Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Mpaka msokolwe ndo mnageuka!bora kujiajili...kuishi kwa mishahara inayotokana na kodi za watu ni utumwa!ona sasa Dr.Kashilila kabadili msimamo!misuli yote ya jana leo kasalimu amri!aibu mbele ya mke na watoto!mana ni baba anayetishwa na tamko la kamanda JJMNYIKA....ila hapo pa kuzuiwa waandishi kuingia ndani na badala yake kutumia picha zilizopgwa na camera za Bunge!sio hapo ndo tunapigwa changa la macho?
 
Ilisemwa hapa kuwa huyu Jomba atarudi na kukana kauli yake au kusema alinukuliwa vibaya.

Na kweli yametimia.
 
Kusema NImenukululiwa vibaya nayo ni matusi makubwa kwa wanahabari, ni kuwafanya wanahabari mazezeta
 
Halafu hiyo taarifa ameandika kama anakimbizwa maneno yameungwa ungwa hovyohovyo tu! Chezea Chadema wewe!
 
Lakini ukiisoma vema hiyo statement yao bado kuna mtego. Watakachokuwa wanafanya ni wao wenyewe Bunge kupiga picha na kurekodi sauti na kisha kuwapa waandishi link ya kurusha watakavyo. Trick ipo hapo kwenye kupiga p[icha na kurekodi, tuna uhakika gani watapiga picha zile ambazo watu watataka kuziona? Si ajabu Chadema watakapoamua kusimama tena kushinikiza hoja zao hatutaziona picha hizo, au Tundu Lissu atakapokuwa anampa Spika vidonge kwa kusigina kanuni, tunaweza tusiwekewe hiyo sauti

hata picha za yale yanayosinzia kama Captain au Wasira hazitarushwa...
 
Yeah hadi tuwashukie kwanza kama mwewe ndio mnageuka.. smart move.. msiwatishe wananchi hivi...


Cheki ameandika RTD (Sijui ni kitu gani). Kusema NImenukululiwa vibaya nayo ni matusi makubwa kwa wanahabari, ni kuwafanya wanahabari mazezeta
 
.... Usisahau radio Mawingu na kipindi chao, sijui wanaita jicho la ng'ombe.!

Umenikumbusha.Hii Radio Clouds iliyoshadadia ujinga huu sijui watangazaji wake watajificha wapi.
 
ila i sense censorship motives on the way kuna uwezekano kukawa na ubanaji wa baadhi ya matukio! Kw mfano kwa kutoruhusu camera kuingia bungeni ina maana hatutawaona wakina Lyatonga na Wasira wakimwaga udenda ndani ya Bunge maana recording itafanywa na wafanyakazi wa Bunge! na watakuwa na uwezo wa ku-scip baadhi ya matukio yenye kubana maslahi ya serikali!
 
code of conduct!!nani anayeiweka ?
Hapa naona kuna dalili ya kuminya haki ya kupata habari!
 
Ina maana KASHILILAH ULINUKULIWA VIBAYA?
Walikuwa wanapima maji kwa mti, wakagundua yamejaa. Hata kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali huwa wanalikisha habari kusudi ili wasikie maoni ya wengine, wakiona anakubalika wanendelea ila wakiona anapingwa sana wanabadili
 
Nasubiri Jicho La Punda Cloudz fm (radio ya WAFU) jumatatu yule mpuuzi Hando atasema kipi, maana napata mashaka na hata uwezo wake wa kushughulikia hata masuala ya ndoa yake (kama ipo). Hawa WAFU na radio yao ni vilaza kupita maelezo, sijui HANDO na PJ mmenisikia, (hata kama sio ID zenu)
 
Last edited by a moderator:
CHEZEYA CDM weye...., CCM navurugwa,naogopa yeye gwanda kama zazi yake.
 
Poor Kashilila!!! Ulikuwa unabeep watu??? Unakimbia kivuli chako mwenyewe???
 
Wakuu hivi hii ndio LIVE ????




​
Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge


Hapo tunaonaje kina Wassira waliozoea kulala ?


Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.


Ukienda vingine na wanavyotaka wao basi fahamu kwamba utaondolewa kwenye hii shughuli

Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi.

Hizi code of conducts si ndio kubana watu kuonyesha baadhi ya vitu na kuacha baadhi ?


In short hii hatua ni kuwabana waandishi kurusha kile wanachotaka wao, in short hili Bunge la huyu mama limekuwa Bogus sababu ya uongozi mbovu
 
Kwanini Dr Kashilila alianzisha hoja ambayo hata mtoto wa darasa la 7 angeweza kujua yangezua sokomoko? Tayari damage imeshatokea, na hili kanusho haliwezi kuondoa hisia mbaya na chuki dhidi ya mwelekeo wa uongozi wa bunge.

Siku nyingine wawe makini, watanzania wa leo sio wa mwaka 47.
 
Back
Top Bottom