Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Mbunge Nadine Dorries wa chama cha wahafidhina nchini Uingereza amesema kuwa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu David Cameron pamoja na serikali yake ya muungano iko jikoni na huenda ikawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura wakati wowote kutoka sasa.
Mbunge huyo amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya Cameron kukosa kutekeleza ahadi aliyotoa kwamba angeandaa kura ya maoni ili Waingereza waamue iwapo wanataka kubakia au kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Nadine Dorries amesema kuwa jambo lingine lililopelekea wahafidhina kuanda muswada huo ni hatua ya Cameron ya kubadilisha sheria za haki za binadamu na hivyo kutoa nafasi kwa polisi kuwahangaisha wananchi kwa kisingizio cha kulinda usalama wa taifa.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la Daily Mail umeonyesha kuwa Cameron amepoteza umashuhuri kwa kiwango kikubwa nchini Uingereza na kwamba kwa sasa ni asilimia 33 tu ya Waingereza ndio wanaomuunga mkono.