Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Mwananchi yoyote wa kawaida tu aneunga mkono ccm na viongozi wake anastahili kupimwa akili!
 
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

__________

TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

______________​

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge.
Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti.
Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.

Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge.
Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi.

Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo.


Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati.
Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).


Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.


Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.

Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE​

Kwa mlipa kodi mimi naona kuna matumizi mabaya ya KODI yetu katika mpango wenu-Ofisi ya Bunge. TBC inaendeshwa kwa KODI zetu. Kwetu sisi wananchi tutakacho kuona ni nijadala LIVE ya wawakilisho wetu Bungeni.

Kama mnaongelea kuwezesha upashaji habari wa yae yanayojiri Bungeni kupitia njia za KISASA zaidi-u-tube na mtandanoni, sipingi suala hilo.


Kuna sababu gani kufungua TV ya Bunge running 24hrs times 365dys hali TBC inatupa kile tutakachokuona na KWA GHARAMA za kodi yetu? Acheni kutafuta njia za kuwa na kitengop ndani ya kitengo, ndano ya Taasisi! Multiplicity of efforts does not mean efficiency (hasa kwa mijizi yetu)
 
Watajibeba akina NAPE, COUDS Radio na akina Mrema, wapuuzi sana hawa watu!
 
Ivi alikua anatype mwenyewe? Mbona typing error nyingi na hakuna space?
Nahisi ni mwanzo wa wabunge wa chadema kuviziwa wamelala. Kamera zitakua zinawamulika muda wote.
 
Lakini kitakachofanyika ni kilekile, siku hizi technohama inawezesha kuhakiki matangazo huku yakiwa hewani na kisichotakiwa kusikika/kuonekana kikawa omitedbila mtazamaji kugundua.....So the bottom line is HATUTAKUWA TUKIPATA KILA KINACHOTENDEKA NDANI YA BUNGE.
 
Hakika Chadema Inatisha.Tamko la John Mnyika tu la Jana wamesalimu Amri.Ahsanteni sana Chadema.Mungu awabariki kututetea wanyonge.

Wewe inaelekea una matatizo makubwa sana ya kuelewa. Soma vizuri uelewe kilichoandikwa, halafu kumbuka swali nililokuuliza kuleee kuhusu redio.
Bado hujaielewa hii taarifa ya Bunge.
 
Lakini kitakachofanyika ni kilekile, siku hizi technohama inawezesha kuhakiki matangazo huku yakiwa hewani na kisichotakiwa kusikika/kuonekana kikawa omitedbila mtazamaji kugundua.....So the bottom line is HATUTAKUWA TUKIPATA KILA KINACHOTENDEKA NDANI YA BUNGE.

Watu wazito kuelewa. Wafafanulie waelewe. Yaani kilichosemwa ni kilekile ila lugha tu ndio tofauti na watu wameshachanganyikiwa.
 
mimi ninatafuta namba yake nimpe vitu vyake kama kawaida! na inasikitisha sana kuwa huyu jamaa ni lini alikuwa na akili?je ni siku ile anatangaza kuwa wamepanga kusitisha kuonesha vipindi vya bunge au ni leo anapoandika haya?
 
chezea chadema wewe!!kwa kumuumbua makinda &co tungeambatanisha na ile nakala ya kashilila alivyoongea na waandishi wa habari
 
Lakini ukiisoma vema hiyo statement yao bado kuna mtego. Watakachokuwa wanafanya ni wao wenyewe Bunge kupiga picha na kurekodi sauti na kisha kuwapa waandishi link ya kurusha watakavyo. Trick ipo hapo kwenye kupiga p[icha na kurekodi, tuna uhakika gani watapiga picha zile ambazo watu watataka kuziona? Si ajabu Chadema watakapoamua kusimama tena kushinikiza hoja zao hatutaziona picha hizo, au Tundu Lissu atakapokuwa anampa Spika vidonge kwa kusigina kanuni, tunaweza tusiwekewe hiyo sauti


Mkuu uko sawa kabisa, hayo yatakuwa mambo ya ku edit ndio wawapatie watu wenye makampuni ya runinga waonyeshe. Itakuwa vizuri wakiendelea na huo mpango uliopo sasa hivi hayo maboresho yao ni yakichina.
 
tuwe makini na hawa duduwasha sisiem kuna mbinu kali zinatumika ku edit matangazo kwa kutumia studio zao na watangazaji watakaokuwa wanefunzwa vyema.tukatae studio ya bunge as soon as possible!!
 
Hii sio taarifa ya bunge trust me,haina vigezo vya uandishi wa taasisi kubwa kama ile na wala haina muhuri wa ofisi ya bunge halafu imeandaliwa haraka haraka tu bila hata kueditiwa,wanachoogopa ni nini hasa hawa watu? Mwenye video ya Kashilila siku alipokuwa anatoa hizo taarifa akiwa ofisi ndogo ya bunge pls aitupie humu tumjaribu kulinganisha haya maneno pls actufanye sio mazuzu
 
Jamani,

1. "Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini na kuwasajili"....Lengo hapa ni nini? Mwandishi msemakweli atasajiliwa kweli?

2. Bunge kulinda heshima na maadili ya utangazaji? Kweli? Si kuna mamlaka husika? Hawa jamaa hawana lengo la kuruhusu matangazo ya bunge kurushwa live? Bado wanataka kuchuja (censor) ili watakachoona wananchi kiwe ni kile ambacho wao wameridhia.

Hii statement inapigia msitari kile alichokisema Kashililah kwenye kikao na waandishi wa habari.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

__________

TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

______________​

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge.
Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti.
Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.

Hivyo basi utaratibu uliopo sasa
utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge.
Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi.

Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge
hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo.


Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani
yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati.
Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

Aidha ili kulinda heshima na
maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati,
bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).

Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.


Tunasikitika kwa usumbufu
uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.

Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE​


Du, hivi huyu ndiye Dr. Kashilila, katibu wa bunge lenu na taarifa yake. Hivi huyu jamaa anaweweseka na ----- alioueneza ama nini, hebu angalieni kwenye maeneo niliyoweka alama nyekundu (RED) kwenye taarifa yake muone DR wenu alivyo kisha mlinganishe na uendeshaji wa Bunge.

Pia pale penye bluu (BLUE), anasema bila kuegemea popote. Je kilichowafanya mtangaze kusitisha matangazo si ni ili muegee kwa mafisadi zaidi!! Watanzania sio mabwege ki-hivyo.
 
Hakuna kitu kinachoitwa RTD hapa Tanzania kwasasa. Kwahiyo,taarifa ya kusitishwa matangazo ilizuliwa na nani? Atasikitikaje aliyeitoa mwanzoni? Sio hivyo jamani...

Halafu Radio STAR ndiyo ipi? Ama kweli Dr Kashilila kaipata, alikubali kutumika sasa anaona wanasiasa walivyo, wamemruka na kumwagiza kufuta kauli yake.
 
Viongozi wanatembea na vipima upepo, huufuata upepo kule unakoelekea. zama zileeee za merikebu za upepo.
 
Ni aibu kubwa kwa bunge kuongozwa kiujanjaujanja namna hii. Kashillila hakusema nani alimnukuu vibaya na alimnukuu nini. hajui anachosema anajaribu kukanusha kisichokanushika. aibu kubwa kwa taasisi kama Bunge kuongozwa kiccm au kichadema. mbona amegeuka sasa, angenyamaza aone nguvu ya umma
 
Katikisa kibiriti akakuta kimejaaaaa tele wala hakitikisiki?
 
Back
Top Bottom