BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

Hamad Rashid anahoji mkanganyiko wa kusamehe Kodi kwa makampuni ambayo yanataraji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa hazina ya mafuta.

Anahoji: "Inakuwaje kama wao walishapanga gharama zao zote za uendeshaji wa shughuli zao na wakajiridhisha kuwa inawezekana inakuwaje leo waje wafike hapa waombe msamaha wa kodi wakati tunafikiria kuondosha misamha hii ili kuongeza ukusanyaji wa mapato, tusifanye kosa hapa'' amaliza Hamad Rashid Mbunge wa Wawi - CUF
 
duh, siasa za bongo kunakucha sasa................... wala rushwa wanatajwa live mbele ya spika!!...................
 
pengine hii itasaidia kuwavua magamba yao halisi................wanajifanya kujivua magamba halafu wanabaki na sumu ileile................kikwete halipwi anapokagua miradi kweli?
 
Huyu sio Hamad Rashid ninayemfahamu.

Anaponda maandamano kwamba katika nchi zilizoendelea maandamano hufanywa usiku. Amesahau kuwa CUF waliandamana huko Tabora na Mbunge wao akakaa ndani wiki mbili.

Amesahau kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) Julius Mtatiro na Mwenyekiti wa Prof Lipumba walikuwa wanahimiza maandamano yaliyopangwa kuanza saa 4 asubuhi. Pole sana Hamad Rashid Mohamed nadhani safari yako ya kurudi uraiani imewadia
 
Ametamka hayo leo akichangia mpango wa maendeleo ya taifa.Kati ya hao ametaja mh.Zambi.
source tbc1-bungeni live jioni.
 
pengine hii itasaidia kuwavua magamba yao halisi................wanajifanya kujivua magamba halafu wanabaki na sumu ileile................kikwete halipwi anapokagua miradi kweli?
Ndio maana tunasema yote ni magamba tu. Hakuna tofauti na Edward Lowassa na Rostam Aziz
 
Huyu sio Hamad Rashid ninayemfahamu.

Anaponda maandamano kwamba katika nchi zilizoendelea maandamano hufanywa usiku. Amesahau kuwa CUF waliandamana huko Tabora na Mbunge wao akakaa ndani wiki mbili.

Amesahau kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) Julius Mtatiro na Mwenyekiti wa Prof Lipumba walikuwa wanahimiza maandamano yaliyopangwa kuanza saa 4 asubuhi. Pole sana Hamad Rashid Mohamed nadhani safari yako ya kurudi uraiani imewadia
Nchi gani hiyo maandamano yanafanywa usiku au na wewe hujamsikikia vizuri?
 
Mkuu unataka kusema hata Mwenyekiti Simbachawene hajamsikia vizuri, maana amerudia mwishoni. Hamad ametumia zaidi ya dakika tatu kuelezea namna maandamano yanavyofanyika katika nchi alizosema zinajua maagement of time, nipo makini Mkuu
 
Mbunge wa CHADEMA David Silinde Akitolea uvivu Chama Cha Mapinduzi, asema mpango wa Maendeleo wa 2011/12 - 2015/16 ni changa la macho hauwezekani kutekelezeka, asema inakuwaje wenzake hawasomi alama za Nyakati.

Kapigwa stop na Mwenzie kwa mwongozo kuwa kapotosha kuwa maelezo aliyoyatoa yanalenga kuupotosha Umaa, Duuhh Hii kali baadhi ya wabunge wanashabikia ati CCM

Apaza sauti upya na kudai haitaki taarifa hiyo kwa kuwa imelenga kujipatia ujiko kwa mbunge aliyempiga stop bila kufuatilia kwa umakini alichokisema.

Inafurahisha kuona kama wabunge hakuna kulemba bendera za vyama ni hoja tu.
 
Duhhh hapo ipo kazi
 
Mkuu unataka kusema hata Mwenyekiti Simbachawene hajamsikia vizuri, maana amerudia mwishoni. Hamad ametumia zaidi ya dakika tatu kuelezea namna maandamano yanavyofanyika katika nchi alizosema zinajua maagement of time, nipo makini Mkuu

Basi kama ni hivyo inathibitisha watu wengi tunatembea bararabarabi huku tukiwa ni magonjwa mbali mbali. Kama kasema hivyo basi inabidi atumie stahiki yake ya kutumia pesa za walipa kodi kwenda kuchekiwa afya ya ubongo wake india.
 
Alikuwa bado anatema moto kuhoji inakuwaje ndani ya miaka minne tukaweza kuleta maendeleo yaliyotushinda kwa miaka 50, katulizwa muda umekwisha ila sijui kama walizihesabu na zile wakati anapewa taarifa na mbunge mwenzie.

Kaibuka Nyambari Nyangwine sasa ngonja tumsikie
 
yani ndani ya nyumba ni mashamb ulizi ya ukweli mi natabiri kama wabunge wa sisiem wanaendekeza kushabikia tuu basi nadhani sasa kwa level ya kuambiana ukweli watashikana mashati
 
Back
Top Bottom