Bungeni: Ngonjera yaendelea! Wabunge waendeleza mipasho dhidi ya CHADEMA (Nov 17)

Status
Not open for further replies.
BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.bAkichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011, Assumpter Mshama (Nkenge - CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.b"Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi," alihoji.bAliongeza: "Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

"CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni Kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje."bKwa upande wake, Livingstone Lusinde (Mtera - CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.
Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.
"Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme," alisema. Ingawa Lusinde hakuwataka kwa majina ndugu hao wa viongozi wa juu wa CHADEMA, lakini inafahamika kwamba, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, mtoto wake ni Lucy Owenya na mkwewe ni Grace Kiwelu ambao ni wabunge wa viti maalumu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa mkewe Rose Kamili naye ni mbunge wa viti maalumu, kama kwamba haitoshi Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu naye ana dada yake, Christina Mughwai ambaye ni mbunge wa viti maalumu.
Kigogo mwingine wa CHADEMA, ambaye ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar, naye ana mtoto wa dada yake bungeni kupitia nafasi hizo. Mjomba wake kigogo huyo ni Raya Ibrahim Khamis.
Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo, kwani wa kuzuia fujo wapo.

"Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu," alisema.
Lusinde alihoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.
Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.
CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.
Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.
Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo ambayo yaliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano, na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.
John Lwanji (Manyoni Magharibi - CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno 'abrakadabra'.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu - CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.
"Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kana kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona," alisema.
Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

"Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana," alisema.
Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.
Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.
 
BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.bAkichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011, Assumpter Mshama (Nkenge - CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.b"Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi," alihoji.bAliongeza: "Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.
.

ni ukweli mtupu huo,,,,, nafasi ndani ya CDM wanapeana kidini... kikabila... kiundugu .. na kiuchumba .... wachache kina zito wamewekwa pale kuziba ziba huo uchafu ...

Sijaona muswada uliochangiwa kwa umakini kama huu. "MUSWADA WA MIPASHO KWA CHADEMA". TOT imepewa uwakilishi wa kudumu bungeni.
 
yan ww ndo upupu kabsa..mbona hamsemi magambaz wanaeka wake zao wa nje..catherine,vick ,batilda..vp yule mkuu wa wilaya ya manyoni
 
Sijaona muswada uliochangiwa kwa umakini kama huu. "MUSWADA WA MIPASHO KWA CHADEMA". TOT imepewa uwakilishi wa kudumu bungeni.

Mkuu mie nimeleta hapa maandiko haya tuyachambue hakika CCM imepoteza mwelekeo na sina hakika kama majimboni wataeleweka wakisha rudi watanzania wamesha amka wacha tuone
 
Fuatilia ujue chadema viti maalumu wanapatikanaje,mwaka jana kumbuka walikodi consultant kutoka UDSM watu wakatable CV zao na vigezo vingine viliangaliwa ikiwa ni pamoja na uzoefu wa siasa,ujasiri wa kugombea majimboni na mchango katika harakati za kukiimarisha chama.Huko CDM hatuangalii Taarabu na kwaya kama mnavyofanya,lakini pia ni muhimu ufuatilie zaidi.Na mwisho hili ni gazeti sijaona ukiweka hoja,
 
Zamamako anapewa na nani?

minafikiri ni ufinyu wa fikra na maono kimtazamo hasa hawa wabunge wa ssm na upendeleo wao toka kwa rais yani mme wao!NIANZE KWA KUSEMA HIVI KILA CHAMA KINA MWANZO NA CHIMBUKO LAKE KAMA UNAVYOONA CONSERVATIVE, LABOUR HUKO UINGEREZA NA DEMOCRATIC AU REPUBLICAN HUKO USA, KW HAPA TANZANIA MTEI NDO MWANZILISHI WACDM+BOB MAKANI BAADAE AKAACHIWA MBOWE, HAPO UNAWEZA KUPATA MWANGA CHAMA KIMEANZA LINI, NI CHAMA AMBACHO KIMEPATA UMAARUFU ZAIDI NDANI YA MIAKA MIWILI AU MITATU ILIYOPITA BAADA YA KUONEKA KUWA CHAMA CHA HOJA NA SI KELELE KAMA CCM, KUTEUA NAFASI YOYOTE YA UONGOZI SIO SUALA LA MCHEZO KATIKA CHAMA, IFAHAMIKE KWAMBA, CHADEMA KUPATA WANACHAMA WA KUDUMU IMEANZA KUWAPA MIAKA YA 2009 WALIO WENGI HIVO WALE WAASISI SIO WENGI KAMA MNAVYODHANI, UKIMWONGELEA NDESAMBURO NA RUSSI OWENYA LAZIMA UJIULIZE JE WAMEJIUNGA NA CHADEMA TANGU LINI?ZITTO KABWE SIO WA UKANDA HUO ILA ANA JUMLA YA MIAKA 16 NDANI YA CHADEMA, MWONE MNYIKA NAMBOWE, HATA HAWA WALIOCHAGULIWA VITI MAALUM, NIWATU WENYE CHUMVI NYINGI NDANI YA CHAMA NA HAO TAYARI KAMA NI PROBATION NADHANI WATAKUWA WAMEKUWACONFIRMED BAADA YA KUWA CHINI YA CHUNGUZI KWA KIPINDI KIREFU SASA WAMEANMINIWA NA KUPEWA UONGOZI,

SASA WENZANGU MNATAKA WATU WALIOJOIN MWAKA MMOJA AU MIEZI SITTA WAPEWE UONGOZI?SI UTARATIBU HATA KIDOGO, LAZIMA UTARATIBU UWEPO WA KUCHUNGUZANA KWANZA TUONE UWEZO WAKO NA TUJIHAKIKISHIE KAMA HUJATUMWA KUIBA SIRI ZA CHAMA AU KUVURUGA CHAMA, NINA IMANI KADRI MUDA UNAVYOKWENDA TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA NDANI YA CHAMA KWANI KINAKUWA NA KUPATA WANACHAMA WENGI WENYE UWEZO, CHAMA CHETU NI CHAMAM CHA HOJA SIO KUPEANA NAFASI KUTOKANA NA KUMTAFUTIA WANAWAKE MKUBWA FULANI AU KUIBA KURA KITUO FULANI NDIPO UPEWE UONGOZI NDANI YA NCHI! NANI ASIYEJUA HAWA GHASIA NI NDUGU NA MAMA SALMA KIKWETE, SHUKURU KAWAMBWA NI MPWA WA KE, KABAKA, MEMBE RAFIKI YAKE WA KUTUPWA, NANI ASIYEJUA MASHA ALIPEWA UWAZIRI KWA SABABU GANI! HUYU ASUMPTA UWEZO WAKE NI MDOGO SANA NDO MAANA BADALA YA KUJADILI HOJA ANAJADILI WATU NA AJUE MWAKANI NACHUKUA FOMU KUGOMBEA NKENGE, HAJAFANYA KITU HUKU HATA DARAJA MOJA LIMEMSHINDA, KAZI KUHONGA VITENGE NA NDO MAANA HATA SHULE YAKE YA MBEZI BEACH IMEMSHINDA KUENDESHA, SASA JIMBO KWELI ATALIWEZA, NI MDAKU NA MTU WA KUKURUPKA, ALIVUA CHUPI AKAPEWA UBUNGE SO SISHANGAI SANA MTU MWENYE MTAZAMO KAMA WAKE!
 
Tatizo la CCM ni uelewa mdogo mno. Urais wa kifalme katika context ya utawala ni pale mtu mmoja anapohodhi mamlaka karibu kwa kila jambo na hakuna wa kumuuliza wala hakuna sheria ya kumzuia. Kwa mfano Tanzania kama ilivyo nchi zenye wafalme (Swaziland) Rais wa Tanzania ndiye kila kitu, anateua baraza la mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wao, wakurugenzi wa wilaya (DED), wakuu wa mashirika (hadi gazeti la Daily News amini usiamini), anaunda tume ya uchaguzi, anateua majaji, mwanasheria mkuu, mwendesha mashitaka, mkuu wa polisi, mkuu wa usalama wa Taifa - list ni ndefu mnooo. Na katika uteuzi huu hakuna mtu wa kumzuia. Anagua kwa kadri 'inavyompendeza' yeye hakuna cha interview kama ambavyo tunaona sasa huko Kenya.

Na kama ambavyo tumeshughudia hata pale watu hawa wanapofanya vibaya raia hawana nguvu ya kuwaondoa kisheria maana mwenye mamlaka ni mtu mmoja tu - rais. Ni jambo la kustusha tena sana kusema kuwa Tanzania tuna utawala wa demokrasia, demokrasia gani hiyo inayomfanya mtu mmoja awe juu ya sheria kama ambavyo rais yupo? Katiba tuliyonayo sasa ni ya urais wa kifalme kama sio kidikteta, wala hili halina ubishi. Kilichofanya watu wakawa 'watulivu' huko nyuma ni kwa sababu kwa kipindi kirefu tangu tupate uhuru tulikuwa na mtu ambaye walau alikuwa na ana maslahi ya raia (Mwl Nyerere). Pale unapokuwa na uongozi dhaifu, ulijaa wezi, wabinafsi na waongo kama sasa basi ndipo unapoona madudu ya katiba yetu. Na hili ndilo lilitokea.

Sasa CCM wanapoambiwa kuwa tuna utawala wa kifalme kwa uelewa wao mdogo wanafikiri watu wanaongelea mahusiano ya kifamalia! Huu ni upofu na ni aibu kwa watanzania wooote (sio ccm tu) kwamba tuna viongozi wasioelewa vitu so basic kama dhana ya utawala wa kiflame. It is an embarassment of monumental proportion na kwa kiongozi yoyote anayeonekana kutafsiri dhana ya urais wa kifalme kwa maelezo ya kifamailia ni vizuri watu wamgope kama ukoma! Gazeti la Uhuru nalo kwa sababu akili zao wamegandisha kwenye freezer na utashi wao wametupa baharini wanakubali kujidhalilisha kwa ku-copy & paste nini Wassira &co wanawapa? Sijui waandhishi hawa wakirudi nyumbani jioni wanawaeleza nini watoto wao? CCM kweli janga la kitaifa!
 
ni ukweli mtupu huo,,,,, nafasi ndani ya cdm wanapeana kidini... Kikabila... Kiundugu .. Na kiuchumba .... Wachache kina zito wamewekwa pale kuziba ziba huo uchafu ...

ni kweli siku tukiwageukia watatutambua
 
BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.bAkichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011, Assumpter Mshama (Nkenge - CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.b"Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi," alihoji.bAliongeza: "Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

"CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni Kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje."bKwa upande wake, Livingstone Lusinde (Mtera - CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.
Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.
"Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme," alisema. Ingawa Lusinde hakuwataka kwa majina ndugu hao wa viongozi wa juu wa CHADEMA, lakini inafahamika kwamba, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, mtoto wake ni Lucy Owenya na mkwewe ni Grace Kiwelu ambao ni wabunge wa viti maalumu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa mkewe Rose Kamili naye ni mbunge wa viti maalumu, kama kwamba haitoshi Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu naye ana dada yake, Christina Mughwai ambaye ni mbunge wa viti maalumu.
Kigogo mwingine wa CHADEMA, ambaye ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar, naye ana mtoto wa dada yake bungeni kupitia nafasi hizo. Mjomba wake kigogo huyo ni Raya Ibrahim Khamis.
Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo, kwani wa kuzuia fujo wapo.

"Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu," alisema.
Lusinde alihoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.
Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.
CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.
Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.
Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo ambayo yaliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano, na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.
John Lwanji (Manyoni Magharibi - CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno 'abrakadabra'.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu - CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.
"Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kana kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona," alisema.
Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

"Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana," alisema.
Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.
Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi aawangeshindwa kishujaa.
He elimu yao no sawa na za magamba? Wanastahili kuwepo halo walipo
 
Hii ni pumba kwasababu sio ndugu wote viongozi kwani wake na watoto wa mawaziri wa Tanzania mbona ni wa CCM na sio Chadema. Raisi wa Nchi Mke, Mtoto wote wako CCM na wana piga kampeni waziwazi!. Mtoto wa raisi ni kiongozi kwenye chama!!!! hii pumba
 
Ndio maana hata rais ambaye ndioye mwenyekiti wa ccm hajui kwa nini nchi ni masikini, wala hana uwezo wa kuifanya mvua inyeshe. Katika mweleko huo dhana ya urais wa kifalme utaeleweka kweli na hao magamba na ukizingatia wanafikiria kwa masaburi
 
chadema walikosa watu?kama ni kweli basi sio fresh'sikubaliani nao kutenda kitendo kama hicho
 
we ni mchovu na ni mvivu wa kufikiria hebu rudi nyuma na uone jinsi ambavyo CHADEMA walivyotumia vigezo kupata wabunge wa viti maalam sio unabwabwaja tu.
 
shetani alikuwa akigawa ukilaza kidogo kidogo killa kwa mwanadamu ILA ALIPOFIKA KWA LUSINDE kapu likamponyoka ukilaza wooooote uliobaki ukamwingia LUSINDE.

LUSINDE ni kilaza sjawai asiyeelezeka

Na huyo Lusinde, ndiyo mmojawapo wa 'Thinktank' za CCM!!! what a hell..............!!!!!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom