Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,554
- 113,737
Wanabodi,
Hatimaye ile sintofahamu kuhusu kuwasilishwa kwa muswada huu wa marekebisho madogo ya ule ile sheria ya Tume ya kukusanya maoni ya katiba, itamalizika rasmi leo asubuhi hii kwa muswada huo kuwasilishwa rasmi asubuhi hii katika kikao cha bunge.
Hata hivyo mjadala wa marekebisho hayo haitaanza kujadiliwa ili kutoa fursa kwa wabunge kujadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari ambayo itawasilishwa leo na M/Kiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Magret Sitta.
Akitoa uthibitisho huo, Waziri wa Mahusiano ya Umma, Mhe. Stephen Wasira, ameiambia TBC leo asubuhi kuwa marekebisho hayo ni ya serikali na sio ya chama chochote!.
Nawasilisha.
Pasco.
Update:
Muswada umewasilishwa, maoni ya kamati ya bunge ya sheria na katiba pia yamewasilishwa.
Maoni ya kambi ya upinzani ndiyo yanawasilishwa, majadiliano yatafuatia.
NB, hoja yangu ya kuanza kwa hoja ya dharura ya kujadili mgomo wa madaktari, nimeshaitolea ufafanuzi kwenye ile thread yake.