​Katika mchango wake katika bajeti ya Serikali, Mhe Mbatia amegusia suala moja ambalo kwakweli lina utata sana.
Taasisi ya Aghakan nchini ina mkataba na serikali wa kutolipa kodi zote (zero tax) nchini kwa sababu kwamba wanatoa huduma za elimu na afya kwa watanzania masikini kwa ghafama nafuu
Lakini cha ajabu ni kwamba hospitali na shule za aghakhan ni most expensive kuliko shule na hospitali nyinginezo. Je kuna maaana gani watu hawa kuendelea kupewa exemption. Naambiwa hata toilet paper inayonunuliwa na aghakhan hailipiwi kodi...achilia mbali magarim vifaaa n.k
Tena wanachofanya, wanawatoza watanzania waswahili na makampuni ya nchini very high premium pale hospitali alafu wana wa subsidize wahindi wa jumuiya ya ISMAILIA ndio wanatibiwa bure pale. Kufanya operation ya appendix pale ni shilingi milioni 2, wakati same operation Tumaini Hospitali ni shilingi 400,000 na St Benard hospital ni shilingi 600,000.
Iweje Agakhan wasilipe kodi ihali Hindumandal ambayo nayo ni ya kidini wanalipa kodi?. Tunaambiwa Regency Hospital ni moja ya walipakodi wakubwa katika TRA kanda ya Ilala.....wanalipa kodi karibia shilingi bilioni 2 kwa mwaka.....sasa aghakhan ambayo ni ghali kuliko regency na ina operations maradufu ya regency si ilipe kodi tu. hii ndio mianya ya upotevu wa fedha za serikali...
Hongera Mhe Mbatia kwa kuliongelea suala hili bungeni