Nimefuatilia sana Bunge hili na kugundua lipo nyuma sana kwa mahitaji ya sasa. Serikali imejitahidi sana kubadilisha mambo mengi kuanzia mazingira ya biashara, utalii, miradi, Kilimo, siasa na mahusiano ya nchi za nje. Lkaini Bunge ni kama vile halijitambui . Kwanza Spika hajiamini na hana uhusiano mzuri na Mama yaani hakuna sehemu spika ananuna kama akienda Ikulu. Pili wabunge wengi hawana upeo na kasi ya Raisi. Wabunge wamejikita zaidi kwenye kusifia au kulalamika badala ya kutoa mapendekezo kiasi kwamba hata Raisi mwenyewe anaona Bunge halisaidii chochote. Lakini kikubwa zaidi wananchi haliamini Bunge na kuona kama ni sehemu ya vihoja. Ushauri wangu hawa Wabunge wasitumike kwenye mchakato wa katiba kabisa. Itafutwe timu ya kitaalamu na watu wenye uzoefu kushughulikia katiba sio hawa wakina Tulia ambao wanafikiria uchaguzi kila siku na hawapendeki na hawakubaliki huo ndiyo ukweli. Nashauri kwenye katiba mpya Raisi aruhusiwe kuteua waziri nje ya ubunge ili tupate viongozi bora badala ya bora viongozi