Bunge letu linapoteza hadhi!

Bunge letu linapoteza hadhi!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
  • Kama kila linalosemwa na Wabunge wa CCM ni jema na linapita wakati linalosemwa na Wabunge wa vyama vya upinzani linapingwa na kutupiliwa mbali,Bunge halina maana.


  • Kama Wabunge wa chama tawala wanaachwa kutumia lugha za kuudhi na wale wa upinzani wakitolewa nje ya Bunge na kutakiwa kuwasilisha maelezo,basi Bunge letu linakosa maana.


  • Kama ushahidi unaoletwa mbele ya Spika na Wabunge wanaotakiwa kuuwasilisha unafichwa na kunyamaziwa,Bunge letu linakosa mshiko.


  • Kama maazimio mbalimbali ya Bunge hayatekelezwi na yanapuuzwa,kuna maana gani ya kuwa na Bunge lenye nguvu ya kikatiba kuisimamia Serikali?


  • Ikiwa Wabunge wanakuwa mstari wa mbele kuongoza watu kupiga wenzao na kufanya vurugu(tukio la jana Dodoma),i wapi heshima ya Bunge?

Tujadili...
 
Mkuu ilo Bunge lishaozaa zamani tunasubiri tuu litoe harufu....
 
Dawa yake ni usajili wa gari hii T2015CDM basi utahuzika tena mkuu.
 
Hiyo laana wa kuitengua ni Mama maria Nyerere maana nadhani inatoka kwa baba wa taifa eti.
 
Mimi niliacha kulifuatilia muda mrefu sana, tangu aanze huyu binti sokela mimi na bunge baaaaaaaaaaaasi. Nasubiri usajili mpya mwaka 2015 labla tutapata wabunge na spika.
 
Bunge linastahili kuongozwa na mwanasheria. Sasa Makinda ni karani hawezi kujua sheria/ kanuni za namna ya kuliendesha.
 
bunge la kiitikadi si la kitaifa. chama tawala kinavutia kwao
 
Bunge legelege, lenye robotatu wabunge wa ccm, shauri yetu watz.
 
Kamwe sintocha kuwasikiliza maana wananiongezea ari nguvu na DHAMIRA YA DHATI KABISA kutokupiga kura kwa awaye yeyote katika chama cha mapinduzi kama kwao maaana ya mapinduzi ni kupindua kila jambo jema basi kauli yao maarufu ya MAPINDUZI DAIMA inaonekana katika haya yanayoendelea bungeni, kungekuwa na mwenye akili CCM angewaambia kuwa hili la upinzani ni jema ila kwa kuwa wote wamesahau ni heri pia, kwani hata mfale Louis wa Ufaransa alijisahau hivi hivi mwishowe akakosa kila kitu katika nchi yake.
 
Bunge hata King'wendu na Diamond, afande Sele, Wema, Wolper washatangaza kugombea unategemea nini?

Maazimia ya Bunge yanabuuzwa, Wapi maazimio ya Jairo!!
 
Nimekuwa nikifuatilia siasa za bunge letu tukufu kwa muda mrefu lakini uendeshaji wa bunge la kumi unakera, unakamia kulipiza visasi, kama umeelemea upande mmoja hivi, wabunge wanatukana wenzao , wanawadhalilisha .. viongoz wao kimyaah! et wafute kauli bhaasi. matukio ya hiv punde ya kusitishwa kwa bunge yamenishtua kidogo.. naomba kueleweshwa je muendelezo wa mnyukano wa hoja za upinzani dhidi ya zile za chama tawala, bila kujali kama zina maslah kwa taifa ama lah je ni Siasa za kuoneshana umwamba au ni kutojali kwa wabunge wa CCM na serikal yake? naomba ufafanuz barid wa suala hil nielewe vzuri maana hata wabunge wa upinzani wamekuwa wakipinga hoja za wenzao wa chama tawala lakini kwa hoja.., wakat wenzao wana2mia ubabe zaid! bado cjaelewa kuna nini behind bunge politics!! jamanie wanaojua naomba mnidadavulie!
 
Kwa kifupi kinachoendelea sasa bungeni ni mnyukano kati ya watetea haki kwa upande mmoja na watetea uovu kwa upande mwingine, kati ya watetea maslahi ya wananchi na watetea maslahi ya wateule wachache ndani ya sisiemu (na serikali), kati ya wawakilishi wa wananchi na wawakilishi wa chama tawala (na serikali yake).

Ni mnyukano kati ya wabunge wachache wanaojua shida za wananchi wanaowawakilisha bungeni na wengi ambao wameziba masikio (kwa kujua au kutokujua) na kugeuka kuwa watetezi wa serikali, kati ya 'wachumia tumbo' hata kama wanajiita first class economist na wachumi wa kweli, kati ya wale wanaona rasilimali za nchi na namna zinavyoweza kutumika kama vitega uchumi na 'vibaka uchumi'.

Ni mnyukano kati ya utandawazi na 'mtandaowizi', kati ya uhuru wa kuzungumza na 'uhuni' wa kuzungumza, kati ya wasomi wachache na watu waliowahi kwenda kupasha joto madawati shuleni. Ni mnyukano kati ya nuru na giza, kati ya chumvi na kitu kingine chenye ladha chungu.

Naam, yote haya yapaswa yatokee ili watanzania wajue ya kuwa kile chama walichokiamini (au kuaminishwa) kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi sasa ni chama cha mafisadi, wahamisha twiga na wauza pembe za ndovu. Chama ambacho tuliambiwa kuwa kinaamini kwamba binadamu wote ni sawa sasa kimebadilika na kuwa 'binadamu wote si sawa' maana kuna wanasisiemu na wapinzani, kuna wanamtwara na wanabagamoyo. Chama kilichosema rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa, sasa kinasema wagombea wake wote wanatoa rushwa kwenye chaguzi. Ile ahadi ya kuwa nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote, sasa elimu inatumika kwa 'faida' ya chama kwanza.

Hii ni sauti inayopazwa kwa mwito na mshindo mkuu kwa baba, mama, kaka, dada na wadogo zangu kule Namiyonga (Newala), Lumuma (Mpwapwa), Kinalilya (Iramba), Makere (Kasulu), Lubafu (Bukoba), Kabanga (Nzega) au Nkwarungo (Hai) na vijijini kote katika nchi hii, msidanganyike tena kwa pombe, tshirt, kanga au chumvi na kuuza haki zenu za msingi kwa makuwadi wa mafisadi.

Nionapo yote haya, najua kwa hakika mwisho wa mambo yote umekaribia. Naam, hata huo mwisho hauko mbali sana maana naoina Tz mpya yenye tumaini jipya. Naona anguko kuu la sisiemu, naye ajidhaniye amesimama aangalie asije akaanguka. Asomaye na afahamu!!!!!
 
Back
Top Bottom