Tundu Lisu na Chadema wamfagilia kikwete bungeni, utadhani si hawa waliotoka nje wakidai hawamtambui... Hata hivyo ni ukomavu kisiasa, kumtambua Rais na nia yake njema ya kutaka nchi yetu ipate katiba nzuri kwa masilahi ya watanzania wote! Bravo Lisu, bravo Chadema kwa kuamua kula matapishi yenu... Mwendo mdundo
" Rais Kikwete ameonyesha uungwana na busara za hali ya juu sana, hakika ametoa muda wake mwingi kuhakikisha nchi yetu inapata katiba bora na safi kwa miaka ijayo, huu ni uzalendo na ukomavu mkubwa wa kiuongozi. Rais Kikwete anastahili pongezi"