"Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati. Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe." sidhani kama nimeelewa maana yake wadau nisaidieni hapa