Bungeni: Mjadala wa dharura juu ya mgomo wa wauza mafuta

Mheshimiwa Zitto kasema, ikifika saa kumi na mbili leo jioni, kama hawajafungua vituo, basi jeshi liende likasimamie na lifanye kazi hiyo, wakati hao waliofunga vituo wanachukuliwa hatua za kunyang'anywa leseni zao. Kama na jeshi watashindwa, basi dalili za kutokea yaliyotokea London siku tatu hizi zilizopita ni wazi kwa Tanzania, hasahasa ktk miji yetu mikubwa. Hayo yote yanakuja kutokana na udhaifu wa baadhi ya watendaji Serikalini.
 
Issue hii ni sawa na uhaini, matajiri wakubwa wanne wanataka kuiweka nchi rehani, Wakurugunzi wa makampuni haya makubwa walitakiwa kupewa saa 24 wasiwepo nchini
 
Kwa mara ya kwanza naona bunge limesimama likiwa moja kumtetea common mwananchi bila kujali khaki, kijani au rangi nyingine!

CCM wameshagundua kuwa wapinzani mara zote wana hoja ambazo wananchi wanazikubali hivyo wameanza kuchukua mbinu za kuwa pre-empt. Waliotufikisha hapa si wao wenyewe? - wamepigiwa kelele juu ya kufufua shirika la mafuta (TPDC?) lakini wamepiga chenga na kutia nta ndani ya sikio. Biashara huru haizuii serikali ku intervene pale inapoona maslahi ya nchi yanatishiwa. Nchi tajiri zenyewe zinazotupatia solutions za kizumbukuku wako tayari kuvamia mahala wanapoona pana maslahi yao kiuchumi - kwani hawajui forces za demand and supply? Mtu asitudanganye kuwa kwenye biashara za kwetu huku tuna perfect competition -- haipo na bila serikali kuwa macho na kinachoendelea kwenye uchumi basi wanyonge ambao ni wananchi daima wataumia.
 
Whatever the case mkuu serekali lazima ioneshe ipo na sio ya kuchezewa hata kwa gharama fulani fulani.....

1. Tatizo ni kama alivyocomment PAULSS, #7
2. wanaotegemewa kutoa maamuzi upande wa Serikali baadhi ni sehemu ya wawekezaji kwenye sekta hiyo ya mafuta. Si tumeona hama waliokwenda bungeni au Waliokuwa mawaziri ndo wameshikiria au wanafukuzia taasisi zilizobinafsishwa!(zilizobinafsishwa na wao wakiwa madarakani/bungeni)!
 
Wanajamvi, ktk thread niliyotuma punde, maneno kuanzia "kama Jeshi likishindwa....." hayo ni maoni yangu na si ya mheshimiwa Zitto.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
I have to say pamoja na ulegelege ambao serikali imekuwa inaonesha huko nyuma sikuwahi kufikiria hata chembe kuwa ingefikia kiwango hiki! Utendaji wa serikali umeshuka mno wandugu. Waziri mkuu anajisikiaje haya yote yanayotekea under his watch?
 
I have to say pamoja na ulegelege ambao serikali imekuwa inaonesha huko nyuma sikuwahi kufikiria hata chembe kuwa ingefikia kiwango hiki! Utendaji wa serikali umeshuka mno wandugu. Waziri mkuu anajisikiaje haya yote yanayotekea under his watch?

what to u expect from a planted PM who drops in tears so cheap like a woman?
 
Me namshangaa huyu rais wetu na Waziri wa Nishati na Madini ina maana wameshindwa kutoa tamko na likatimizwa ina maana wauza mafuta ndo wameshikilia nchi wanafanya wanavyopenda, Poor Kikwete
 
Sioni mantiki yeyote leo hii bunge linakaa kujadili hili suala wakati CCM wenyewe ndo walilianzisha. Na bado umeme ulifukuzisha watu kazi karibu kila kona, lakini haikuwahi kukubaliwa dharura, IPTL walikuwa wanazalisha 0 - 10MW wakati wana uwezo wa 100MW kisa mafuta,serikali ikakaa kimyaaaa sababu ya maslahi yao kukuguswa! Leo hii mafuta ndo yanasababisha waamke usingizini. Hii inchi inakoelekea siko, tutakuja kufanyiana mbaya.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Niseme kwa nguvu zote kabisa kwenye hii saga ya mafuta kuna OPTION moja tu.

Serikali IFUTE leseni zote (zote kabisa) za wazuza mafuta, na watoe application form upya na kuweka masharti yanayolinda maslahi ya nchi.

Kwa miaka mitano sasa wauza mafuta wamefanya Tanzania shamba la bibi na wametengeneza faida kubwa sana kiasi kwamba hata kama watufunga watagoma/wataacha kuuza mafuta kwa mwezi bado hawatatikisika financially. Hii ni hatari sana kuwa na kikundi cha watu wanatumia pesa wanakwamisha shughuli za jamii yote.

Nadhani serikali kama ingeweleza wananchi na kuwaomba uvumilivu wakati wanasuka upya utuoji wa leseni watu wengi wangewaelewa. Futa wote anza upya.

Kwenye hili tupo pamoja, hawa watu wamezidi-wangeonyeshwa njia ya kutokea na wasirudi hata kusalimia rafiki zao!!!
 
Arudishe kwanza mamilioni ya dola alizozikopa NASDAQ kwa ajili ya kununulia ubunge Bubumbuli ili thamani ya shilingi ipate kuimarika na hatimaye bei ya mafuta ipate kushuka nako baada ya CCM yenyewe nayo kuondoa cha juu chake cha kampeni kwenye bei zetu za mafuta.

Tofauti na hapo huyu bwana mdogo atakua tu anatafutia tu kwetu bakora!!!!!!!!

Mbunge wa Bumbuli Januari makamba ameomba mjadala wa dharura kujadili ukosekanaji wa mafuta unaotokana na wenye vituo kugoma na kupelekea nchi kuwa kwenye wakati mgumu

UPDATES
Hoja imekubaliwa na mjadala unaanza sasa kwa January mtoa hoja kuanza
 
Vile vituo vilivyokubali kuuza muda huu unavigeuza kuwa vya 'dharura' wakati unasuka upya mambo.

Pamoja na hayo, kauli ya Rais au Waziri mkuu iko wapi? kwa nini hawajaongea mpaka sasa. Bunge limeguuka kuwa Ikulu? This is a tragedy of its own, and where is the cabinet in all these? Bunge ni kitu cha mbali sana maana wabunge are 'legislatures' - watunga sheria. Serikali ni watendaji, sasa, wako wapi hawa watendaji?

Mkuu kwa kifupi hakuna Serikali, nasema hivi kwa sababu haiwezekani Watendaji wakuu wa Serikali wawe kimya kabisa katika tatizo kubwa kama hili. Serikali inabidi ishinikiwe ili ijiuzulu lakini hili la kujiuzulu Bongo halipo hivyo wataendelea kupeta tu huku Wananchi wakiendelea kutaabika.
 
Ingekuwa ni wanafunzi wamegoma kuingia darasani basi wangevurumishiwa mabomu ya machozi, risasi za moto na maji ya kuwasha.....lakini muuza mafuta ANAIPA SERIKALI 24hrs na "serikali" inachekacheka tuuuu...

Umeona eeh! Undumilakuwili wa Serikali hii dhaifu ina ubavu wa kuonea Wanafunzi kila wanapodai haki zao huwaamrisha FFU wawapige virungu na mabomu ya machozi lakini hawa mafisadi wauza mafuta inawaogopa sana, Serikali imefyata mkia.
 
Hivi ni kwanini CCM na serekali yake wanashindwa kufanya maamuzi rahisi kama kuwafungia leseni. Inakuwaje wana nguvu ya dola ya kudhibiti upinzani wana wanawashindwa wafanya biashara wa mafuta ambao hawafiki hata elfu kumi?
 
Mheshimiwa Zitto kasema, ikifika saa kumi na mbili leo jioni, kama hawajafungua vituo, basi jeshi liende likasimamie na lifanye kazi hiyo, wakati hao waliofunga vituo wanachukuliwa hatua za kunyang'anywa leseni zao. Kama na jeshi watashindwa, basi dalili za kutokea yaliyotokea London siku tatu hizi zilizopita ni wazi kwa Tanzania, hasahasa ktk miji yetu mikubwa. Hayo yote yanakuja kutokana na udhaifu wa baadhi ya watendaji Serikalini.
<br />
<br />

sidhani kama kutumia jeshi ni strategy yenye kuleta suluhu ya muda mrefu. Kumbuka issue si wasambazaji tu, ila pia ni waagizaji wa mafuta.

Kama jeshi litalitaingilia kuuza mafuta yaliyoko kwenye pump, yakiisha basi tena.
Kumbuka huwezi kuwalazimisha wafanyabiashara waagize kwa nguvu kwa pesa yao. Je serikali inayo hela ya kuagiza mafuta yenyewe kwa dharula hii?

Kama serikali itachukua ushauri wa zitto basi itaifanya hali kuwa mabaya zaidi!
Mimi sioni hata faida tuliyoipata watumiaji wa mafuta kwa kupunguziwa sh. 100 kwa lita na kusababishiwa huu usumbufu! Ni bora tungeendelea kulipa hii sh 100 kuliko huu usumbufu. Na hata hivyo hili punguzo halitadumu hata mwezi mmoja kabla bei haijapanda tena.

Serikali haina nia ya kupunguza bei ya mafuta maana bado wanapata hele nyingi tu ya kodi zaidi ya 500 kwa lita. Kama wangekuwa na nia ya dhati wangepunguza angalau wabakiwe na sh. 200 kwa lita kama kodi ya serikali. Kodi zenyewe wanazokusanya zinaishia mifukoni mwa watu. Kodi za mafuta na Paye ni rahisi kukusanywa ndo maana ni kubwa kupita kiasi. Kuna kodi nyingi hazikusanywi kwa sababu zinzugumu wa kuzifatilia kutokana na mfumo mbovu

Serikali imeshindwa hata kuanzisha system ya namna transaaction zote kubwa zifanyike kupitia computerised system na banking ili kudhibiti ukwepaji kodi kwa sababu ya cash based transactions.

Wamekalia kubana tu kwenye vyanzo rahisi vya kodi kama mafuta na paye.

Mimi napendekeza wawaachie tu wauza mafuta maana hamna faida yoyote mtumiaji anaaipata kwa kupunguza hiyo sh.100 kuliko kusababisha hii kharaha ya misongamano ya magari,pikipiki, bajaji na vidumu kwenye vituo vinavyouza mafuta.
 
Mnyika ana ushahidi wa maafisa wa serikali waliohongwa kuhusu hili swala....anashangaa serikali inamiliki 50% ya hisa za BP lakini wao ndo kwanza wamegoma....
<br /> <br / wezi wote hao magamba wamiliki hisa 50% hlf wajidai kugoma! TUINGIENI MTAANI KM JANUAR MAKAMBA ALIVYOSEMA
 
Back
Top Bottom