Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source: Nipashe Ijumaa
Kumekuwepo na Uvumi na upotoshaji mkubwa unaoendelea katika mitandao ya kijamii hasa hapa JF kuhusu kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye.

Upotoshaji huo umejitokeza kufuatia Nukuu ya gazeti moja la kila siku la Nipashe kunukuu kauli ya Nape juu ya mjadala unaoendelea hivi sasa kuhusu kuonyeshwa ama kutooneshwa kwa Bunge la Jamhuri. Kilichojitokeza ni kuwa Mwandishi wa Gazeti hili aliwasiliana na Mwenezi kutaka maoni yake juu ya suala hilo na ndipo Nape alipofafanua kuwa hawezi kupinga suala la kuonyeshwa kwa Bunge live na kueleza kuwa tunalo tatizo la msingi la kushuka kwa nidhamu ndani ya vyombo vyetu vya maamuzi wakati mwingine lakini lazima tufikiri katika njia sahihi zaidi katika kutatua matatizo hayo bila kuzalisha matatizo mengine zaidi.

Hakuna maana wala tafakuri iliyo sawa inayoweza kukubaliana na uamuzi wa kutoonyesha bunge ili kukuza nidhamu ya wawakilishi bali ni lazima kanuni zilizopo zifuatwe na zipewe makali zaidi ya kuwashughulikia wale wenye kufanya makosa.

Ninachokisema ni kuwa tunahitaji muda zaidi wa kuonyesha bunge letu, ili kuwapa fursa wananchi kulifuatilia kwa umakini zaidi na kwa namna hiyo kuwaongezea ushiriki wao katika vyombo hivi vya kimaamuzi, lakini pia kuwaongezea hoja na vigezo vya maamuzi juu ya wawakilishi wao kwa yale wanayoyasema bungeni. Lakini pia hili la kutoonesha linakinzana na kanuni za utawala bora ambazo tunazifuata na kuzidumisha.

Hata hivyo Nape ameendelea kufafanua juu ya mjadala huo kupitia mitandao yake ya Kijamii, ambapo kwenye facebook ameeleza kama inavyoonekana chini
Nape Nnauye said:
Naunga mkono juhudi za kulifanya bunge letu liwajibike zaidi kwa wananchi na kuwa na heshima zaidi. Lakini naamini kutolionyesha "live" si moja ya juhudi hizo!

Lakini ni muhimu kujadili pia muda wa kurusha bunge ambapo wananchi wengi wanapata muda wa kuliangalia badala ya utaratibu wa sasa ambapo naamini watu wengi wapo/wanapaswa kuwa kazini.

Nape Nnauye
NILICHOKISEMA ni kuwa ni vizuri zaidi bunge likipewa airtime ya ziada hasa kwa muda ambao watu wengi wanakuwa majumbani.

Wakati mwingine ni makosa yanayojitokeza kwa waandishi wetu, lakini mara nyingine hayawi makosa halisi bali makosa yanayokusudiwa.
 
Anaelewa lakini Nape anachoongea!kwani suala ni watu wanaangalia saa ngapi!au ni vurugu zinazotokea bungeni!Mimi naona serikali imeshindwa na watu wachache je itaweza wananchi 44M.
 
Tatizo si muda,kuonyeshwa kwa bunge ni haki ya mtanzania....
 
nape sababu za kashilika na zako haziendani hapo ndipo nafahumu kuwa ww ni wa propaganda tu
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Huyu ana akili timamu kweli? Hivi anajua kuwa ni Watanzania wangapi wanaenda kazini? Tena maofisini? Mbona yeye anafanya mikutano ya hadhara saa za kazi?
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Hii ni kuthibitisha kwamba uamuzi wa kutaka bunge lisionyeshwe live umefanywa na ccm na katibu wa bunge ndugu Kashilila ameutangazia umma maamuzi ya ccm kwa mgongo wa ofisi ya bunge.
Nape Nnauye anachekesha sana tena huyu bwana mdogo ni wa kuhurumiwa. Yani hajui kwamba kuna watu wengi sana wanafuatilia bunge? ni ukweli kwamba wananchi wengi wanafuatilia bunge na ndio maana wamekuwa mstari wa mbele kukosoa mwenendo mbaya wa uendeshaji wa vikao vya bunge hasa kwa vitendo vya spika na naibu wake kusigina kanuni kukipendelea chama chao.
 
Last edited by a moderator:
Yaani serikali imeshindwa kabisa bungeni sasa wanaamua kujizika kabisaaaa
 
Asubuhi ni muda wa kazi. Ukienda ofisini halafu usihudumiwe kisa mfanyakazi yupo busy kwa kuangalia bunge utajisikiaje?

Bunge lisionyeshwe live, wawe wanaonyesha marudio yake yote saa tano na nusu usiku.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
HII MANENO NDIO INAWAPONZA...........HAWAPENDI TUIONE

bingoland.jpg
 
Tatizo si muda,kuonyeshwa kwa bunge ni haki ya mtanzania....

Kaka sio ufinyu wa kufikiri. Ni fanya yote usiombe kutawaliwa na kuendeshwa na akili za watu wengine ambao wanakuendesha kwa matakwa yao. Kama vile remote contol na TV. Unakuwa kama upo kwenye ndoa vile maana saa nyingine inabidi ufanye kila jitihada kumfurahisha mwenzio hasa wakiume.
 
Dalili za mwisho wa Uhai wa ma CCM. Bado kidogo tu wapige marufuku vikao vya bunge kwa singizio hakuna pesa za kuendesha shughuli za bunge
 
Nape Basi kipindi cha bunge kirushwe live kuanzia saa 1 usiku hadi 6 watu wanakua wapo majumbani si ndio?
 
Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo
lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu
wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa
mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa
mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta
heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Nape na Kashilila lao moja,kashilila ametumwa na nape.Suala hapa sio naangalia bunge saa ngapi,mimi nataka, nikitaka kuangalia bunge niangalie.Kwani watu wote wanaenda kazini asubuhi?
 
Nape akipata wasaa, asome tena hiyo nukuu aliyotoa kwenye gazeti la Nipashe. Inamvunjia heshma - yeye Nape- na pengine ni vema , in the future, akavuta pumzi na kutulia kabla ya kuongea na waandishi wa habari.

Kuonesha ni jinsi gani Nape amelikoroga, anasema: 'anaunga mkono jambo lolote linalota heshma kwa bunge'. Lakini anaendelea kwa kusema kuwa bunge linarushwa 'live' wakati wa asubuhi, na wakati huo (kwa maoni ya Nape) watu wako makazini, hivyo hawana muda wa kufuatili'

Kwa maneno mepesi sana, Nape anataka watu waazima na akili zao waamini kuwa kuonesha vikao vya bunge live- asubuhi kunalivunjia heshma bunge! Hii ni hadithi ya ajabu kabisa toka kwa Nape, na ndio maana nashauri asome tena nukuu yake ili aepushe chama chake na taifa kwa jumla na haya masimulizi ya kuanga-unga.

Heshma ya bunge haina uhusiano wowote na kurushwa live asubuhi, mchan, jioni au usiku wa manane. Kama bunge linaendeshwa kihuni kihuni, bila kufutata kanuni na taratibu zilizowekwa, usitegemee heshma. Kwa bahati nzuri tunayo mifano halisi. Bunge la Tanzania lilipata hesham kubwa wakati wa Spika Sitta. Na hii ni kwa sababu ya uelewa wake na kuheshimu utawala wa sheria lakini pia kuelewa kuwa bunge ni mhimili huru na wa muhimu kwa uhai wa taifa. Sitta aliongoza bunge kwa HAKI.

Makinda, kwa sababu anazozijua yeye, licha ya kuwa Naibu Spika wakati wa Sitta, amerudisha nyuma hatua zote tulizofikia, kama taifa kwenye suala zima la utawala wa sheria. Bunge haliwezi kuwa na heshma kama anayeongoza haelewi 'equation' ya heshma ya bunge inajumuisha nini? Bunge haliwezi kuwa na heshma kama mkalia kiti cha Spika anavuruga kanuni, taratibu,tamaduni/desturi zilizowekwa kuongoza bunge? Ukisshavuruga kanuni maana yake unaruhusu 'chaos'. Na dawa yake si kutoonesha vikao vya bunge 'live'. Hivyo, hoja ya Nape ni ya kipuuzi na haiwezi kutatua tatizo la msingi linaloharibu bunge.
 
ccm mfa maji haachi kutapatapa..... mwisho wa siku mtazuia ata camera bungeni...
 
Huyu ana akili timamu kweli? Hivi anajua kuwa ni Watanzania wangapi wanaenda kazini? Tena maofisini? Mbona yeye anafanya mikutano ya hadhara saa za kazi?

hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.
 
Kwani wananchi tuliwalalamikia kuhusu muda? Lengo sio hilo, naona mnataka kuedit kipindi ili kuficha madudu yanayopitishwa bungeni ikiweno kukwamisha hoja zenye maslahi kwa wananchi mf. hoja ya maji ya Mnyika. Hata mkituficha tayari tumeshawang'amua. brrrrr!!!!!
 
Back
Top Bottom