BUNGENI: Mchango wa Prof. Sospeter Muhongo amechangia na kutoa ushauri ufuatao

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu Jana Prof Sospeter Muhongo amechangia Kwenye Bajeti ya Nishati na kutoa ushauri ufuatao:

(1) Ukuaji wa uchumi wetu uendae na upatikanaji wa umeme mwingi na wa bei nafuu

GDP/Capita:
*US$ 3,000 na MW 10,000 -15,000
*US$ 1,500 na MW 5,000

(2) Tuwe na Vyanzo vingi vya uzalishaji wa umeme - Energy Mix yetu ni: (i) Natural Gas, (ii) Hydro, (iii) Coal na (iv) Renewable Energies (solar, wind na aina nyingine 9)

(3) TPDC ibaki kwenye majukumu yake ya kutafuta mafuta na gesi asilia (oil & gas exploration and development)

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
HAYO NI MANENO YA PROFESOR MHONGO MWAKA 2013

Tanzania inakusudia kuanza kuuza umeme nchi za nje kufuatia mapinduzi yanayotazamiwa kufanyika kwenye sekta ya nishati na madini ukiwamo uendelezwaji wa mradi wa uzalishaji umeme katika eneo la Kinyerezi.

“Mipango yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2014 tayari tutakuwa na umeme wa ziada kiasi cha megawati 500 ambao tutauuza nje ya nchi, ilielezwa jana.

Ili kufikia azma hiyo, Wizara ya Nishati na Madini imebainisha maeneo ambayo inatazamia kuyawekea mkazo ili kuzalisha umeme wa kutosha. Maeneo hayo ni pamoja na uendelezwaji wa nishati ya gesi inayotazamiwa kuanza kuchimbwa mkoani Mtwara pamoja na utumiaji wa makaa ya mawe.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye alikuwa akizungumza kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya maelewano baina ya Shirika la Umeme Tanzania Tanesco na Kampuni ya kuzalisha umeme ya China Power Investment (CPI).

Waziri Muhongo alisema kuwa, Serikali pia inakusudia kuimarisha vyanzo vingine vya uzalishaji umeme ambavyo vitajumuisha umeme utokanao na upepo, jua na maji.
 
Asituchanganye huyu,kwenye hydro kwenyewe hatujamaliza,huyu anataka kuanza kutuvuruga,tumeshaingia gharama kubwa sana kwenye hili wacha kwanza limalizike ndio mlete siasa zenu...
 
Wakuu Jana Prof Sospeter Muhongo amechangia Kwenye Bajeti ya Nishati na kutoa ushauri ufuatao:

(1) Ukuaji wa uchumi wetu uendae na upatikanaji wa umeme mwingi na wa bei nafuu

GDP/Capita:
*US$ 3,000 na MW 10,000 -15,000
*US$ 1,500 na MW 5,000

(2) Tuwe na Vyanzo vingi vya uzalishaji wa umeme - Energy Mix yetu ni: (i) Natural Gas, (ii) Hydro, (iii) Coal na (iv) Renewable Energies (solar, wind na aina nyingine 9)

(3) TPDC ibaki kwenye majukumu yake ya kutafuta mafuta na gesi asilia (oil & gas exploration and development)

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sasa huo ndio mchango? Nikajua kuna kitu spesheli..

Badala ya Biteko,huyu angepewa Wizara ya Madini anaonekana kuyajua Sana haya mambo na ni mfuatiliaji mzuri.
 
Back
Top Bottom