Bungeni: Ngonjera yaendelea! Wabunge waendeleza mipasho dhidi ya CHADEMA (Nov 17)

Status
Not open for further replies.
Hakuna hata mbunge mmoja wa Ccm ambae ameamka na kuzungumzia muswada bila kuongolea Chadema! Wamehamisha mjadala kutoka kwenye mkondo wake wa asili na kuituhumu Chadema kwa kila neno.
Hii ina maanisha nini kwa wabunge hawa wachangiaji?
 
Tatizo ni kuto kuwa na hoja/mawazo toka kwa wananchi Ndiyo maana hawana hoja ya msingi isipokua kuijadili CDM kwani hawana cha kuongea Spika naye haoni kuwa la kudadili halipo

Haiwezekani toka juzi watu wanakijadili chama as if ndiyo hoja iliyopo mezani na spika kawa kimya kama hayupo vile 'kinacho nihuzunisha ni hela yangu watakayo gawana pasipo kufanya kazi niliyo watuma "
 
Tanzania : A nation full of bogus politicians/leaders:
Hivi ndivyo ilivyo nchi yetu kwa sasa. Ukiangalia yanayoendelea Bungeni utajua ninachokisema. Hakuna tena wanasiasa makini nchini hasa baada ya kujaza Idadi ya wachumia TUMBO, SIFA na VYEO katika Bunge.
CHADEMA wamesusia mjadala kwa sababu wanazoamini ni sahihi na muhimu kwa maoni yao. Baadhi ya watanzania wameelewa kinacholalamikiwa na baadhi wanaona CDM wanapenda fujo. Binafsi siumizwi kichwa na hilo maana mwenye akili anaujua ukweli na ataweza kutenga uongo/pumba.
Jambo ambalo limeanza kunipa shaka ni uwezo wa viongozi/wawakilishi wetu katika kujua kipi kisemwe wapi na kwa wakati upi na lipi muhimu kwa wakati gani na lipi si muhimu kwa wakati fulani. Je kuna sababu ya kila mbunge anayesimama kuchangia kulaumu wabunge na CDM kwa kususia mjadala na hicho kinachoitwa kuidhalilisha Zanzibar wakati kuna muswada mezani unaohitaji kuchangiwa mawazo na hatimaye kupitishwa?
Naomba kwa pamoja tutafakari fikra hizi katika mitazamo kadhaa ili tuone kama kuna hekima sana kwa wabunge wa CCM, CUF na wengine kujadili vitendo vya CDM kama kipaumbele katika michango yao wakati issue ni mswada.
  1. Je ni kweli kwamba katika maelezo yote ya Mh. Lissu hakuna lolote muhimu isipokuwa pumba tu kiasi cha watu kutokuwa na lolote la kuishauri serikali kutazama upya mtazamo wake katika baadhi ya vifungu? Je itakuwaje kama kuna mapendekezo mengine mazuri kwa watu wote lakini yamefunikwa na hasira za baadhi ya wabunge hao wanaoona CDM inatumiwa?
  2. Je wabunge wetu wapendwa, waliozoea mbinu chafu/njama za chinichini katika kutafuta madaraka wana uhakika gani kwamba CDM hawatumii udhaifu wao wa kutochambua vifungu kwa umakini unaostahili kuwatoa katika hoja ya msingi ili baadaye waonekane wamepitisha madudu na wao, CDM wapate nafasi ya kuwashtaki kwa wananchi kama walivyofanya kwenye ufisadi na kuwapora majimbo kibao na kura nyingi za urais?
  3. Kama CCM wamekuwa wanatumia mbinu chafu kushinda wakiwa watawala nini kinawazuia CDM kutumia kutotafakari kwa majority ya wabunge wetu kuwaumiza kwa mbinu za kuwa-misslead ili wajadili kauli za Lissu wakati Mswada unapita pasipo kujadiliwa kwa umakini unaostahili?
  4. Mh. Hamad Rashid ametafakari kwa makini na kujua CUF yake imefikaje serikalini huko Zanzibar kama si kutumia nguvu yao ya umma na kususia mambo mengi katika SMZ mpaka kilipoeleweka?
  5. Na wenzetu CHADEMA; Kama swala lenyewe ni wazi litapita Bungeni kwa kutumia wingi wa viti vya CCM na vyama rafiki wao, kwa nini msibakie Bungeni mkatoa michango yenu ambayo baadhi yetu tunaikubali zaidi? Ili ijulikane Mnyika alipendekeza nini na kikatolewa nje n.k.?
Hali hii imenishawishi kuamini kwamba tunao wanasiasa wengi Ma-Bogus wanaoenda kwa mkumbo tu na hawatumii muda wao kusoma, kusikiliza na kutafakari mambo kabla ya kuchangia. Huwezi kuushutumu ubalozi wa kigeni kwa madai ya kuingilia mambo ya ndani wakati serikali yako inatengeneza sera kwa kuwasilikilza mabalozi hao hao zaidi hata ya wanataaluma wazalendo. Hapa Mh. Ndasa ama amepotoshwa au hajui anachokisema maana ukifuatilila maamuzi mengi ya serikali za CCM yamekuwa yanaamini watu hao hao wa kutoka nje kuliko wazalendo na ndiyo sababu tunazidi kuvurugikiwa kiuchumi.
Naomba niishie hapa kwanza. Natarajia kuwa open to more discussion.
 
Sikio la kufa halisikii dawa. .........watasingizia mpaka mawe mwaka huu...... mmoja jana BBC alikuwa anasema kila walipopeleka mjadala wa katiba walikuta CDM wameandaa vijana wa kuwazomea wakiongea na kuchana au kufanya fujo hivyo wakaacha.

Mkuu huyo gamba ni mbunge wangu nilijisikia aibu sana maneno ya uwongo aliyokuwa anaongea eti wabunge wa CCM walipita katika majimbo yao kuuliza maoni ya wapiga kura!! Alichanganya mpaka ikawa aibu,mwisho hata mtangazaji wa BBC alimstukia akampuuza!
 
na wabunge wengine wa CCM wanafuata kuchangia wanasema upupu gani?.....updates please wadau...!
 
kama ni mtaji basi ni chama cha demokrasia na maandamano ndicho kinachofaidika ama kitafaidika mana maandamano yataongezeka.
 
Hivi ni kweli kwamba huyu jamaa ni mtoto wa Job Lusinde?? Maana haiingii akilini mwasiasa maarufu kama huyo awe na mtoto wa Dizaini hii!!
 
Wadau hiyo Ndiyo cv Ya Lusinde Mbunge wa Mtera


GENERAL

Salutation
Honourable
Member picture
1694.jpg

First Name:
Livingstone
Middle Name:
Joseph
Last Name:
Lusinde
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Mtera
Political Party:
CCM
Office Location:
Box 50, Dodoma
Office Phone:
+255 755 453327/+255 785 679927
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
Mbigili Primary School
Primary Education
1980
1987
PRIMARY
CCM College Ihemi
Certificate
2007
2008
CERTIFICATE
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type
Certification No.
Issued
Expires
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From Date
To Date
The Parliament of Tanzania
Member - Mtera Constituency
2010
2015
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location
Position
From
To
Chama Cha Mapinduzi, CCM
Secretary - Tarime District
2006
2010
Chama Cha Mapinduzi, CCM
Assistant Secretary/Accountant
2006
2007
CHADEMA
Member - National Executive Board
1995
Civic United Front, CUF
Secretary - Kawe Constituency
1992
1995
Chama Cha Mapinduzi, CCM
Secretary
 
Astaghfilullah,
huyu ana'waza nini?anaesema hvo ni mwanaume?jaman ni mbunge wa wapi?
..Jamaa kaanza kuchangia kwa mipasho kama kawaida.Anasema anaomba tumuongezee muda JK kwa miaka 2 baada ya 2015 ili aweke mambo sawa ya katiba na baadae tufanye uchaguzi 2017..na akasema mwanaume mwenye sharubu ni JK pekee na si vinginevyo....
 
Tangu bunge limeanza kujadili mswada wa katiba mpya wabunge wamekuwa wakisema ITV wanachafua amani kwa kuruhusu majadiliano ya katiba..na leo mbunge wa Mafia karudia hilo na kumsema Wilfred Masako kuwa vipindi vyake ukipiga simu kuchangia uwa haipatikani na uwa anaruhusu wapingaji wa serikali ndio wapate line,utadhani Masako ndio Vodacom au Tigo au TTCL ..na ameenda mbali kusifia TBC kuwa wanafanya vyema....

Je,hii ni kweli na kwanini hawa wabunge wanaboa namna hii..
Mabaki ya misngi ya chama kimoja yamewalemea kichwani hawa wabunge wa CCM. Wanapinga Itv kwa kuwa ni tv station inayorusha vipindi vinavyowasilisha fikra na dhamira huru kwa watanzania juu ya mswada huu.
Kupunguza mamlaka aliyozidishiwa raisi ndio suluhisho tosha dhidi ya matatizo ya watanzania.
Taifa kwanza, chama baadae.
 
Hawa ccm wamechanganyikiwa kwa maana kama wananchi watakomaa muungano uvunjike, maana yake hakutakuwa na chama cha mapinduzi sasa wanatetea matumbo yao na ya chama chao ambacho 2015 kitakuwa ndio chama cha upinzani kichanga, wanang'ang'ania rais aendelee kuwa na madaraka makubwa kwa maslahi ya ccm.
 
Hilo lipo wazi ndugu kweli tindu lissu ana akili sana nampa hongera zake ila juzi kuna mbunge mmoja wa cuf alitoa hilo angalizo kwamba wabunge tumetolewa nje ya hoja na akawaomba wenzake wasiijadili chadema na tindu lissu ila cha ajabu baada ya kutamka maneno mawili nae akaanza kumshambulia tindu lissu na chadema....

Mimi ninachokiona huu mswada umekuwa na wachangiaji wengi kwasababu wabunge wengi wa ccm ni watu wa mipasho na hio ndo sehemu yenyewe ya mipasho na kama chadema wangeukubali ungeshaangaa wachangiaji wengi wangekuwa ni wa upinzani na wachache wa ccm coz ccm hawana cha kuongea kwenye huo mswada
 
Me naipenda hii Vita sasa maana imefika kutamu. Wao wameiponda ITV na jana ITV wameanza kujibu mabomu taratibu. Taarifa ya habari mtangazaji alisema wabunge wanatumia muda mwingi kuijadili CHADEMA


Usitafute ugomvi wa mawe na wewe unaishi nyumba ya kioo.


From Tundu Lissu to CHADEMA n now to ITV.
Who is next kwenye mashairi yao ya Taarab?
 
..Jamaa kaanza kuchangia kwa mipasho kama kawaida.Anasema anaomba tumuongezee muda JK kwa miaka 2 baada ya 2015 ili aweke mambo sawa ya katiba na baadae tufanye uchaguzi 2017..na akasema mwanaume mwenye sharubu ni JK pekee na si vinginevyo....

Stupid! Would've slapped the hell outta him if i was close
 
kwa kweli siasa za wakati huu ni changamoto kubwa sana kwa ccm..................... wiki mbili nzima ziliyopita, aliyekuwa akijadiliwa ni lema wa cdm arusha na chama chake, .........................wiki hii yote anayejadiliwa ni lisu na chama chake, wameufunika mpaka mjadala wenyewew wa katiba uliokusudiwa........................ nimesikia simachawene kajikuta "anabembeleza" eti "...................wananchi, tusikilizeni na sisi basi.............."................

hahahaa, kazi wanayo wanaccm.......................
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom