Bunge, sala ya ijumaa na sensitivity to religious issues

sharrif2

Member
Sep 5, 2008
9
4
NAAM, sasa nadhani nimejua kwanini kuna baa zinajengwa karibu na misikiti au kanisa; kwanini nguruwe wanafugwa jirani na Waislamu; kwanini magesti hausi yako nyuma ya makanisa na mambo kama hayo.

Hivi Waziri Mkuu na Spika naye hawakujua kwamba Ijumaa iliyopita yaani tarehe 30 Agosti 2009 wabunge Waislamu walipaswa kuwa misikiti kuaga Shabani na kukaribisha Ramadhani?

Mbunge uko wapi mbona hoja hii hukuitoa au kwa kuwa mwenzangu ulitoka kimya kimya tu kwenda sali bila kunishtua?

Lakini utani tuache mbali lazima jamani tujenge utamaduni wa kuwa na hisia nzito juu ya mambo ya dini hasa panapakuwa na mikutaniko na mikusanyiko ya watu. Hivi tunashindwa kupanga mambo yetu tukawastahi wanaoswali mchana au kwa kuwa wengine hawasali basi watajua huko huko. Mimi nina wasiwasi kama tutakuwa salama sana tukiendelea na tabia hiyo huko mbele ya safari.
 
Sasa kama misikiti na makanisa yalikuta hizo baa na gesti haus? Kwani kuwa karibu na baa na gesti haus nako ni makosa? Mbona yanayofanyika humo yanafanyika katika nyumba zetu? Kwani kukaa karibu na kuliko na nguruwe nako kunakatazwa? Mimi nilidhani ni kula tu?

Kwani kila ijumaa inakuwaje? Mbona kwenye maofisi ya serikali waislamu ni ruksa kwenda kuswali wakati huo! Huko bungeni ni tofauti? Yaani KM na Spika waliwazuia waislamu kwenda kuswali? Kama ni hivyo walikosea.
 
Kuna watu katika nchi hii wana utamaduni wa kulalamika hata kwa vitu visivyo na miguu wala kichwa! Poleni sana
 
Hivi Waziri Mkuu na Spika naye hawakujua kwamba Ijumaa iliyopita yaani tarehe 30 Agosti 2009 wabunge Waislamu walipaswa kuwa misikiti kuaga Shabani na kukaribisha Ramadhani?

Mbunge uko wapi mbona hoja hii hukuitoa au kwa kuwa mwenzangu ulitoka kimya kimya tu kwenda sali bila kunishtua?

.

Ratiba ya public holidays inajulikana na ipo kwenye kalenda ya Serikali wewe ukipewa uspika utafanya vituko vya kujiwekea kalenda yako. Mbunge hakutoa hoja hii kwa sababu aliona haina kichwa wala mkia.
 
Hivi Waziri Mkuu na Spika naye hawakujua kwamba Ijumaa iliyopita yaani tarehe 30 Agosti 2009 wabunge Waislamu walipaswa kuwa misikiti kuaga Shabani na kukaribisha Ramadhani?

Mbunge uko wapi mbona hoja hii hukuitoa au kwa kuwa mwenzangu ulitoka kimya kimya tu kwenda sali bila kunishtua?

Lakini utani tuache mbali lazima jamani tujenge utamaduni wa kuwa na hisia nzito juu ya mambo ya dini hasa panapakuwa na mikutaniko na mikusanyiko ya watu. Hivi tunashindwa kupanga mambo yetu tukawastahi wanaoswali mchana au kwa kuwa wengine hawasali basi watajua huko huko. Mimi nina wasiwasi kama tutakuwa salama sana tukiendelea na tabia hiyo huko mbele ya safari.

hakuna mbunge anazuiliwa kuondoka Bungeni kwenda kwenye ibada, wakati wowote ule. hakukuwa na haja ya Spika kuahirisha shughuli za bunge kwa ajili hiyo.
Wenye kujali dini yao nakuhakikishia walitoka na kwenda kutimiza takwa hilo.
naanza kupatwa na woga sana kutokana na kauli yako kuwa 'tujenge utamaduni wa kuwa na hisia nzito juu ya mambo ya dini'. Napatwa na wasi wasi kwa kuwa sijakuelewa kiundani unamaanisha nini ingawa kwa juu juu unaonekana kushabikia fundamentalism. Kuwa na hisia nzito kama hizo kwenye mikutano na mikusanyiko ya watu, katika nchi ambayo katiba yake inasema kuwa suala la dini ni la mtu binafsi, ni kutaka kuwahusisha watu wengine katika hisia ambazo hawapendi kuwa nazo. Is that what you are trying to tell us bwana mkubwa?
 
NAAM, sasa nadhani nimejua kwanini kuna baa zinajengwa karibu na misikiti au kanisa; kwanini nguruwe wanafugwa jirani na Waislamu; kwanini magesti hausi yako nyuma ya makanisa na mambo kama hayo.

Hivi Waziri Mkuu na Spika naye hawakujua kwamba Ijumaa iliyopita yaani tarehe 30 Agosti 2009 wabunge Waislamu walipaswa kuwa misikiti kuaga Shabani na kukaribisha Ramadhani?

Mbunge uko wapi mbona hoja hii hukuitoa au kwa kuwa mwenzangu ulitoka kimya kimya tu kwenda sali bila kunishtua?

Lakini utani tuache mbali lazima jamani tujenge utamaduni wa kuwa na hisia nzito juu ya mambo ya dini hasa panapakuwa na mikutaniko na mikusanyiko ya watu. Hivi tunashindwa kupanga mambo yetu tukawastahi wanaoswali mchana au kwa kuwa wengine hawasali basi watajua huko huko. Mimi nina wasiwasi kama tutakuwa salama sana tukiendelea na tabia hiyo huko mbele ya safari.

Kwa mtazamo wangu,unaweza kuwa na kitu kizuri cha kusema kwenye hili..
Ila ya kupasa kukaa chini na kutazama ...mambo yanavyo kwenda hapa kwanza.
Then unajenga HOJA vizuri na unatuletea tuchangie ikiwa ina eleweka.
No string attached ila ilikupasa utulie kwanza kama mnavyo kua huko MJENGONI.
 
Serikalai haina dini, wenye dini kazi kwenu nenda msali hamtaki msilalamikie wengine hapa.
Kwani kwenda sala unahitaji ruhusa ya nani?
Mwisho sasa nadhani bado kidogo mtaomba spika au PM awape chumba bungeni ili wabunge waislamu wawe wanasalia hapo.
This is nonsense
 
Back
Top Bottom