Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
Ntaweka hotuba yote ili muweze kuona jinsi ambavyo hakujibu maswala ya msingi na ambayo yanapaswa kujibiwa .
Magufuri ni Msanii tu, anadanganya watoto wadogo.
Ntaweka hotuba yote ili muweze kuona jinsi ambavyo hakujibu maswala ya msingi na ambayo yanapaswa kujibiwa .
Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2005-2010 kitakwimu ni kuwa serikali iliweza kukamilisha miradi 15 kwa kiwango cha lami na hivyo kujenga barabara zenye urefu wa Kilomita 1,398.6. Kasi hii Haitii matumaini hata kidogo kwani kwa mujibu wa ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2010-2015 imepanga kumalizia ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1,140 (barabara 9 )ambazo ni miradi ambayo ilikuwa haikukamilika kwenye kipindi cha 2005/2010 na kuanza ujenzi mpya wa kilomita 5,282 kwa kipindi cha 2010-2015 (takwimu hizi ni kwa mujibu wa Ilani ya CCM 2010-2015).takwimu hizi ni sawa na kusema kuwa serikali itaweza kujenga kilomita 6,422 za lami katika kipindi cha miaka mitano.
Wakati huo huo Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano unaonyesha kuwa ni barabara zenye urefu wa kilomita 5,552 tuu ndio zitaweza kutengenezwa kwa kiwango cha lami kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2011/2012-2015/2016).
Mheshimiwa Spika, takwimu hizi hazijahusisha mpango wa serikali wa kujenga barabara kwa viwango vya Changarawe na zile za vijijini kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.
Kambi ya Upinzani, tunasubiri kuona muujiza huu wa serikali kujenga barabara zenye urefu mkubwa kuliko zilizojengwa tangu wakati wa uhuru yaani kwa kipindi cha miaka 50 ndani ya miaka 5 . Na haswa ikizingatiwa kuwa kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita (2005-2010) serikali hiyo hiyo iliweza kujenga kilomita 1,398.6 tuu za kiwango cha lami kwa kipindi hicho (Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010-2015 -Mafanikio katika Sekta ya Miundombinu" uk.6 ) .
Tunasema hivyo kwa sababu tunaona kuwa wananchi wanapewa matumaini makubwa ya miradi mingi ya barabara wakati fedha kwa ajili ya barabara hizo hazionekani kutengwa kwa ajili ya kuweza kuzijenga.
Pili, kambi ya Upinzani, tunataka kupata majibu ni takwimu zipi zipo sahihi, je? Ni za Ilani ya uchaguzi ya CCM ama ni mpango wa Taifa wa Maendeleo? kuhusiana na jumla ya kilomita za barabara ambazo zitajengwa kwa miaka mitano ijayo.
Shida yake ni pale anapochanganya siasa na miundo mbinu, hilo ndilo litakalomshinda!
Hili ni jambo kubwa sana na hakutaka kulizungumzia kabisa na ameamua kulikalia kimya .
Miradi maalum ya ujenzi wa Barabara (kasma 4168).Mheshimiwa Spika, kitabu cha Miradi ya Maendeleo part-A volume iv katika fungu 98, kasma 4168 utaona kuwa kuna mradi unaitwa Miradi ya ujenzi wa barabara maalum (special road construction projects) na fungu hili limetengewa kiasi kikubwa kuliko mradi mwingine wowote wa ujenzi wa barabara katika mwaka huu wa fedha kwani zipo jumla ya shilingi 348,075,000,000 na hizi zote ni fedha za ndani, kwa hakika hizi ni fedha nyingi sana na haswa ikizingatiwa kuwa kitabu hicho kimeonyesha miradi yote ya ujenzi wa barabara ambayo itatekelezwa katika mwaka huu wa fedha , ila hii miradi maalum haijaonyeshwa ni miradi ya barabara gani na zitajengwa wapi.
Mheshimiwa Spika, kasma hii kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na 2010/2011 haikuwa imetengewa kiasi chochote cha fedha na ndio maana imetustua kuona mwaka huu fedha nyingi kiasi hicho kinatengwa kwa miradi isiyojulikana kuwa itajengwa wapi.
Mheshimiwa Spika, hata ukiangalia maelezo yaliyotolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Miundombinu juu ya mpango na bajeti ya mwaka 2011/12 kasma 4168 haipo kwenye randama na hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhusiana na fedha hizo ambazo zimetengwa.
Shida yake ni pale anapochanganya siasa na miundo mbinu, hilo ndilo litakalomshinda!
<br /><font size="3"><br />
Ahaa aaa ulikuwa umelala wapi? unadhani anaweza kutetea chama gani Mkuu? umenichekesha sana kama ulikuwa humjui Magufuri</font>
Kabisa Mkuu. Ana base sana kwenye ilani ya CCM kuboresha miundombinu. Tatizo kubwa la ilani ya CCM hatekelezeki. Realistically, ilani ya CCM ya kutengeneza kilomita za barabara walizotaja ndani ya miaka mitano, is not achievable. Chukulia mfano Serengeti Highway. Hii ilikuwepo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2005, tuliambiwa kuwa barabara ingekamilika kabla ya uchaguzi uliopita. Ilani ya uchaguzi wa 2010 tumeambiwa hivyo hivyo.
Ilani inaandaliwa na nani?
Unajua Magufuli anatumia kutokujua kwa wananchi kuipa ccm umaarufu sasa kwa bahati mbaya anakutana na maswali ambayo hawezi kujibu pamoja na umahiri wake.Ntaweka hotuba yote ili muweze kuona jinsi ambavyo hakujibu maswala ya msingi na ambayo yanapaswa kujibiwa .
....Umenena vyema...anajua ku-memorize ndo silaha yake kwa wenye kumbukumbu haba.kwa lipi kutaja idadi ya barabara bila kujibu hoja za msingi?
Mheshimiwa Spika, Serikali iliandaa mpango wa kujenga barabara wa kipindi cha miaka 10 (2007/08- 2016/17 Transport Sector Investment Program (TSIP). Na kwa awamu ya kwanza mpango huu ulikadiriwa kutumia US$6.2 billion (takribani trilioni 9 za kitanzania) (2007/08 mpaka 2011/12) .Ni dhahiri kuwa mpango huu kwa awamu ya kwanza ndio unafikia ukomo wake kwenye bajeti hii.
Kambi ya Upinzani, tunataka kupata majibu kama lengo lililokusudiwa lilifikiwa ama kulikuwa na ukomo wa bajeti katika kutekeleza mpango huu ili hatimaye sasa tuweze kuingia kwenye awamu ya pili.
Pia tunataka kupata majibu ni kilomita ngapi za lami zilijengwa katika awamu hii ya kwanza na haswa ikizingatiwa kuwa Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 umetenga kiasi cha shilingi trilioni 6,793 kwa ajili ya kujenga kilomita 5,204.7 za lami hapa nchini (Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 uk.55) ambazo ni ndogo kuliko zilizotumika kwenye awamu ya mpango huu ambao unafikia ukomo wake mwaka huu wa fedha.
Sasa turidi nyuma. Kwa nini Waziri Mkuu Pinda alipanda ndege kwenda kwenye jimbo la Magufuli na kutangaza mbele ya wapiga kura wake kuwa bomoabomoa imepigwa stop? Kama ilikuwa ni lazima ku-mpiga stop kwa nini asifanye hivyo hapa Dar au akamuita ofisini kwake na kumweleza hayo aliosema mbele ya kadamnasi?. Pinda 'alitumwa' kumshushia hadhi mbele ya wapiga kura wake? Na kama ndio, nani alimtuma Pinda na kwa sababu zipi? Siasa za kuviziana ndio zimeua CCM.