Bungeni: Ngonjera yaendelea! Wabunge waendeleza mipasho dhidi ya CHADEMA (Nov 17)

Status
Not open for further replies.

Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
180
"Wananchi tunaomba mtusikilize na sisi" - George Simbachawene, alipokuwa akichangia muswada wa katiba mpya. Natafakari ina maana wananchi hawawasikilizi?mbona wameshinda na wapo bungeni? Mbona anazungumza kiujumla na kama hao wa kijumla hawasikilizwi mbona wao wapo wengi bungeni? Wamejipeleka au wamepelekwa?

Nikitafakari kwa makini kauli hii napata shaka na ushindi wao, napata shaka kwanini wanataka kuonewa huruma na sio kuweka hoja na ukweli mbele?kimsingi wao wapo wengi bungeni, kimsingi wao ndio wanastahili kusikilizwa zaidi sasa ukiona wananchi hawataki kuwasiliza uje wamejiepeleka na hawakupelekwa na wananchi, walienda kwa ubabe, nguvu ya mtutu na advantage ya uelewa mdodo wa wananchi sasa wameamka chupi zinawabana

Hii inathibitisha ule usemi wa kiiengereza kuwa "YOU CAN FOOL PEOPLE FOR SOMETIME BUT YOU CANNOT FOOL THEM ALWAYS"
 
Sikio la kufa halisikii dawa. .........watasingizia mpaka mawe mwaka huu...... mmoja jana BBC alikuwa anasema kila walipopeleka mjadala wa katiba walikuta CDM wameandaa vijana wa kuwazomea wakiongea na kuchana au kufanya fujo hivyo wakaacha.
 
Watashika uchawi kila mtu tatizo hawajui wachawi ni wenyewe kwa kujali matumbo yao na ya watoto wao.wana wa tanzania hawana dhamani yoyote kwao.
 
Huyu mbunge wa Mafia nae katoa pumba tu! Yaani kutokupata line kwake kila alipokuwa akipiga simu ITV basi ITV wamekuwa na upendeleo na kwamba wanapanga watu wa kuongea, nadhani huu ni uzushi usio kifani! Natamani ITV waombe uthibitisho kutoka kwake kama wamekuwa wana-upendeleo wowote ule kwa mtu au chama chochote kile, vinginevyo huyu ni wa kumshtaki kabisa mahakamani kwa kuharibu reputation nzuri ya kituo hicho! Anaisifia TBC1 kwamba imekuwa fair ktk mchakato huu kitu ambacho si kweli kabisa! Huwezi sema mchanganyiko wa CCM (A) na CCM (B)-CUF ati ni mchanganyiko wa upinzani na chama tawala. Huu nao ni upuuzi mtupu!
 
..Jamaa kaanza kuchangia kwa mipasho kama kawaida.Anasema anaomba tumuongezee muda JK kwa miaka 2 baada ya 2015 ili aweke mambo sawa ya katiba na baadae tufanye uchaguzi 2017..

Na akasema mwanaume mwenye sharubu ni JK pekee na si vinginevyo....
 
anaongea upupu mtupu, yahakuna hoja hapo.zaidi ya kuattack cdm.hakuna hata moja linalohusu muswada wenyewe.
 
huyu jamaa badala ya kuongelea katiba ye anawatukana cdm.lusinde inaoneka lisu anakukosesha usingizi sana,pole sana roho inakuuma ccm inavyokufa hahahahahahahahaha
 
anasema kwamba kuna wengine wameanzisha mitandao ya kuwatukana
 
shetani alikuwa akigawa ukilaza kidogo kidogo killa kwa mwanadamu ILA ALIPOFIKA KWA LUSINDE kapu likamponyoka ukilaza wooooote uliobaki ukamwingia LUSINDE.

LUSINDE ni kilaza sjawai asiyeelezeka

huyu ndiyo vuvuzela lao.nafikiri kwenye kikao chao cha chama kuwa wapange mavuvuzela ili wapige kelele bunge.
 
Ninashangazwa sana uendeshaji wa bunge letu jamani, hoja iliyopo ni mjadala wa uundwaji wa katiba, kinachoshangaza ni hawa wabunge wa ccm wao ni kujadili watu wa chadema tu, mara tundu lisu, mara mke wa Slaa, mara mboye.. Duu, na spika kakalia kiti.. Eti wanasema Lisu,Sendeka, Mboye ,Slaa wameweka ndugu zao tu bungeni, wana ukoo., Eti CCm haijaweka ndugu... Dah, upuuzi mtupuuu
 
Paza sauti, lia hadi pandez zote za nchi....wananchi ndio watawadharau zaidi.....sasa wanajua kuwa wananchi wana power....wakati wanapobanwa!!!Vinginevyo, wananchi ni kwa kutumia tu kama ladder ya kupandia and then to be thrown and trampled upon...Not at all, wananchi wameamka na bado....
 
Lusinde anadai kuwa uchaguzi uhairishwe na uwe 2015 eti sababu raisi ana majuku mengi yaliyo ongezeka
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom