana, ila mmesabisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwq na ndugu zao kwa kufanyiq shughuli happ na wauguxi kukosekqna wodini tangu saa 6 mpaka saa 9 na nusu.
 
Back
Top Bottom