Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?

Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu hizi za kwa maslahi ya taifa ambazo ziko kwa mfumo wa maswali, halafu majibu utayatoa mwenyewe wewe msomaji.

Maswali ya leo ni Bunge Letu ni Bunge la Hovyo? Bunge Letu Linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika Aanze Kuita Watu Kwenye Kamati, au Waachwe Tuu?.

Maswali haya ni kufuatia mkutano wa jana na waandishi wa habari Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi



Baada ya kuzisoma hizo hoja, kabla sijaandika, nikatafuta kwanza clips ili kujiridhisha ni kweli maneno haya ameyamtaka kweli?, maana fani ya uandishi wa habari siku hizi imevamiwa, kuna waandishi wa habari wa kila aina kuanzia comedians, wasanii, na waandishi wengine wa hovyo sana, usipokuwa makini, sometimes waandishi hawa wa habari wa hovyo hovyo, hawachelewi kukulisha maneno!, hivyo nikamsikiliza mwanzo mwisho na kujirishisha kuwa ni kweli maneno hayo ameyasema, na sio tuu ameyasema, bali pia ameyaandika kwanza kisha akaja kutusomea sisi waandishi wa habari.



Kabla sijaendelea, naomba kuwakuwakumbusha wasomaji wangu, tujifunze kutofautisha definite statements na maswali. Hakuna statement kwenye bandiko hili, ni bandiko la swali! Natoa angalizo hili kwasababu mimi mwenzenu nimeisha wahi kuitwa all the way from Dar to Dodoma, kufika kule nikaulizwa kwanini umetoa hii statement? Nikajibu hiyo sio statement ni swali! Hivyo hapa nasisitiza hili ni bandiko la swali sio bandiko la statement!

Dr. Slaa ameliita Bunge Letu ni Bunge la Hovyo, na kilichofanyika kuridhia IGA ni uhuni? Ndio maana nauliza waungwana humu, hiki alichokisema Dr. Slaa kinaukweli kuhusu Bunge letu ni Bunge la hovyo?. Kilichofanywa na Bunge letu kuridhia IGA ya DPW ni uhuni?. Wanaofanya uhuni ni wahuni, jee Wabunge wetu ni Wahuni?.

Bunge letu Tukufu haliwezi kudhalilishwa hivi tukanyama! Je, tumshauri Madam Spika aanze ule utaratibu kama wa mtangulizi wake kuita watu kwenye Kamati, watu wowote watakao toa kauli za kulidhalilisha Bunge, au waachwe tuu kwasababu wanatoa maoni yao kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba kuhusu uhuru wa kutoa maoni?

Nashauri Daktari aitwe mbele ya Kamati!. Mimi nilipouliza tu, hili swali Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? niliitwa Bungeni kuhojiwa na kamati!, sasa leo Bunge linaitwa la hovyo! na kilichofanyika ni uhuni!, mtu huyu hawezi kuachwa hivi hivi tuu au aitwe mbele ya kamati kuthibitisha kauli yake?

Na ikitokea asipoitwa, jee hii haitaaminisha alichosema ni kweli?, ndio maana nawauliza waungwana humu, jee ni kweli Bunge letu ni Bunge la hovyo? Jee ni kweli kilichofanyika kwa Bunge kuridhia hii IGA ya serikali yetu na Mwarabu wa Dubai ni uhuni? Mtu anayefanya uhuni ni muhuni, jee waheshimiwa wabunge wetu ni wahuni?

Paskali

Mkuu

Wewe ni mwanasheria na wakili wa mahakama kuu unatambua fika utaratibu wa kumshughulikia balozi active na balozi mstaafu sawa na rais mstaafu endapo atakengeuka. Je, unafikiri Dk Slaa alikurupuka au alifanya kwa makusudi akijua matokeo yake na wale ambao ndio waroho wa kushughulika na watu hawafahamu udhaifu wao? Je, unataka hata siri ya chini ya tandiko la kitanda iwekwe hadharani kila raia aione? Je hicho kilichotokea kwa Dk Slaa kuongea ukweli wa kutoka kwenye jiko husika wewe unauonea wivu kisa ulishawahi kushughulikiwa na ukakaa kimya hadi leo hujawahi kutamka hadharani kitu gani ulichofanywa huko kwenye kamati inayoshika pumzi ya mhojiwa?

Haya makubaliano ya serikali na DP World yatawaumbua sana viongozi ikiwemo ninyi mnaochongea wengine kisa mklishawahi kushughulikiwa!! Ulitakiwa ukae kimya kisha uje kushitaki kwamba bunge liko 'Biased' kaika maamuzi yake huku ukiweka hadharani rejea za kuthibitisha lalamiko lako badala ya kuchongea wakati mwenizio kaongelea maslahi ya nchi, watu wake, rasilimali zake na historia ya Tanzania
 
P.
Makuzi yako kuanzia utoto Hadi ujana yalikuwa ya shida na taabu nyingi. Niamini. Haya unayoyafanya ni malipo kwa yake uliyotendewa utotoni yaani kusingiziwa na Sasa wewe unasingizia wengine!
Tafuta therapist akuvushe kwenye Hilo bonde.
Je, ni kweli kabisa husikii yanayoendelea nchini? Hujazisikiliza hoja za hao wawakilishi japo sijui wanamwakilisha Nani!
Mpe credit Dr. Slaa kwa kulivaa bomu kwa niaba ya wengi acha kumsakazia mbwa!
 
Wabunge ni hovyo, na wabunge ni wahuni.

Ila naunga mkono Dr Slaa aitwe kuhojiwa bungeni ili akawashushie nondo hawa mbumbumbu wanaojiita waheshimiwa wasiokuwa na heshima yoyote ile.
Wangekuwa wanarusha live hapo sawa bahat mbaya huyafanya hayo mahojiano gizani,hawatak wananchi wasikie,bado tuko mbali sana kidemokrasia na utawala bora,Kenya tu hapo mambo huwa wazi on Tvs
 
P
Yapi maoni yako kuhusu DP World?
Au na wewe umeshalambishwa bahasha?
Karibu sana.
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
 
Miaka michache iliyopita nilitembelea Nchi ya KUSADIKIKA kwenye Jamhuri moja hivi..

Bahati mbaya mwenyeji wangu alinipa mwaliko kutembelea Bunge hilo na kuona mijadala mbali mbali..

Cha ajabu na cha kusikitisha sikuona mijadala yenye fikra pevu Kwa Ustawi wa Taifa lao, Niliona Viroja na mipasho Tu huku pesa za walipa Kodi zikiteketea..

Sikuona Bunge,Niliona "Rubber Stamp" Tu ambalo wamekaa wahuni ndani humo Kwa nia "OVU' ya kula bila huruma pesa za Wananchi wao pasi na kuona soni

Kibaya zaidi Jamhuri Ile ya KUSADIKIKA ipo kwenye mkwamo wa masafa marefu WA fikra tata huku Jamhuri yao Ikiteketea chambilecho cha Marehemu Dr Remmy..

Tafakari
 
Back
Top Bottom