Bungeni: Magufuli azichambua barabara Tanzania kama karanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni: Magufuli azichambua barabara Tanzania kama karanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchemsho, Aug 2, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Waziri wa ujenzi Mh. Magufuli yuko anajibu hoja mbalimbali za wabunge kwa kutamka idadi ya umbali kwa km, wakandarasi wanaojenga na kiasi cha fedha zinazotumika.

  Anachoni-boa ni anaposema wanajenga barabara za lami ili wale wanaoandamana wapite kwenye barabara za lami zinazojengwa na CCM inayoongozwa na Kikwete.

  Je na yeye anaanza kuwatetea magamba.?

  =============
  Wapinzani:
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Amezitaja barabara kibao za tz na kilometa zake pamoja na idadi ya wakandarasi bila kudesa
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hapa dar mbona mavumbi tuu!!! miaka 50 bado anataja vumbi tuuu. hana lolote huyo.
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,032
  Likes Received: 3,056
  Trophy Points: 280
  Ameanza kulewa pombe!!!
   
 5. M

  Masanyaraz Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akanichekesha aliposema CHADEMA watengeneze libarabara lao waliite chadema,hata ccm wakitaka kuandamana waandamane huko!nimecheka lakini kwa hasira kwasababu MAKUFULI ameongea kinafiki.
   
 6. oba

  oba JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa uhakika pamoja na siasa anazochanganya huyu jama magufuri( ambazo zinaboa infact) yuko smart ktk eneo lake la kazi, kama ccm wote na serikali yake wangekuwa na nia ya kuzingatia sheria kama mzee magufuri basi nchi hii ingekuwa mbali na wapinzani wasingekuwa na hoja ktk eneo la miundo mbinu. Tatizo la viongozi wengine wa ccm ni irresponsible, jifunzeni kwa magufuri mtaikomboa ccm yenu!
  Nawasilisha!
   
 7. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Magufuli ni mbabaishaji mkubwa sana kwani hajajibu hoja za msingi kama zilivyoibuliwa na kamabi ya upinzani jana kwenye hotuba yao na badala yake amekuwa akitaja barabara tuu ambazo hazieleweki.
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, Serikali iliandaa mpango wa kujenga barabara wa kipindi cha miaka 10 (2007/08- 2016/17 Transport Sector Investment Program (TSIP). Na kwa awamu ya kwanza mpango huu ulikadiriwa kutumia US$6.2 billion (takribani trilioni 9 za kitanzania) (2007/08 mpaka 2011/12) .Ni dhahiri kuwa mpango huu kwa awamu ya kwanza ndio unafikia ukomo wake kwenye bajeti hii.

  Kambi ya Upinzani, tunataka kupata majibu kama lengo lililokusudiwa lilifikiwa ama kulikuwa na ukomo wa bajeti katika kutekeleza mpango huu ili hatimaye sasa tuweze kuingia kwenye awamu ya pili.

  Pia tunataka kupata majibu ni kilomita ngapi za lami zilijengwa katika awamu hii ya kwanza na haswa ikizingatiwa kuwa Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 umetenga kiasi cha shilingi trilioni 6,793 kwa ajili ya kujenga kilomita 5,204.7 za lami hapa nchini (Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 uk.55) ambazo ni ndogo kuliko zilizotumika kwenye awamu ya mpango huu ambao unafikia ukomo wake mwaka huu wa fedha.
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kwamba hilo neno amechomekewa na waliomsaidia ku-type katika dakika za mwisho kabisa. Tetesi zinadai yeye aliandika hivi "tunajenga barabara za lami ili ziweze kupitika nyakati zote". si unajua CCM kwa uchakachuaji hata hotuba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. oba

  oba JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shida yake ni pale anapochanganya siasa na miundo mbinu, hilo ndilo litakalomshinda!
   
 11. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2005-2010 kitakwimu ni kuwa serikali iliweza kukamilisha miradi 15 kwa kiwango cha lami na hivyo kujenga barabara zenye urefu wa Kilomita 1,398.6. Kasi hii Haitii matumaini hata kidogo kwani kwa mujibu wa ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2010-2015 imepanga kumalizia ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1,140 (barabara 9 )ambazo ni miradi ambayo ilikuwa haikukamilika kwenye kipindi cha 2005/2010 na kuanza ujenzi mpya wa kilomita 5,282 kwa kipindi cha 2010-2015 (takwimu hizi ni kwa mujibu wa Ilani ya CCM 2010-2015).takwimu hizi ni sawa na kusema kuwa serikali itaweza kujenga kilomita 6,422 za lami katika kipindi cha miaka mitano.

  Wakati huo huo Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano unaonyesha kuwa ni barabara zenye urefu wa kilomita 5,552 tuu ndio zitaweza kutengenezwa kwa kiwango cha lami kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2011/2012-2015/2016).

  Mheshimiwa Spika, takwimu hizi hazijahusisha mpango wa serikali wa kujenga barabara kwa viwango vya Changarawe na zile za vijijini kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.

  Kambi ya Upinzani, tunasubiri kuona muujiza huu wa serikali kujenga barabara zenye urefu mkubwa kuliko zilizojengwa tangu wakati wa uhuru yaani kwa kipindi cha miaka 50 ndani ya miaka 5 . Na haswa ikizingatiwa kuwa kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita (2005-2010) serikali hiyo hiyo iliweza kujenga kilomita 1,398.6 tuu za kiwango cha lami kwa kipindi hicho (Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010-2015[FONT= ] -Mafanikio katika Sekta ya Miundombinu"[/FONT] uk.6 ) .

  Tunasema hivyo kwa sababu tunaona kuwa wananchi wanapewa matumaini makubwa ya miradi mingi ya barabara wakati fedha kwa ajili ya barabara hizo hazionekani kutengwa kwa ajili ya kuweza kuzijenga.

  Pili, kambi ya Upinzani, tunataka kupata majibu ni takwimu zipi zipo sahihi, je? Ni za Ilani ya uchaguzi ya CCM ama ni mpango wa Taifa wa Maendeleo? kuhusiana na jumla ya kilomita za barabara ambazo zitajengwa kwa miaka mitano ijayo.
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,399
  Trophy Points: 280
  la kuvunda halina ubani!
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hili ni jambo kubwa sana na hakutaka kulizungumzia kabisa na ameamua kulikalia kimya .

  Miradi maalum ya ujenzi wa Barabara (kasma 4168).Mheshimiwa Spika, kitabu cha Miradi ya Maendeleo part-A volume iv katika fungu 98, kasma 4168 utaona kuwa kuna mradi unaitwa "Miradi ya ujenzi wa barabara maalum" (special road construction projects) na fungu hili limetengewa kiasi kikubwa kuliko mradi mwingine wowote wa ujenzi wa barabara katika mwaka huu wa fedha kwani zipo jumla ya shilingi 348,075,000,000 na hizi zote ni fedha za ndani, kwa hakika hizi ni fedha nyingi sana na haswa ikizingatiwa kuwa kitabu hicho kimeonyesha miradi yote ya ujenzi wa barabara ambayo itatekelezwa katika mwaka huu wa fedha , ila hii miradi maalum haijaonyeshwa ni miradi ya barabara gani na zitajengwa wapi.

  Mheshimiwa Spika, kasma hii kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na 2010/2011 haikuwa imetengewa kiasi chochote cha fedha na ndio maana imetustua kuona mwaka huu fedha nyingi kiasi hicho kinatengwa kwa miradi isiyojulikana kuwa itajengwa wapi.

  Mheshimiwa Spika, hata ukiangalia maelezo yaliyotolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Miundombinu juu ya mpango na bajeti ya mwaka 2011/12 kasma 4168 haipo kwenye randama na hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhusiana na fedha hizo ambazo zimetengwa.

  Kambi ya Upinzani, tunataka kupata maelezo ya kina ni miradi gani hii ambayo haiwezi kuandikwa na inatengewa fedha nyingi kiasi hicho? Kwani hii italiwezesha Bunge kuweza kupitisha bajeti inayolifahamu na kuisimamia serikali na kuweza kufuatilia utekelezaji wa miradi hii.
   
 14. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ntaweka hotuba yote ili muweze kuona jinsi ambavyo hakujibu maswala ya msingi na ambayo yanapaswa kujibiwa .
   
 15. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  magufuli kichwaaaaa.
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  kwa lipi kutaja idadi ya barabara bila kujibu hoja za msingi?
   
 17. A

  Amanyisye Member

  #17
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kichwa kulinganisha na magamba wengine lakini pale alikuwa anapiga porojo tu,yaani mtu yoyote anayeweza kuongea na kuchomekea utani watu wakacheka mwisho wa siku watu watasahau kama hakuongea point.
   
 18. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Twitter ya zitto
  yangu macho sasa   
 19. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Jamaa najitahidi kuifahamu nchi yetu vizuri,anajitahidi kuwa katika miradi husika kwa wakati
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Ahaa aaa ulikuwa umelala wapi? unadhani anaweza kutetea chama gani Mkuu? umenichekesha sana kama ulikuwa humjui Magufuri
   
Loading...